`

Home » » FUATILIA KISA CHA KUSISIMUA TOKA KWA FABBY KIJANA TOKA MTWARA SEHEMU YA KWANZA

FUATILIA KISA CHA KUSISIMUA TOKA KWA FABBY KIJANA TOKA MTWARA SEHEMU YA KWANZA


KUFUATILIA MKASA WA FABI KIJANA KUTOKA MTWARA AMBAYE KWA MUDA FLANI MWAKA JANA TULIWEZA KUSIKIA YANAYOMSIBU HADI TULIPOFIKIA...KWA NAFASI HIYO SASA TUNAMRUDISHA TENA ILI KUJUA MENGINE YALIYOFUATIA....KI UFUPI KUHUSU MAISHA YAKE NI KWAMBA

FABI SIKU MOJA AKIWA ANACHIMBA JALALA AKIWA NA WENZAKE WAWILI NA WAKATI HUO ILIKUWA NI ZAMU YAKE KUWA SHIMONI..WAKATI ANACHIMBA GHAFLA NDANI YA SHIMO LA JALALA ALILIGONGA JIWE GHAFLA JIWE LILE LILIANZA KUTOA DAMU NA KISHA UKATOKA MWANGA MKALI SANA…HAPO HAPO JAMAA AKAANGUKA NDANI NA KUZIMIA……WENZAKE WAKIWA NJE YA SHIMO NA STORI ZIMENOGA BAADA WANASHANGAA UKIMYA SHIMONI NDIMO KUMCHUKUA NA KUMPELEKA NDANI

 FABI AKIWA AMELALA KITANDANI GHAFLA ANASHTUSHWA NA MWANGA MKALI AMBAPO WAKATI HUU AKIWA AMEZUNGUKWA NA WATU WENGI PALE KITANDANI IKIWA NI PAMOJA NA MAMA YAKE WANAULIZANA KULIKONI…BASI KATIKA ULE MWANGA ANASEMA ALIMUONA KIUMBE AU BINTI AKIWA AMEVAA MAVAZI MITHILI YA MASISTA WA KIDINI NA YULE KIUMBE ALISOGEA MPAKA PALE KITANDANI NA AKANYOOSHA MKONO AKAMSHIKA KTK PAJI LA USO AKAWA KAMA MTU ANAYEMUOMBE 

 LAKINI FABI ANASEMA ALIONEKANA KAMA ANASALI LAKINI ILE LUGHA HAKUIFAHAMU LICHA YA KUHISI KAMA ANAOMBEWA..GHAFLA YULE KIUMBE ALITOWEKA. JAMAA ALISHTUKA KUTOKA KITANDANI NA AKAKAA NDIPO ANASHANGAA UMATI WA NDUGU WAMEMZUNGUKA LAKINI ALIPOWAULIZA KUHUSIANA NA YULE KIUMBE ALIYEKUWA MLE NDANI KILA MTU AKAWA ANAMSHANGAA YEYE BASI FABI AKAGUNDUA ALICHOKIONA ALIKUWA ANAKIONA PEKE YAKE

BASI KUANZIA HAPO YAKAWA YANATOKEA MATUKIO YA AJABU AJABU HADI ALIPOTOKA KWAO AKAWA AMEPANGA MTAA MWINGINE KAMA UNAVYOJUA KIJANA UMRI UKIWADIA..LAKINI SIKU MOJA AKIWA ANATOKA KAZINI ALIPOFIKA NA KUFUNGUA MLANGO WANGE ULIOKUWA UMEFUNGWA NA KUGULI GHAFLA NDANI ANAMKUTA BINTI MMOJA AMELALA KITANDANI KWAKE..BINTI HUYO ALIYEKUWA NA UZURI WA PEKEE NA ALIYEPELEKEA HATA HALI YA CHUMBA KUKIONA TOFAUTI, BASI JAMAA AKIWA AMESIMAMA MLANGONI BINTI HUYO AKAWA ANAAMKA PALE KITANDANI AKIWA KAMA MTU ALIYEBANWA VICHEKO..

LAKINI JAMAA KUMTAZAMA ALIGUNDUA KIUMBE HUYU NI TOFAUTI NA YULE ANAYEMTOKEA AKIWA NA MAVAZI YA MASISTA…NA KIUMBE HUYU NDO MTATA ZAIDI AMBAPO ALIANZA KUKUTANA NA MENGI

JE, NINI KINAENDELEA BASI USIKOSE KISIWA CHA SIMULIZI JUMAPILI IJAYO KUANZIA SAA NNE KAMILI USIKU KUPITIA 90.6 VICTORIA FM MUSOMA MARA.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK