MUSOMA.
WAKALA WA
BARABARA MKOANI MARA TANROADS WAMEOMBWA KUWEKA MATUTA KATIKA BARABARA YA MUSOMA
MWANZA ILI KUONDOKANA NA AJALI ZITOKANAZO NA MWENDO KASI WA MADEREVA.
KAULI HIYO
IMETOLEWA NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU UVCCM WILAYANI BUTIAMA BW. MGINGI MHOCHI
WAKATI WA KUUAGA MWILI WA YOHANA MASHAKA MOMA ALIYEFARIKI DUNIA JANA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI WAKATI AKIVUKA BARABARA KATIKA KIJIJI CHA NYAMIKOMA KATA
KYANYARI WILAYANI BUTIAMA.
MHOCHI AMESEMA
KUWA ILI KUONDOKANA NA VIFO HIVYO WAJIBU WA TANROAD KUHAKIKISHA INATOKA
MAOFISINI NA KWENDA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI PAMOJA NA MATUTA ILI KUONDOKANA
NA AJALI HIZO ZINAZOENDELEA KUJITOKEZA MARA KWA MARA.
AIDHA BW. MHOCHI
AMEONGEZA KUWA KUTOKANA NA AJALI HIZO ZA MARA KWA MARA NI WAZI KUWA TANROAD IKAONDOKANA
NA NENO MKAKATI NA BADALA YAKE WANATAKIWA KUCHUKUA HATUA ILI KUONDOKANA NA
TATIZO HILO AMBALO LINAPELEKEA HALI YA WASI WASI KWA WAZAZI WENYE WATOTO
WANAOSOMA KATIKA SHULE HIYO.
NAYE MAKAMU MTENDAJI WA KIJIJI HICHO BW. SAIMON
MATHEO AMESEMA KUWA KUTOKANA NA ENEO HILO KUWA NDIYO MAKAO MAKUU YA KIJIJI
HICHO WANAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA KUWEKA KITUO CHA MABASI ILI KUPUNGUZA MWENDO
KASI WA MADEREVA PINDI WATAKAPO KUWA KATIKA SAFARI ZAO.
HATA HIVYO MAKAMU MWENYEKITI HUYO AMEOWAOMBA
WANANCHI WA KIJIJI HICHO KUJIEPUSHA NA TABIA ZA KUKAA KANDO KANDO YA BARABARA ILI
KUJIEPUSHA NA HATARI INAYOWEZA KUJITOKEZA PINDI AJALI PANAPOTOKEA AJALI.
AJALI HIYO ILIYOSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI HUYO
PIA IMESABABISHA MAJERUHI KWA WANAKIJIJI WAWILI WALIOKUWA KARIBU NA AJALI HIYO PAMOJA
NA WATU WATATU WALIOKUWAMO NDANI YA GARI AINA YA LAND CRUISER PRADO LILILOKUWA
LIKITOKEA JIJINI MWANZA KUELEKEA MJINI MUSOMA.
0 comments:
Post a Comment