BUTIAMA.
VIONGOZI WA CHAMA CHA
MAPINDUZI KWA NGAZI YA MATAWI NA KATA KATIKA KATA YA KYANYARI WAMETAKIWA
KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO IPASAVYO KWANI KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA KUKIIMARISHA
CHAMA CHA MAPINDUZI.
HAYO YAMESEMWA NA MJUMBE WA MKUTANO MKUU NA MJUMBE WA
HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI BW. MUGINGI MUHOCHI ALIPOKUWA
AKIZUNGUMZA WANANCHI WA KIJIJI CHA NYAKISWA KATA YA KYANYARI KWAAJILI YA
KUJIONEA SHUGHULI MBALI MBALI ZA MAENDELEO IKIWA KAMA SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA
ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
AMESEMA KUWA VIONGOZI WA
VIJIJI, VITONGOJI, WATENDAJI NDIYO WENYE MAMLAKA YA KUCHUKUA HATUA KWAKUWA WAO
WAMETOKANA NA CHAMA CHA MAPINDUZI HIVYO WAZI KUWA WANAUWEZO WA KUSIMAMIA
SHUGHULI MBALI KATIKA JAMII ZAO ILI KUSAIDIA MAENDELEO NDANI YA JAMII.
KATIKA ZIARA YAKE HIYO BW.
MGINGI PIA AMEWEZA KUJIONEA SEHEMU ZA SHUGHULI ZINAZOFANYA NA WANANCHI WA
KIJIJI CHA NYAKISWA IKIWA NI PAMOJA NA UJENZI WA ZAHANATI, KANISA NA OFISI YA
CHAMA NA HIVYO KUAHIDI KUSHIRIKIANA NAO BEGA KWA BEGA ILI KUKAMILISHA SHUGHULI
HIZO ZA UJENZI.
MIONGONI MWA AHADI
ALIZOZITOA NI PAMOJA NA MIFUKO MITANO YA SEMENTI KWA ZAHANATI YA KIJIJI, UJENZI
WA KANISA LA TUMAINI LILILOPO KIJIJINI NYAKISWA NA KUAHDIHI KUCHANGIA NONDO
KUMI NA MIFUKO MITANO YA SEMENTI HUKU AKIAHIDI KUTOA SHILINGI LAKI MOJA NA NUSU
KWAAJILI YA KUKAMILISJHA UJENZI WA OFISI YA TAWI LA NYAKISWA.
KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI
WA CCM TAWI LA NYAKISWA BW. THOBIAS DINDA AMEONESHA KUFURAHISHWA KWAKE NA AHADI
ILIYOTOLEWA NA BW. MUHOCHI HUKU AKIKIIITA KITENDO HICHO KUWA NI CHA KIMAENDELEO
NDANI YA KIJIJI HICHO HUKU AKIMTUPIA LAWAMA MWENYEKITI WA KIJIJI HICHO KWA
KUTOTEKELEZA AHADI ZAKE TANGU ALIPOINGIA MADARAKANI.
MWISHO.........
0 comments:
Post a Comment