NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani Jeshi la Polisi Pereira Silima amesema kluwa msaada wa jengo la kituo cha polisi kilchojengwa na Kampuni ya Singita Grumeti Reserves utongeza kasi ya kubaini uharifu endapo wananchi watatoa ushirikiano.
Aliyasema hayo leo(jana) wakati wa makabidhiano wa jengo la la kituo cha polisi cha Natta katika eneo la kituo hicho katani hapo.
Silima alisema kuwa endapo wananchi hao hawatatoa ushirikiano kwa jeshi la polisi hakuna kitakachofanyika kitu ingawa kungaliko kituo hicho cha kisasa na kwamba bila ushirikiano kuwepo hali itaendelea kuwa tete, ‘’Kwa mujibu wa ibara 27 alisema kuwa katika kazi ya ulinzi ni watu wa nchi ya Tanzania ndio walinzi shirikishi wa jamii,’aliongeza Naibu Waziri huyo.
Aliwataka wananchi kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi jamii ambao utasaidia na kutumika kuongeza ulinzi na usalama ambapo aliwashukuru wananchi pia kwa kutoa taarifa za watu wa harifu ambazo zimeweza kusaidia kuwakamata waharifu.
Amewashukuru Grumeti kwa kufanya ujenzi wa kituo hicho na kwamba ujenzi huo ni moja ya mikakati iliyowekwa katika utekelezaji wa serikali ambapo alisema uewepo wa kituo hicho kutasaidia kuongeza ulinzi na usalama katika eneo hilo na lazima imalike zaidi.
Akizungumzia suala la uzagaaji ovyo wa siliha zinazofanya uharifu hasa mkoani Mara alisema serikali imejipanga kikamilifu na kuhakikisha unadhibiwa kwa kufanya doria na misako maalum na kuwataka wananchi kuwaheshimu askari wanapofanya kazi zao.
Alisema serikali imekusudia kufanya maboresho katika sekta zote kwa kufanya mabadiliko ambayo yanaendana na wakati ambapo mkakati huo ulianza mwaka 2006 na sasa ni mwaka wane katika utekelezaji ili kupanua mawazo na kuwa jeshi la kisasa na linaloendeshwa kiueledi na kuhakikisha wanapata elimu.
mwishoo..........
PEREIRA SIRIMA
0 comments:
Post a Comment