MUSOMA.
SERIKALI IMEANZA KUCHUKUA HATUA ZA
HARAKA ZA KUKABILIANA NA TATIZO KUBWA LA UGONJWA WA ZAO LA MUHOGO MKOANI MARA
AMBAO UMESABABISHA MAENEO MENGI KUKABILIWA NA NJAA KALI.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA SERIKALI
MTUMISHI KUTOKA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA AMBAE NI MRATIBU WA
TAIFA JUKWAA LA BIOTEKNOLOJIS NCHINI BW. PHILIBERT NYINONDO AMESEMA WAMEKUWA
WAKIPOKEA TAARIFA ZA MKOA WA MARA KUHUSU NJAA YA MARA KWA MARA KUTOKANA NA
MAGONJWA YA ZAO LA MUHOGO KUWA NI ZAO KUU LA CHAKULA.
AMESEMA KUWA PAMOJA NA JUHUDI ZA
SERIKALI MKOANI MARA ZA
KUHAKIKISHA WANAFANYA KILA LIWEZEKANALO KUTOKOMEZA UGONJWA HUO,LAKINI ZIMEGONGA
MWAMBA HIVYO SERIKALI IMEAMUA KUANZA KWA UTAFITI ILI KUJUA CHANZO CHA UGONJWA
HUO NA SABABU ZA KUENDELEA KUSHAMIRI.
KWA UPANDE WAKE AFISA KILIMO NA
MTAFITI MKUU KUTOKA KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO BW. JOSEPH NDUNGURU,
AMESEMA KUWA KUFUATIA HALI HIYO KUNA NJIA AMBAYO WAMESHAIGUNDUA KUWA NDIO NJIA
MWAFAKA YA KUKINZANA NA UGONJWA HUO AMBAYO KABLA YA KUANZA KUTUMIKA NI LAZIMA
ELIMU ITOLEWE KWA WAKULIMA NA VIONGOZI WAWE NA LUGHA MOJA YA KUTOKOMEZA UGONJWA
HUO.
NAE AFISA KILIMO MKOA SAMWELI SASI,
AMESEMA SERIKALI IMEFANYA JAMBO LA BUSARA KUSAIDIA KUONDOA TATIZO LA MAGONJWA
YA MAZAO MASHAMBANI HASA ZAO LA MUHOGO AMBALO NDIO ZAO TEGEMEO LA CHAKULA
KATIKA MKOA WA MARA.
AFISA KILIMO HUYO WA MKOA WA MARA
AMESEMA KUWA ZAO LA MUHOGO LIMEKUWA LIKISHAMBULIWA NA UGONJWA WA BATOBATO KALI
NA MICHIRIZI YA KAHAWIA HIVYO KWAMAENEO AMBAYO HULIMA MIHOGO KUSHINDWA KUPATA
CHAKULA HIVYO KUKUMBWA NA NJAA KILA MWAKA.
MWISHOO...
0 comments:
Post a Comment