MUSOMA.
Jumla ya Tsh12,770,831,000 imetengwa kwa ajili ya matengenezo ya mbalimbali ya barabara na madaraja mkoani Mara ambapo jumla ya kilomita 1,552.18 na madaraja 60 yalifanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali. Pia serikali imetenga jumla ya 21.8 millioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye barabara mbalimbali ambapo kilomita 2.2 zitajengwa kwa kiwango cha lami na kilomita 45.5 za changarawe zitakarabatiwa.

Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara Eng. Emmanuel Korroso ameyasema hayo wakati akiwasilsha taarifa ya utekelezaji na njia za mapendekezo ya bajeti sambamba na miradi kwenye kikao cha wajumbe wa bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji kilchofanyaka kwenye ukumbi wa uwekezaji wa mkoa wa Mara januari 20 mwaka huu.
Aliongeza kuwa jumla ya fedha iliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni Tsh.14,915,701,00.00 kwa ajili ya matengenezo na kazi za miradi ya maendeleo.Fedha hizi ni ongezeko la asillimia 4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2012/2013.
‘’hadi kufikia mwisho wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2013/2014 utekelezaji wa kazi za matengenezo ulikuwa umefikia asilimia 66.’’ Alisema.
Kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa kitaifa Kossoro ameongeza kuwa serikali imetumia jumla ya bilioni 85.363 kwenye ujenzi wa barabara kuu ya Lami itokayo Manispaa ya Musoma Mkoani Mara hadi Mkoani Simiyu.
“Kati ya kilomita 85.5,kilomita 74 zimekamilika ukarabati na ukarabati huu unahusisha madaraja mawili makubwa ya Suguti na Rubana ambayo tayari yamekamilika.pia mradi huu unatekelezwa na kampuni ya kichina ya M/S CHIKO chini ya mhandisi mshauri wa mradi huo ambaye ni Consuliting Engineering Services (India) private ikishirikiana na NORPLANT (T) LTD Kampuni ya kizalendo” Aliongeza.
Mwisho…… …………………………..
0 comments:
Post a Comment