KATIBU Tawala wa Mkoa wa Mara Benedict Ole Kuyani amewataka wadadisi na Wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 kutumia vizuri mafunzo waliyoyapata kwa makini na madhubuti kama walivyoahidi katika kuwaelimisha wadadisi watakaoshiriki kukusanya takwimu za utafiti.
Hayo ameyasema leo wakati akifunga mafunzo hayo ya zaidi ya wiki mbili yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa Afrilux mjini Musoma mkoa wa Mara.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni mbinu za kuhoji namna ya kujaza dopdoso katika ngazi ya Kaya ,kuhakiki na kutunza madodoso kwa makini kwa kujaza taarifa sahihi kwa kudhibiti ubora wa takwimu zitakazokusanywa.
Alisema kuwa watambue kuwa serikali imewapa dhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa wanapata mafanikio katika zoezi hilo la utafiti na kwamba kipimo cha mafanikio ya kazi yao kitaonekana dhahiri wakati wa utoaji wa matokeo ya utafiti huo.
“Juhudi zenu ndizo zitakazosaidia kupatikana kwa takwimu bora na sahihi za soko la ajira nchini ambazo zitatumika katika kupima na kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika soko ili kuwezesha serikali kuboresha sera na program za kukuza ajir, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleokama vile Mlengo ya Millennia,dira ya maendeleo ya Taifa yas mwaka 2025 kwa Tanzania Bara na malengo ya MKUKUTA”,Alisema Kayani.
Amewaomba viongozi wote wa serikali katika ngazi pamoja wananchi kutoa ushirikiano wakujibu maswali yatakayoulizwa na viongozi kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa kushirikiana na wadadisi na wasimamizi wa utafiti katika maeneo yatakayohusika.
Meneja wa ofisi ya Takwimu wa mkoa wa Mara Ramathan Mbega alisema kuwa wadadisi hao wamefuzu vya kutosha juu ya usomaji wa ramani za maeneo ya kuhesabia watu na namna ya kuchagua sampuli ya wanakaya watakaohojiwa dodoso la utafiti wa matumizi ya muda na wameshiriki kweenye mazoezi ya vitendo baadhi ya maeneo ya mjini Musoma na Butiama.
Amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wakati wa kukusanya takwimu za hali ya soko la ajira ili serikali iwe kupata takwimu sahihi na zenye ubora kama ilivyokusudiwa.
Ameahidi kuwa taarifa zitazokusanywa kutoka katika kaya pamoja na binafsi za wanakaya zitatunzwa kwa usiri mkubwa kwa mujibu wa sheria ya takwimu sura 351 ambapo matokeo ya utafiti huo yatasaidia kupatikana viashiria vya takwimu za soko la ajira nchini kama ukosefu wa ajira kwa makundi mbalimbali ya jamii,ajira isiyo timilifu,ajira isiyo sekta rasmi,ushiriki katika kazi kwa wanawake na wanaume na utumikishakji wa watoto.
Mwishoo........
0 comments:
Post a Comment