`

Home » » THOM OLABA AANZA KAZI RASMI LEO NI KOCHA MPYA WA RUVU SHOOTING

THOM OLABA AANZA KAZI RASMI LEO NI KOCHA MPYA WA RUVU SHOOTING

KOCHA MPYA wa ruvu shooting leo ameanza kazi kwaajili ya kuitumikia timu hiyo katika raund ya pili ligikuu soka tanzania bara kwa kutembelea mazoezi mepesi ya timu hiyo katika uwanja wa mabatini mlandizi mkoani pwani.

Akizungumza na busati la michezo hii leo msemaji wa klabu hiyo masau bwire amesema pamoja na kuanza kazi hiyo lakini anachokitaraji kikubwa na nidhamu toka kwa wachezaji hao  pamoja na ushirikiano ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.

Masau amesema kuwa ujio wa kocha olaba unatazamiwa kuwa na mafanikio makubwa hususan katika mzunguko wa pili wa ligi inayotaraji kuanza jan 25 mwaka huu.

Ameongeza kuwa kocha huyo aliyewahi kuwika katika klabu mbali mbali afrika mashariki anatazamiwa pia kuleta mabadiliko makubwa katika soka la kitanzania na afrika mashariki pia.


                       KOCHA MPYA WA RUVU SHOOTING (PICHANI).

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK