`

Home » » ENDELEA KUFUATILIA STORI YA FABBY KIJANA KUTOKA MTWARA SEHEMU YA 5

ENDELEA KUFUATILIA STORI YA FABBY KIJANA KUTOKA MTWARA SEHEMU YA 5



SEHEMU YA TANO (5)

HABARI ZA JUMAPILI YA LEO WADAU WA KISIWA CHA SIMULIZI!!!! KWANZA NAOMBA LADHI KIDOGO KWA WALE WANAOFUATILIA MKASA WA FABI HUMU FB KWA KUTOPATA POST ZA STORI HIYO KWA WIKI KADHAA LAKINI HIYO NI KUTOKANA NA MSONGAMANO WA MAJUKUMU MENGINE. KWA NAFASI HIYO NIMEADHIMIA KILA NAPOPATA NAFASI HATA KAMA NI DK 15 NITAANDIKA KADRI INAVYOWEZEKANA ILIMRADI TU USIKOSE UHONDO HUO
"ANYWAY" NAOMBA NIENDELEE KATIKA SEHEMU TULIOISHIA.....

AMBAPO NI KATIKA TUKIO LILE LA KUJIKUTA ANAZUNGUKWA NA DUARA LA MWANGA (NURU) AMBAPO NI MOJA KATI YA MATUKIO YALIYOWEZA KUSHUHUDIWA NA BAADHI YA WAKAZI WA "RAILWAY" HUKO MTWARA, NA KWA WALE WALIOKUWA WANAYASIKIA TU YANAYOTOKEA KWA FABI NA KUYAONA KAMA STORI NDO WAKAANZA KUAMINI

BASI BAADA YA TUKIO HILO KUPITA NA WATU KUSAMBAA FABI AKAWA AMEINGIA NDANI NA MARA BAADA YA MUDA MFUPI ALITOKEA YULE KIUMBE WA PILI AMBAYE ANAVALIA KAMA SISTER NA KUMWAMBIA AONDOKE MLE CHUMBANI HARAKA, KISHA YULE KIUMBE AKATOWEKA. FABI HAPO HAPO PASIPO KUPOTEZA MUDA ALIAMKA KUTOKA KITANDANI NA KUTOKA NJE LAKINI KABLA YA KUUFIKIA MLANGO ULISIKIKA KAMA UPEPO UNAVUMA KWA NGUVU KISHA ULE MLANGO UKAJIFUNGA KWA KUJIBAMIZA NA HAPO HAPO ALISIKIA SAUTI YA KICHEKO NYUMA YAKE UPANDE ULE WA KITANDANI ANAKOTOKA

BAADA YA KUSIKIA SAUTI HIYO HOFU ILIMJAA GHAFLA AKATAKA KUWAHI KATIKA MLANGO LAKINI CHA AJABU ALIJIKUTA ANAIACHA ARDHI NA KUELEAELEA ANGANI (HEWANI) YAANI MIGUU IKAWA HAIGUSI CHINI YUKO HATUA CHACHE KIDOGO KWENDA JUU KATIKA TUKIO AMBALO KAMA MTU MWINGINE ANGEMUONA ANGEDHANI KAGANDISHWA HEWANI. KUFUATIA TUKIO HILI FABI ALIPIGA KELELE BILA MSAADA WOWOTE

ANASEMA LILIKUWA NI TUKIO KAMA LA SEKUNDE 45 LAKINI ALIONA KAMA NI WIKI, GHAFLA ALISIKIA MLANGO UMEFUNGULIWA KWA NGUVU KAMA UMEGONGWA NA KITU KIZITO SANA NA MUDA HUO HUO ALIHISI KAMA KUNA MTU AMBAYE HAKUWEZA KUMUONA ILA ALIHISI KAMA KUNA MIKONO IMEMSHIKA MABEGANI KISHA KAMSUKUMA KWA CHINI ILI AGUSE ARDHI.

