Home »
» JAMBAZI MUUAJI AUAWA TARIME, NA LINGINE LAKAMATWA MKOANI TANGA.
JAMBAZI MUUAJI AUAWA TARIME, NA LINGINE LAKAMATWA MKOANI TANGA.
Na Dinna Maningo,
Tarime.
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kwa kushirikiana na kikosi kazi Wamefanikiwa kukamata watu wanaojihusisha na mtandao wa Ujambazi akiwamo jambazi sungu Charles Range Kichune (38) ambaye anadaiwa kuhusika na mauwaji ya watu ya hivi karibuni Tarime ambapo mtu mwingine kwa jina Marwa Keryoba (30-38) emeuwawa kwa kupigwa risasi na Askari polisi kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Musoma Mjini.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisema kuwa mnamo Tarehe 7 February 2014, majira ya saa 1.45 asubuhi katika kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Musoma Mjini Mkoani Mara Mtu aitwae Marwa Keryoba(30-38) mkazi wa Kebeyo Sirari Wilayani Tarime aliuwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi.
Kamanda Kamugisha alisema kuwa Marehemu alipigwa risasi baada ya askari polisi kufika karibu na nyumbani kwake na yeye kushituka na kuanza kukimbia huku akiwa amebeba silaha aina aina ya SMG ambapo Askari Polisi walipiga risasi hewani wakimtaka ajisalimishe lakini alikahidi amri hiyo na kuanza kuwarushia risasi askari na ndipo Askari waliendelea kurusha risasi na hatimaye kumpiga risasi.
Kamugisha aliongeza kuwa Marehemu ameuwawa kutokana na taarifa zilizopatikana toka kwa mtuhumiwa mwenzake aitwae Charles Range Kichune kwa jina lingine Charles Josephat Msong,o au Josephat Chacha (38) Mkazi wa Kijiji cha Kenyamanyori Kata ya Turwa Wilayani Tarime aliyetoroka na kukamatiwa Mkoani Tanga jioni ya tarehe 6 February 2014 saa mmoja na nusu jioni.
Kamugisha alisema kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kujihusisha na Matukio ya mauwaji na Unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyotokea Wilayani Tarime kuanzia usiku wa tarehe 25 hadi 21 january na katika mahojiano ya wali na Jeshi la Polisi anakiri kuhusika na matukio hayo pamoja na wenzake.
“ Mahehemu alipigwa risasi baada ya kuombwa ajisalimishe badala yake akaanzakurusha risasi na ndipo alipopigwa risasi na akafa njiani akiwa anapelekwa hospitali kwa matibabu, tulikuwa tunamuhoji mtuhumiwa aliyekamatiwa Tanga akasema siraha iko kwa rafiki yake Musoma kweli akakutwa na silaha SMG ikiwa imefutwa namba na imekatwa mkono”alisema Kamugisha.
Anaongeza” Nyumbani ndani kwa Marehemu vimekutwa vitu mbalimbali vikiwamo CD, simu za mkononi, msako huu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunavunja mtandao wa wezi na hadi sasa tayali watu 8 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime kwahiyo wananchi wawe na amani “alisema Kamugisha.
Kamugisha alisema kuwa Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya linatoa shukrani kwa wananchi wa Wilaya za tarime na Rorya na Mikoa ya Mara na Tanga kwa ushirikiano walioutoa katika kuwezehsa kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambapo pia anaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi kutoa taarifa za wahalifu ambapo zawadi ya milioni moja iatolewa kwa mtu atakayetoa ushirikiano na polisi.
Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
0 comments:
Post a Comment