NA AHMAD NANDONDE,
SEHEMU YA NNE (4)
BAADA YA FABI
KUWASHA TAA KWELI ALIMUONA YULE BINTI AKIWA AMECHUCHUMAA NA BAADA YA MUDA
AKASIMAMA HUKU AKIWA KAMA KABANWA VICHEKO..NA MUDA WOTE HUU BABA YAKE JAMAA
KAJIBANANISHA KWA KIJANA YAANI YALE MAMBO ALIYOKUWA ANAYASIKIA KWA KIJANA WAKE
AKAWA KAMA HAAMINI SASA SIKU HIYO NDO IKAWA LIVE
YULE BINTI
ALIYEKUWA KAMA AMEBANWA SANA VICHEKO GHAFLA AKABADIRIKA NA KUONEKANA KAKASIRIKA
SANA, KISHA AKAMWANGALIA AKAMKAZIA MACHO BABA'KE FABI AKAONEKANA ANAKUJA KWA
KASI UPENDE ULE WA KITANDA KAMA KAWAIDA YAKE ANATEMBEA KWA HATUA TATU NA HII
NDO ISHARA YAKE YA KUTOWEKA. KWAHIYO ALIONEKANA HAPA KULE AKIWA AMEKARIBIA
KARIBU NA KITANDA..FABI ANASEMA HATA HAKUONA TENA KILICHOENDELEA MAANA ALIFICHA
SURA NA KUPIGA KELELE HUKU KICHWA KINATAKA KUPOTELEA KWENYE MAGOTI.
ANASEMA ALIKAA
KIMYA HUKU CHUMBA CHOTE KILISIKIKA KIMYA SANA HAKUNA MOVEMENT YA KITU CHOCHOTE,
WAKATI HUO HUO BILA KUFUNUA KICHWA ALINYOOSHA MKONO KUPAPASA SEHEMU ALIYOKUWA
AMELALA BABA'KE AKAMGUSA. LAKINI AKASHTUKU MZEE YUKO KIMYA, FABI AKAITA "
BABA"..... MZEE KWA MBALI AKAITIKA "MMMMMM". FABI ANASEMA SAUTI
HII ILIMFARIJI KIDOGO MAANA ALIPATA WASI WASI KWAMBA LABDA BABA YAKE KASEPA.
BAADA YA MUDA
FABI ALIFUNGUA MACHO NA KUANZA KUANGAZA ANGAZA CHUMBANI LAKINI HAKUONA KITU
NDIPO ALIGUNDUA YULE KIUMBE KATOKA. ALIMUAMSHA BABA YAKE NA KUMWAMBIA HAKUNA
KITU..NA WAKATI WOTE HUO MZEE ANATETEMEKA YAANI IKAWA KAMA FABI NDO MZAZI NA
BABA NDIYO MTOTO..MAANA MZEE ALIKUWA MPOLE MPAKA BASI. ALIKAA KIMYA KWA MUDA NA
WAKATI HUO HAKUNA ALIYELALA TENA WALA ANAYEHISI USINGIZI YAANI WOTE WAMEKAA TU
KITANDANI.
BAADAYE KIDOGO
FABI ALIMUONA MZEE ANAAMKA KITANDANI AKAENDA AKACHUKUA SHATI LAKE AKAVAA,
BAADAE AKACHUKUA VIATU AKAVAA KISHA AKAMWAMBIA FABI "MIMI NAENDA LAKINI
ASUBUHI KUKICHA NAOMBA UJE NYUMBANI"..AKAAGA KISHA AKAFUNGUA MLANGO
AKATOKA NJE, FABI ANACHOSEMA ALISIKIA KISHINDO TU CHA MZEE ANAVYOTOKA MBIO HUKO
NJE.
FABI ALIAMKA
AKAFUNGA MLANGO KISHA AKAWA AMEJIEGESHA TU PALE KITANDANI MAANA HATA USINGIZI
HAKUNA TENA NA WAKATI HUO AKIWA ANAHISI MUDA WOWOTE YULE KIUMBE ATARUDI LAKINI
HAIKUTOKEA NA ILIPOFIKA ASUBUHI ALIENDE KWAO KAMA BABA'KE ALIVYOAGIZA.
ALIFIKA
AKAWAKUTA WAZAZI WANAONGEA NA WALIKUWA WANAONGELEA MAMBO HAYO HAYO YANAYOMHUSU
JAMAA, ALIFIKA AKAJUMUIKA NAO KATIKA MAZUNGUMZO NA WAKATI HUU SASA BABA NDO
ALIONEKANA KUZINGATIA SANA MAANA AMESHUHUDIA KWA MACHO YAKE MAANA MUDA MWINGI
ALIPOKUWA ANAPATA HABARI ZA FABI NI VITU AMBAVYO HAKUVIAMINI KATIKA MAISHA YAKE
ALICHUKULIA KAMA STORY TU AKAHISI LABDA JAMAA PENGINE AMEANZA KUVUTA BANGI SASA
LABDA HIZO NI GIA TU ZA KUTOKEA.FABI ANASEMA NI KWA MARA YA KWANZA ALIMUONA
BABA'KE ANAONGEA HUKU ANAMWANGALIA FABI KWA HURUMA HADI MACHOZI YANAMLENGA
LENGA.
