Rorya:
Chama cha mapinduzi (ccm) kimesema hakitasita kuwasema
na kuwafikisha kwenye vikao vya maadili watumishi ambao watashindwa kufanya
kazi zao na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kupelekea
kulalamikiwa na wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa maazimisho ya miaka 37
ya chama cha mapinduzi ccm wilayani rorya,mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa
geita Joseph Kasheku amesema
wataizingatia kauli ya rais jakaya kiwete aliyoitoa mkoani mbeya kutomuonea
aibu mtumishi na kufatilia kwa karibu utekelezaji wa ilani.
Kasheku amesema kamwe hawatokubali kuona watumishi wazembe
na wanaojiingiza kwenye siasa kukwamisha shughuli za maendeleo kwa kutosimamia
miradi huku shutuma zikielekezwa kwa serikali ya ccm.
Msukuma amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka
taarifa za kuhusu chama cha mapinduzi (ccm) wilayani rorya kulalamikia utendaji
kazi wa mkuu wa wilaya hiyo pamoja na mkurugenzi na kusema ili kazi ziweze
kwenda ni lazima viongozi wa ccm wawe wakali katika kusimamia ilani.
Mwenyekiti huyo wa ccm mkoani geita ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika maazimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa
nyanduga, amewataka viongozi wa ccm wilaya ya rorya kutokusita kuzungumza kila
wanapoona uzembe wa watumishi.
Mwisho.....
0 comments:
Post a Comment