TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBA NA RUSHWA MKOANI MARA TAKUKURU
INAMSHIKILIA MWEKA HAZINA WA MANISPAA YA MUSOMA BW. LIVINGSTONE KAHWA KWA
TUHUMA ZA KUDAI RUSHWA YA NGONO TOKA KWA MSICHANA ALIYETAKIWA KULIPWA POSHO YA
SH. ELFU 40 BAADA YA KUFANYA KAZI YA UKAGUZI WA LESENI YA BIASHARA KWATIKA MUDA
WA ZIADA.
AWALI BINTI HUYO ALIYEFIKA KATIKA OFISI ZA TAKUKURU NA
KUTOA MALALAMIKO YAKE KWAMBA ALIPOKUWA KATIKA MAFUNZO KWA VITENDO KATIKA IDARA
YA FEDHA NA BIASHARA YA MUSOMA ALIFANYA KAZI YA UKAGUZI WA LESENI ZA BIASHARA
AKISHIRIKIANA NA WENZAKE KATIKA IDARA HIYO AMBAPO ALITAKIWA KUPATIWA POSHO YA
SH. ELF 40.
AIDHA MSICHANA HUYO ALIFUATILIA MALIPO HAYO KWA MWEKA
HAZINA WA MANISPAA YA MUSOMA BW. LIVINGSTONE AMBAYE ALIWEKA SHARTI LA KUPEWA
NGONO NDIPO AIDHINISHIWE MALIPO HAYO NA NDIPO MSICHANA HUYO ALIPOAMUA KUTOA
TAARIFA HIZO KWA TAKUKURU.
MARA BAADA YA TAKUKURU KUPOKEA TAARIFA HIZO NDIPO
WALIPOAMUA KUWEKA MTEGO KWAAJILI YA KUMNASA MWEKA HAZINA HUYO KATIKA ENEO LA
KAMUNYONGE AMBAPO MTUHUMIWA HUYO ALIMPIGIA SIMU ILI WAKUTANE ENEO HILO NA KISHA
KUONDOKA KWA GARI AINA YA RAV 4 MPAKA HOTEL YA GIVALEN MOTEL ILIYOPO ENEO LA
MAKUTANO SAA MOJA NA DAKIKA 20 USIKU NA TAKUKURU WALIPOFIKA KATIKA ENEO HILO
WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA HUYO KIURAHISI.
UCHUNGUZI WA KUHUSIANA NA TUKIO HILO BADO UNAENDELEA NA
MARA UTAKAPOKAMILIKA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YA MTUHUMIWA
HUYO.
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU IMETOA
WITO KWA MABINTI WOTE WANAOKUTANA NA VISA KAMA HIVYO VYA UNYANYASAJI WA
KIJINSIA KUWA NA UTHUBUTU WA KUTOA TAARIFA ILI WANAOHUSIKA WAWEZE KUCHUKULIWA
HATUA ZA KISHERIA.
MWISHO....
0 comments:
Post a Comment