KWELI WALIONGEA
MENGI SANA NA KUTAFUTA UFUMBUZI NA MIONGONI MWA MANENO YAO JAMAA APELEKWE KWA
WAGANGA WA KIENYEJI MARA MATAMBIKO YA UKOO WAO, YAANI MANENO MENGI TU YASIYO NA
JIBU LA MOJA KWA MOJA. BAADA YA MJADALA WA MUDA MREFU BAADAE WALIFIKIA
HITIMISHO LA MJADALA WAO WAKAENDELEA NA MAJUKUMU MENGINE AMBAPO SIKU HIYO FABI
ALILALA PALE NYUMBANI KWAO NA KESHO YAKE NA SIKU ILIYOFUATA ALIRUDI GETO KWAKE.
ALIPOINGIA ROOM
ALIKUTA CHUMBA KINANG'AA YAANI KIMEPAMBWA MPAKA BASI, JAMAA ALIKITAZAMA BAADAYE
AKATOKA NJE AKAWAAMBIA WENZAKE ANAOISHI NAO HAPO. ANASEMA KWANZIA TUKIO HILO
WALE WAPANGAJI WAKAANZA KUMUITA " BABA AGNES MAUA". KWAHIYO LIKIFANYIKA
JAMBO LOLOTE LISILO LA KAWAIDA KATIKA ULE MJI UTASIKIA " HAYO NI MAMBO YA
BABA AGNES MAUA" HIVYO HIVYO MAISHA YANAENDA
FABI ANASEMA
ALIKUWA ANAMAZOEA YA KUFANYA MAZOEZI KILA ALFAJILI NA MIDA YA JIONI ANAPOTOKA
KAZINI. SIKU MOJA ALIAMKA ALFAJILI SANA KWA AJILI YA MAZOEZI IKIWA KAMA SAA
KUMI NA MOJA KASORO, AKIWA NJE AMECHUCHUMAA GHAFLA ALISIKIA KUNA KITU KAMA
DUARA LIMEMZUNGUKA LIKIWA LINANG'AA SANA YAANI LINATOA MWANGA MKALI SANA.FABI
ALISIMAMA KWA HOFU LAKINI KUMBUKA LILE DUARA LIMEMUWEKA KATIKATI AMBAPO ANASEMA
KATIKA DUARA LILE KULIJIGAWA MARA MBILI, LILIANZA DUARA DOGO LIKIWA NI JEUSI
SANA LIKIFUATIWA NA HILO DUARA LINALONG'AA.
FABI ALIOGOPA
LAKINI HAKUWEZA KUTOKA KATIKATI MAANA JINSI LILE DUARA LILIVYO HATA ALISHINDWA
KUJUA PENGINE LINAWEZA KUMFANYA NINI KAMA AKILIKARIBIA...ANASEMA ALISIMAMA
TAKRIBANI DK 10 BILA KUFANYA CHOCHOTE LAKINI KADRI MUDA ULIVYOKUWA UNAENDA
ILIONEKANA KAMA MNG'AO WAKE UNAPUNGUA....AKIWA AMESIMAMA HIVYO HIVYO ALISIKIA
KUNA WATU WANAKUJA KUTOKA UPANDE MWINGINE WA NYUMBA YAO MAANA KULIKUWA NA NJIA
INAYOPITA HAPO KARIBU NA NYUMBA YAO.
KWA HIYO ALIANZA
KUSIKIA KWA MBALI WATU WANAKUJA HUKU WANAONGEA NA KWA JINSI ALIVYOSIKIA
ZILIKUWA NI SAUTI ZA WATOTO WA KIKE NA BAADHI YAO AKAWATAMBUA AMBAPO KWA HARAKA
ALIJUA WANATOKA DISCO. BAADA YA HAWA BINTI KUCHOMOZA KWENYE USAWA WA NYUMBA
PALE UWANJANI WALIPIGA YOWE WAKAKIMBIA KURUDI WALIKUTOKA HUKU WANAPIGA KELELE.
HAPO NDIPO FABI AKAJUA ANACHOKIONA SI YEYE PEKEE HATA WENGINE WANAWEZA KUKIONA.
