Musoma.
IMEELEZWA kuwa sababau kubwa inayochangia wanafunzi kufeli masomo ya
kuingia kidato cha kwanza ni kunatokana na
mgogoro uliopo baina ya wazazi na walimu hususan wanapotoa adhabu kwa wanafunzi hao.
Kauli hiyo imetolewa leo na madiwani wa halmashauri ya Musoma
kwenye kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Diwaniwa wa Viti Maalum bi. Debora Mogaya alisema kuwa
kinchochangia ni wazazi kutotoa ushiriano na walimu kwa kuhakikisha watoto
wanafika shuleni na sio walimu kukaa muda mrefu kama alivyosema diwani wenzake
wa kata ya Bulinga Mambo Japan kuwa
walimu kukaa muda mrefu na walimu kupewa vyeo vya ualimu Mkuu wa Shule za
Msingi bila kuwa na sifa hiyo.
“Wanafunzi waliofelini wale ambao hufanya utoro wa kutoenda
shuleni mara kwa mara ,hivyo inatupasa sisi viongozi tufanye mazungumzo na
wazazi na walimu wetu ili tubaini tatizo la elimu’’,AlisemaDiwani Debora.
“Wazazi na walimu
wetu ni mgogoro sana ambayo inamfanya
mwalimu kuwa na ugumu wa utendaji wa kazi hasa pale anapomuadhibu
mwanafunzi”,alisisitiza tena.
Naye diwani wa kata Bukumi Chomya Ndege alimuomba Afisa
elimu wa Halmashauri hiyo kuwasimamia walimu ili kutatua migogoro na kuboresha sekta ya elimu ambayo
ni msingi wa maisha wilayani humo.
“Mitaala nayo inachangia ,zaman iilikuwa aihamihami hivyo
tunaiomba serikali kuu kulingalia hili kwani inachangia pia’’,Aliongeza Ndege.
Awali hoja hiyo ilitaka kuleta mtafaruku baina ya Diwani wa
kata Bulinga Mambo na Afisa Elimu wa halmashauiri Magesa , diwani akidai kuwa walimu Wakuu wakipewa vyeo hivyo bila kuwa na sifa kutokana na
Afisa elimu huyo kupewa rushwa ambapo Afisa Magesa alimtaka diwani huyo
kumuomba radhi ama kumdhibitishia ukweliwa jambo hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amewaomba madiwani hao kufuata
taratibu ni kanuni za uendeshaji wa vikao ili kutatua mapungufu yanayojitokeza
na kwamba kikao cha baraza la madiwani
ni kujenga na sio kubomoa hivyo amewataka kutumia busara zao kwa lugha ya
ustaraab badala ya kutumia lugha za matusi
kwa watumishi.
Amemtaka Diwani Mambo kumuomba radhi Afisa elimu huyo
ilikuendelea ama kuweka kikao vizuri
ambapo diwani huyo alimuomba
radhi na kikao kikaendelea kuda ikuwa Afisa Magesa ndiye wa kulaumiwa
kwani yeye ndiye mtendaji Mkuu katika Sekta hiyo ya elimu.
Kwa upande wa
Mkurugenzi Mtendaji Fidelica Myovela alisema wamejiwekea mkakati wa kuzungumza na walimu na kwamba
kutokana mila na desturi zinasababisha kuwa kwamisha zinawavyunja moyo hali inayowasabisha kuomba uhamisho.
Mwisho.................
0 comments:
Post a Comment