FABI ANASEMA BAADA YA KUFIKA CHINI NA MLANGO WAKATI HUO UKIWA WAZI YAANI UMEFUNGUKA MPAKA MWISHO... ANASEMA IKAWA NI MITHILI YA MTU ALINYONGA BAISKEL HUKU AKIWA AMEIPIGA STENDI KISHA KUONDOA STENDI GHAFLA, KIUFUPI NI KWAMBA MBIO ALIZOTOKANAZO MLE NDANI ILIKUWA NI NOMA

ANASEMA NJE KULIKUWA NA MAMA FLANI MPANGAJI MWENZAKE ALIKUWA ANAOSHA VYOMBO NA MWINGINE ALIKUWA AMEKAA KWENYE NGAZI ZA MLANGONI KWAKE, ANASEMA YULE ALIYEKUWA ANAOSHA VYOMBO ALIRUSHA SAHANI KISHA AKATOKA MBIO KUELEKEA BARABARANI NA YULE ALIYEKUWA MLANGONI KWAKE BADALA YA KUINGIA NDANI NAYE ALIJIKUTA ANAKIMBIA KUELEKEA KWA FABI NA MUDA WOTE WANAKIMBIA HUKU WANAULIZA "NINI???, KUNA NINI???"

FABI ALIFIKA AKASIMAMA PEMBENI KIDOGO YA MJI WAO KISHA AKAKAA CHINI, WALE NAO KWA MUDA HUO HUKU MACHO YOYE WAKITAZAMATAZAMA NYUMA WALISOGEA MPAKA PALE ALIPOKUWA FABI WAKAMUULIZA KULIKONI....FABI AKAWA KIMYA KIDOGO KISHA AKAWAULIZA "KWANI HAMKUNISIKIA NAPIGA KELELE?".

WAKAMWAMBIA HAWAJASIKIA KELELE YOYOTE KUTOKA KWAKE. HII KIDOGO IKAMCHANGANYA MAANA ALIPIGA KELELE ZA NGUVU KWELI NA HAWA WANAWAKE AMEWAKUTA NJE IWEJE HAWAKUSIKIA!!!. BAADAE AKAWAULIZA KWANI NI NANI ALIYEMFUNGULIA MLANGO LAKINI JIBU LIKAWA WAO HAWAJAFUNGUA MLANGO WALA HAWAKUMUONA YEYOTE AKIFUNGUA MLANGO, FABI AKADUWAA

BASI BAADA YA KUTULIA KIDOGO AKAWASIMULIA TU BAADHI YA KITUKO KILICHOTOKEA LAKINI KWA KUFICHA MAMBO MENGI AMBAYO ALIHISI YANAWEZA YAKAWAOGOPESHA KWAHIYO NA WAO WAKACHUKULIA KAWAIDA WAKAANZA KUMLAUMU WAKISEMA "UTATUUA KWA PRESHA, SISI TULIDHANI NI MAMBO YAKO YAMERUDI TENA MAANA MPAKA SASA HIVI HATUNA HAMU". NA KUMBUKA ASUBUHI HIYO NDIYO WATU WALIKUWA WAMEJAA PALE NYUMBANI WAKISHANGAA LILE DUARA LA MWANGA

BAADA YA MUDA ILIBIDI AENDE KUANGALI MLANGO WAKE ALIUKUTA MZIMA KAMA KAWAIDA HAKUNA ALAMA YOYOTE LICHA YA KWAMBA MLANGO ULISIKIKA KAMA UMEGONGWA NA KITU KIZITO SANA, BASI HAKUONA SABABU YOYOTE YA KUINGIA CHUMBANI KWAKE ALIBIDI AENDE ZAKE KAZINI NA WALE WANAWAKE NAO WAKAENDELEA NA RATIBA ZAO MAANA HAWAKUJUA NINI ZAIDI KILITOKEA.

JIONI ILIPOFIKA FABI AKAWA AMETOKA KAZINI NA KAMA KAWAIDA YAKE MIDA YA USIKU KABLA YA KULALA ANAFANYA ZOEZI KWANZA. ANASEMA ILIKUWA KAMA SAA TATU (3) USIKU ALIKUWA ANAFANYA MAZOEZI HAPO NJE YA NYUMBA KARIBU NA MLANGO WAKE GHAFLA ALISIKIA KUNA SAUTI INAMUONGELESHA IKISEMA "POLE KWA MAZOEZI ILA NAOMBA LEO TUTOKE NA WEWE".

