RORYA.
IMEBAINIKA
KUWA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA KWA WAATHIRIKA WA UKIMWI ARVS, ZINAUZWA KATIKA
MADUKA YA DAWA BARIDI NA MADUKA BUBU YA WATU BINAFSI KATIKA WILAYA YA RORYA
MKOANI MARA.
UCHUNGUZI
WA UMEBAINI KUWA MADUKA YANAYOUZA DAWA HIZO MENGI YANAMILIKIWA NA WATUMISHI
KATIKA VITUO VYA AFYA VYA SERIKALI, WAKATI DAWA ZINAZOUZWA NI ZILE AMBAZO
HUTOLEWA NA SERIKALI KWA AJILI YA KUPELEKWA KWENYE ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA
KWA AJILI YA WAGONJWA.
UCHUNGUZI ZAIDI UMEBAINI KUWA AFYA ZA WANUNUZI NA
WATUMIAJI WA DAWA KATIKA MADUKA HUSIKA ZIKO HATARINI KUTOKANA NA MAZINGIRA
YASIYORIDHISHA YA MADUKA HUSIKA, HUKU WAHUDUMU AU WAUZAJI KATIKA MADUKA HAYO
WAKIBAINIKA KUWA SI WATU WENYE ELIMU YA UFAMASIA.
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA
RORYA, EPHRAEM OLE NGUYAINE AMESEMA MALALAMIKO YA KUUZWA KWA DAWA HIZO NJE YA
TARATIBU YAMEFIKA OFISINI KWAKE NA KWAMBA ILIKUWA SABABU YA KUHAMISHWA KWA
WATUMISHI WA AFYA AKIWAMO ALIYEKUWA MGANGA MKUU WA WA WILAYA HIYO, DANIEL
CHACHA.
BAADHI YA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI
WAMEKIRI KUNUNUA ARV NA DAWA NYINGINE KATIKA MADUKA HAYO YA WATU BINAFSI
KUTOKANA NA KILE WALICHOKIELEZA KUWA NI UHABA WA DAWA HIZO KATIKA VITUO VYA
SERIKALI.
INAELEZWA KUWA UUZWAJI WA ARV KATIKA MADUKA YA DAWA
BARIDI, UNACHOCHEWA NA SABABU MBILI KUBWA IKIWEMO BAADHI YA WAGONJWA KUKWEPA
KWENDA VITUO VYA AFYA, AMBAKO HULAZIMIKA KUKAA KWENYE FOLENI KWA MUDA MREFU
WAKISUBIRI KUPATIWA DAWA HIZO.
SABABU NYINGINE NI UHABA WA DAWA HIZO KATIKA VITUO
VYA AFYA, HALI AMBAYO KUWALAZIMISHA WAGONJWA KWENDA KATIKA VITUO HIVYO MARA
NYINGI KUZIFUATA, HIVYO KUCHOKA KUTOKANA NA BAADHI YAO KUTOKUWA NA AFYA NZURI.
MWISHOO.....
0 comments:
Post a Comment