SASA KUTOKANA NA
ZILE KELELE WATU WENGINE WAKAAMKA NA KWA MUDA HUO FABI SASA ILIBIDI ACHUNGUZE
HICHO KINACHOTOA MWANGA NAMNA HIYO NI NINI, SO ALIBIDI ACHUCHUMAE CHINI ILI
ACHUNGUZE VIZURI. ALIPELEKE MKONO KATIKA LILE DUARA LINALING'AA KUONA NI NINI,
WAKATI HUO ANAFANYA KWA UWOGA MKUBWA YAANI ANAPOPELEKA MKONO KISHA ANASITA
MWISHO AKAJIKAKAMUA AKASEMA KAMA KUFA BASI ACHA AFE..AKANYOOSHA MKONO AKAGUSA
PALE KATIKA DUARA LAKINI CHA AJABU ALIONA ANAGUSA MCHANGA WA KAWAIDA TU
AKAJARIBU KUUNUSA AKASIKIA HARUFU KAMA MCHANGA WA BAHARI
LAKINI KINGINE
NI KWAMBA HATA VILE VIDOLE VIKAWA KAMA VINANG'AA ALIJIFUTIA KWENYE BUKTA YAKE
NAYO AKIWA KAMA AMEIPAKA VITU VYA KUMETAMETA. KUMBE KIPINDI WALE MABINTI
WANAKIMBIA HUKU WANAPIGA YOWE KUFIKA BARABARANI WALIKUTANA WA VIJANA WENGINE
KUULIZWA KUNA NINI WAKAELEZA SASA IKABIDI WALE VIJANA NA WALINZI KATIBA MADUKA
YA HAPO JIRANI WAONGOZANE KUJA KUONA NINI KIMETOKEA
WALIKUJA MPAKA
PALE NAO KUFIKA TU KIDOGO WATOKE MBIO ILA KWA SABABU WALIKUWA WENGI
WAKAJIKAKAMUA. FABI AKAWAMBIA "MSIOGOPE NJOO TU". KUMBUKA KULIKUWA NA
MWANGA MKALI KWAHIYO ILIKUWA NI RAHISI KUMUONA NA KUMTAMBUA FABI. YAANI KILA
MTU AKAWA NA LAKE HAKUNA ALIYETAKA HATA KUSOGEA TOFAUTI NA KUHAMAKI TU NA JINSI
WANAVYOSHANGAA NDIVYO WATU WENGINE WALIVYOKUWA WANAZIDI KUAMKA NA KUONGEZEKA.
KWAHIYO WATU WALIJAA SANA KATIKA ULE MJI
LAKINI CHA AJABU
NI KWAMBA KILA PALIVYOKUWA PANAENDELEA KUPAMBAZUKA NDIPO MWANGA UNAFIFIA
KWAHIYO ILIFIKIA HATUA MWANGA UKAWA WA KAWAIDA NA ULE MCHANGA NDO UKAANZA
KUONEKANA VIZURI.
KILA MTU
ALIZUNGUMZA YAKE KATIKA TUKIO HILI NA MWISHO YA SIKU LIKATOKA WAZO LA KUWAITA
USTADHI TOKA MSIKITI ULIOKUWA JIRANI NA BAADA YA KUJA NAYE ALIFIKA AKAELEZA
MAMBO MENGI HUKU KUBWA AKISEMA HAKUNA JAMBO BAYA NA HIYO INAWEZA KUWA NI SEHEMU
YA BARAKA. BAADA YA HAPO ALICHOTA ULE MCHANGA KIDOGO NA KUWAAMBIA KAMA KUNA MTU
ANAAMINI BASI ANAWEZA KUCHUKUA TU. BAADHI YA WATU WAKAONA KUMBE NI DILI BASI
WAKAUZOA WAKAENDA KUMWANGA KATIKA VIWANJI MWAO YAANI KILA MTU KWA JINSI
ALIVYOAMINI.
MIONGONI MWA
WALIOUCHUKUA MCHANGA HUO NI PAMOJA NA MPANGAJI MMOJA WA PALE NYUMBANI AMBAYE
ALICHUKUA MCHANGA NA AKAENDA KUUWEKA KATIKA CHUMBA FLANI CHA STOO KILICHOKIWA
KINATUMIKA KWA KUWEKA MKAA. LAKINI BAADA YA KUUWEKA KILE CHUMBA KILING'AA
UTADHANI UMEWEKA BALBU 50, YAANI ULE MCHANGA ULIKUWA UNAWAKA AJABU..HADI
WAPANGAJI WENGINE WAKAPATA HOFU WAKAMWAMBIA AUTOE NJE. BASI ALIENDA AKAUCHUKUA
BAADAE AKAENDA AKAUWEKA NJE
BASI BAADA YA
MUDA WATU WAKAANZA KUSAMBAA MAJUMBANI MWAO, AMBAPO FABI NAYE AKAINGIA CHUMBANI
MWAKE ALKINI ALIPOKAA TU KITANDANI KWAKE GHAFLA UKATOKEA MWANGA MKALI MLANGO
KISHA AKAMUONA YULE KIUMBE MWINGINE ANAYEVAA KAMA SISTER KAMA ANAHARAKA FLANI
HIVI " AKAMWAMBIA TOKA NJE HARAKA" KISHA YEYE AKATOWEKA.
FABI ANASEMA
HATA BILA KUKAWIA ALIAMKA KWA HARAKA KUTOKA NJE LAKINI KABLA YA KUUFIKIA MLANGO
ALISHTUKIA MLANGO UNAJIFUNGA KWA NGUVU SANA "BAAAAAAA" KISHA AKASIKIA
KICHEKO CHA MTOTO WA KIKE KIKITOKEA UPANDE WA KITANDANI ALIKUKUWA AMEKAA.......
NINI KINAENDELEA BASI USIKOSE MWENDELEZO WA STORI HII SEHEMU YA TANO.
NDANI YA JICHO LA MDADISI BLOG PEKEE
0 comments:
Post a Comment