FABI ANASEMA ALIJIKUTA AMEPATA UJASIRI NA HASIRA AKAULIZA KWA HASIRA " TUTOKE TWENDE WAPI NA WEWE USIKU HUU?" SAUTI ILE IKAMJIBU " NAOMBA UJE MILENIUM BEACH MIMI NITAKUWA KARIBU NA WEWE NIKIKUWEKEA ULINZI WALA HAKUNA KIBAYA KITAKACHOKUPATA". NADHANI SEHEMU HII KWA WAKAZI NA WENYEZI WA MTWARA WATAKUWA WANAPAFAHAMU VIZURI.

FABI ANASEMA KATIKA MAONGEZI HAYO JAPO ANAYEMUONGELESHA HAMUONI ILA ALIWEZA KUITAMBUA ILE SAUTI KUWA NI YULE KIUMBE MWINGINE "YULE MTATA" AMBAPO KATIKA MAONGEZI HAYO FABI ALIKATAA HIYO STORI YA KWENDA HUKO MILENIUM KISHA AKAINGIA NDANI "FASTA". NA AKAWASIMULIA RAFIKI ZAKE KUHUSIANA NA HILO SUALA KWAMBA AENDE MILENIUM BEACH KUNA VITU MUHIMU ANATAKA KUONESHA NA WAO PIA WAKAMWAMBIA ASIKUBALI WALA ASIENDE

BASI BAADA YA MIDA KUSONGA NA KILA MTU AKIWA AMEENDA KULALA KWAKE, ILIPOFIKA KAMA SAA 8 USIKU FABI AKIWA USINGIZINI GHAFLA ALIANZA KUSIKIA SAUTI KAMA ZA MELI YAANI MITHILI YA BANDARINI NA ALIVYOSHTUKA ANASEMA ALIJIKUTA YUKO KWENYE MELI TENA MELI YENYEWE IKO BAHARINI...ANASEMA AKIWA ANASHANGAA AKIWA KATIKA UWAZI MKUBWA WA HIYO MELI AMBAYO HAINA MTU, GHAFLA MBELE YAKE ALIMUONA YULE KIUMBE MTATA AKIWA ANATAZAMA MBELE KULE MELI INAKOELEKEA LAKINI PIA ALIONEKANA KAMA MTU ANAYEBANWA SANA NA VICHEKO ILA ANAJIZUIA KUCHEKA

FABI ANASEMA ALIMUONA AKIWA KATIKA MAVAZI AMBAYO KAMA NI MA-SISTER BASI NI "SISTER DUU" YAANI MITHILI YA WASANII WAKUBWA KUTOKA NJE KAMA BEYONCE AU RIHANA WANAPOKUWA KATIKA SHOW...AMBAPO ALIKUWA AMEVALIA SULUALI NYEUSI NA KI-TOP CHAKE NA MIGUUNI ALIKUWA NA VIATU VIREFU VYA KAMBA, KICHWANI ALIKUWA NA KOFIA FLANI ZA "COW BOY" AMBAYO ILIKUWA KAMA IMEEGESHWA TU JUU YA ZILE NYWELE ZAKE ZILIZOKUWA NDEFU HADI MGONGONI NA MKONO WA KULIA ALIKUWA AMESHIKILIA FIMBO FLANI FUPI INANG'AA SANA AKIWA ANAIGONGAGONGA KATIKA KIGANJA CHAKE CHA MKONO WA KUSHOTO, NA KAMA KAWAIDA AKIWA KAMA ANAJIZUIA KUCHEKA

FABI ALIJITAMBUA KABISA NA KUJUA HAYUKO NDOTONI ILA NI LIVE BILA CHENGA, ALISUBIRI KUONA NINI KINATOKEA NA WAKATI WOTE HUO YULE KIUMBE ANATIZAMA MBELE YAANI KAMTEGEA FABI MGONGO NA AMETULIA KANA KWAMBA HAJUI YANAYOENDELEA NYUMA YAKE

JE, NINI KITAFUATA

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK