NA AHMAD
NANDONDE,
BUTIAMA.
WANANCHI
WA KATA NYEGINA KIJIJI CHA MKILILA WAMETAKIWA KUJITOLEA KATIKA UJENZI WA KITUO
CHA POLISI ILI KUKABILIANA NA VITENDO VYA UHALIFU VINAENDELEA KUJITOKEZA KATIKA
KATA HIYO.
HAYO
YAMESEMWA NA WAZIRI WA MAENDELEO JINSI NA WATOTO BI. SOPHIA SIMBA ALIPOKUWA
AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA KATA HIYO KATIKA ZIARA YAKE HIVI KARIBUNI.
AMESEMA
ILI KUKABILIANA NA TATIZO HILO NI WAZI KUWA WANANCHI WA ENEO HILO WANATAKIWA
KUJITOLEA WAO WENYEWE ILI KUHAKIKISHA WANAPATA KITUO CHA POLISI NA HIVYO
KUONDOKANA NA UHALIFU UNAOFANYIKA KIJIJINI HUMO KUTOKANA NA UMBALI ULIOPO MPAKA
KUFIKIA KITUO CHA POLISI.
KATIKA
KUSAIDIA UJENZI WA KITUO HICHO CHA POLIS AMEAHIDI KUJITOLEA MIFUKO 20 YA
SEMENTI ILI KUFANIKISHA UJENZI HUO AMBAO UTASAIDIA KUPUNGUZA UHALIFU KATIKA
KATA HIYO.
AWALI
NAIBU KAMISHNA WA JESHI LA POLISI KITENGO CHA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO BI.
ADOLFINA CHIALO AMESEMA ILI KUKABILIANA NA MAUAJI NI WAZI KUWA WANANCHI
WANATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUTOKOMEZA UKATILI UNAOENDELEA
KUJITOKEZA.
AIDHA
BI. CHIALO AMETOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA UKATILI HUKU AKIWAOMBA VIJANA
KUUNDA VIKUNDI VITAKAVYOSAIDIA KUKOMESHA UKATILI NA KUAHIDI KUPELEKA MTAALAMU
WA MAFUNZO YA POLIS JAMII ILI KUWAPATIA MAFUNZO NA MBINU ZA KUPAMBANA NA UHALIFU.
KATIKA
ZIARA HIYO WAZIRI SIMBA ALITEMBELEA KATA ZA NYEGINA NA NYAKATENDE NA KUSIKIA
KERO WANAZOKUMBANA NAZO WANANCHI WA KATA HIZO JUU YA MAUAJI YAYONAENDELEA
KUJITOKEZA.
MWISHO…..
SOPHIA AND THE PEOPLE Minister speaking SIMBA
BI. ADOLPHINA CHIALOMinister LEFT WITH LION HEAD OF REGION CCM KATBU BI. Mollel
SIMBA AND SOPHIA Minister speaking AKISALIMIANA NYAKATENDE County Residents.
0 comments:
Post a Comment