`

Home » » WAFA WAKATI WAKIIBA

WAFA WAKATI WAKIIBA

Musoma:

Watu Wanne Wanaosadikiwa Kuwa Ni Majambazi Wamevamia Duka La Rehema Idd (24) Mkazi Wa Nyakato Manispaa Ya Musoma Mkoani Mara Na Kufanikiwa Kumpora Shilingi Milioni Moja Na Laki Nane Pamoja Na Simu 40 Za Aina Mbalimbali Zikiwemo Vocha Ambazo Thamani Yake Bado Haijajulikana.

Mashuhuda Wa Tukio Hilo Wamesema Kuwa Tukio Hilo Limetokea Januari 6 Saa Mbili Usiku Mwaka Huu Ambapo Watuhumiwa Hao Walitumia Silaha Aina Ya Gobore Kumnyang’anya Rehema Kiasi Hicho Cha Fedha.

Wamesema Baada Ya Tukio Hilo Wananchi Waliokuwa Jirani Na Eneo Hilo Walipiga Kelele Na Kuanza Kuwafukuza Watuhumiwa Hao Ambapo Walifanikiwa Kumkamata Mmoja Aliyekuwa Na Silaha Na Kwamba Walimshambulia Hadi Kufa.

Aidha Walisema Wananchi Hao Walifanikiwa Kukamata Bunduki Aina Ya Gobore Na Risasi Mbili Za Shotgun Na Kwamba Aliyeuawa Katika Tukio Hilo Alitambulika Kuwa Ni Marwa Gimonge (40) Mkazi Wa Kijiji Cha Gibeyo Wilaya Ya Tarime Mkoani Hapa Na Mwili Wake Umehifadhiwa Hospitali Ya Serikali Mjini Musoma.

Wakati Huohuo, Mkazi Wa Kata Hiyo Eneo La Mlimani Akuku Aringo Miaka (47) Ameuawa Kwa Kuchomwa Moto Baada Ya Kukatwakatwa Kwa Mapanga Kichwani, Na Sehemu Mbalimbali Za Mwili Wake Na Wananchi Wenye Hasira Kali Kufuatia Kutuhumiwa Kuiba Mihogo Katika Shamba Ambalo Mmiliki Wake Bado Hajajulikana Jina Lake.

Tukio Hilo Lilitokea Januari 6 Saa Kumi Na Moja Na Nusu Jioni Maeneo Ya Kijiji Cha Mkirira Kata Ya Nyegina, Tarafa Ya Makongoro Wilaya Ya Butiama Huku Aliyeuawa Alikuwa Ni Mwendesha Pikipiki Maarufu (Bodaboda)

Jeshi La Polisi Mkoani Mara Limethibitisha Kutokea Kwa Matukio Hayo Na Tayari Limeanza Upelelezi Na Linawashikiria Watu Wanane Wanaohusika Tukio La Wizi Wa Kutumia Silaha.

Hata Hivyo Kamanda Wa Polisi Mkoani Hapa Ferdinand Mtui Ametoa Mwito Kwa Wananchi Kutojichukulia Sheria Mkoni Badala Yake Amewataka Kutoa Taarifa Kwenye Vyombo Vya Dola Mara tu Wanabowabaini Wahalifu.


Mwishoooo...

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK