`

Home » » FUATILIA MKASA WA FABBY KIJANA TOKA MTWARA KUANZIA SEHEMU YA KWANZA HADI YA TATU HAPA.

FUATILIA MKASA WA FABBY KIJANA TOKA MTWARA KUANZIA SEHEMU YA KWANZA HADI YA TATU HAPA.

KWA WALE WALIOKUWAWAKIKIFUATILIA KISA HIKI MWANZONI KABLA SIJAKIKATISHA NAWAOMBENI RADHI KWANI NILIKUWA KATIKA MAUJUKUMU YA KIFAMILIA NILIKUWA NAINGIA KWENYE NDOA KWAHIYO MAJUKUMU YAKAWA MENGI MNO KWAAHIYO SASA NIMEYAKAMILISHA NA NDOA YANGU SASA INA MIEZI MINNE.

SASA BASI NIMEONA SI VIBAYA NIKAENDELEA NA KUAWAPATIA MAMBO MATAMU KUTOKA KWENYE BLOG HII YA JICHO LA MDADISI ISIYOISHA HAMU NA KWA KUANZA TU NIMEAMUA KUANZA MWANZO KABISAAAA AMBAPO NTAENDA HADI SEHEMU YA TATU KABLA YA JUMATATU KUENDELA TENA.

NA KILA JUMATATU NA ALHAMIS NTAKUWA NIKIWALETEA KISA HIKI CHA KUSISIMUA KWA HIYO NAWAOMBA MUJIWEKE SAWA NA KWA WALE AMBAO HAWAKUWAHI KUSIKIA WALA KUSOMA KISA HIKI BASI NI WAKATI WENU NA KWA WALIOKUWA NA MIMI TANGU AWALI BASI ENDELEENI KUWAJUZA NA WENGINE KWANI MAMBO MAZURI YANAKUJA ZAIDI NA ZAIDI.
NIMIMI MSMULIZI WAKO,,.....

NA AHMAD JAY NANDONDE,

SEHEMU YA KWANZA

FABIANI AU MAARUFU KAMA FABI NI MKAZI NA MZALIWA WA MTWARA. KATIKA MAISHA YOTE TANGIA ANAZALIWA HADI MAISHA YAKE YA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI HAKUWAHI KUKUTANA NA JAMBO LOLOTE AMBALO LINGETATANISHA MAISHA YAKE.

LAKINI BAADA YA KUHITIMU KIDATO CHA NNE AKIWA NYUMBANI KWAO TAKRIBANI MIAKA 13 ILIYOPITA BASI MAISHA YAKE YALIANZA KUWA YA WASI WASI SINTOFAHAMU NA HOFU TELE, HII NI MARA BAADA YA KUWA ANATOKEWA NA VIUMBE WAWILI AMBAO NI WA AJABU LICHA YA UZURI WALIONAO AMBAPO KWA NAMNA NYINGINE MMOJA KATI YAO HAZOELEKI NA ANATISHA SANA TU

MAMBO YALIANZA HIVI,FABI SIKU MOJA AKIWA ANACHIMBA JALALA AKIWA NA WENZAKE WAWILI NA WAKATI HUO ILIKUWA NI ZAMU YAKE KUWA SHIMONI..

WAKATI ANACHIMBA GHAFLA NDANI YA SHIMO LA JALALA ALILIGONGA JIWE GHAFLA JIWE LILE LILIANZA KUTOA DAMU NA KISHA UKATOKA MWANGA MKALI SANA…HAPO HAPO JAMAA AKAANGUKA NDANI NA KUZIMIA……

WENZAKE WAKIWA NJE YA SHIMO NA STORI ZIMENOGA BAADAYE WANASHANGAA UKIMYA SHIMONI NDIMO KUMCHUKUA NA KUMPELEKA NDANI

FABI AKIWA AMELALA KITANDANI GHAFLA ANASHTUSHWA NA MWANGA MKALI AMBAPO WAKATI HUU AKIWA AMEZUNGUKWA NA WATU WENGI PALE KITANDANI IKIWA NI PAMOJA NA MAMA YAKE WANAULIZANA KULIKONI…

BASI KATIKA ULE MWANGA ANASEMA ALIMUONA KIUMBE AU BINTI AKIWA AMEVAA MAVAZI MITHILI YA MASISTA WA KIDINI NA MKONONI AKIWA AMEBEBA KITU KAMA KITABU KIKIWA NA MAAANDISHI AMBAYO HAKUWEZA KUTAMBUA NI LUGHA GANI.

YULE KIUMBE ALISOGEA MPAKA PALE KITANDANI NA AKANYOOSHA MKONO AKAMSHIKA KATIKA PAJI LA USO NA AKAWA KAMA ANAMUOMBEA LAKINI CHA AJABU LUGHA ALIYOKUWA ANAITUMIA YULE KIUMBE YEYE HAKUIELEWA LICHA YA KUMUONA NA KUMSIKIA JINSI ALIVYOKUWA BUSY KATIKA MAOMBI.

ANASEMA ALIOMBA KWA MUDA MFUPI SANA NA MWISHO AKAMUITA KWA JINA " FABI AMKA".

NA KISHA YULE KIUMBE AKATOWEKA VILE VILE YAANI UKATOKA MWANGA MKALI UPANDE WA MLANGONI KISHA AKATOWEKA YAANI HAPO HAPO FABI ALIJIKUTA ANAINUKA KWA MSHTUKO AKAJIKUTA AMEROPOKA TU "WAAAAAAAAAAAAAA" BAADAE ALISHTUKA KUONA WATU WAMEMZUNGUKA TENA WANAMSHANGAA, KUMBUKA KUANZIA WAMTOE JALALANI JAMAA ALIKUWA HAJAPATA FAHAMU KIASI KWAMBA BAADHI WALIHISI WENDA KAFA..KWAHIYO TUKIO LA KUMUONA ANAAMKA GHAFLA NA YOWE NAO LILIWASTUA.

LAKINI JAMAA ALIVYOAMKA TU AKAWAULIZA WATU WALIOKUWA MLE NDANI "JAMANI HUYO DADA ANATOKA WAPI". CHA AJABU ANAONA WATU WANAZIDI KUMSHANGAA.

AKAENDELEA KUWASISITIZA MMEMUONA HUYO DADA?. WALA HAKUPATA JIBU TOFAUTI NA KUONA WATU NDO WANAZIDI KUMSHANGAA NA BAADA YA MASWALI HAYO MAMA YAKE ALIANZA KULIA AKAJUA MTOTO WAKE KACHANGANYIKIWA..

MAANA KWANZA AMEDONDOKA AKAPOTEZA FAHAMU KWA MUDA MREFU NA BAADAE ANAAMKA NA KUROPOKA MAMBO AMBAYO HAWAYAELEWI.

KWA JINSI FABI ALIVYOENDELEA KUWAULIZA NAYE ALIGUNDUA KUWA WENZAKE HAWAKUMUONA YULE MTU NA HIVYO NI JAMBO AMBALO NI YEYE PEKE YAKE NDO ALILISHUHUDIA. BASI BAADA YA KUPUMZIKA ALIWASIMULIA ALICHOKIONA KULE JALALANI NA KUHUSU TUKIO LA YULE KIUMBE MLE NDANI.

BAADA YA KUSIKIA HIVYO WALIBIDI WAENDE KUANGALIA MLE JALALANI LAKINI HAWAKUONA CHOCHOTE.

BASI TUKIO HILI LIKAWA LIMEPITA LAKINI MAMA MZAZI AKAWA AMEPATA WASI WASI JUU YA JAMAA. NA KUANZIA HAPO HAKUMRUHUSU JAMAA KUTOKA PALE NYUMBANI ILI YASIJE YAKATOKEA MAMBO KAMA HAYO AKIWA MBALI NA "HOME"

ZILIPITA SIKU KAMA MBILI JAMAAA AKIWA ANASHINDIA PALE NYUMBANI..BASI SIKU MOJA AKIWA PALE NYUMBANI PAMOJA NA WALE RAFIKI ZAKE WALIOKUWA WANACHIMBA NAYE JALALA SIKU ILE YA KWANZA, GHAFLA ALIONA NDEGE FLANI AITWAYE "TUMBUSI" SINA HAKIKA KAMA JINA HILI NIMEPATIA ILA NDEGE HUYU NI JAMII YA MWEWE.

YULE NDEGE ALIWAPITA PALE WALIPOKUWA WAMEKAA NA ALIPITA KATIKA MAZINGIRA AMBAYO SI YA KAWAIDA KIASI KWAMBA LAZIMA UTAPATA WASI WASI TU KWA NAMNA ALIVYOPITA LAKINI PIA NDEGE HUYU NI MUOGA SANA ILA CHA AJABU ALIPITA KARIBU NAO KISHA AKAWA AMEZUNGUKA NYUMA YA NYUMBA.

FABI ALIWAULIZA RAFIKI ZAKE " VIPI MMEMUONA HUYO NDEGE?" LAKINI CHA AJABU RAFIKI ZAKE WAKASHANGAA HILO SWALI WAKAMWAMBIA HAKUNA NDEGE ALIYEPITA, FABI ANASEMA JINSI ALIVYOKUWA ANAONGEA NAO NAO KUKATAA ILIMBIDI AZUNGUKE NYUMA YA NYUMBA KULE NDEGE ALIKOELEKEA ILI AHAKIKISHE LAKINI ALIPOZUNGUKA HAKUMUONA YULE NDEGE.

ALITIZAMA HUKU NA KULE LAKINI HAKUMUONA KISHA AKARUDI KUKAA PALE ALIPOKUWA NA RAFIKI ZAKE LAKINI ILE KUKAA TU GHAFLA AKAMUONA YULE NDEGE AMBAPO ALIKUJA NA KUTUA KATIKA MTI ULIOKUWA KARIBU NAO.

BASI FABI AKAWAAMBIA WENZAKE "YULE NDEGE NINAYEWAAMBIA SI HUYU HAPO" HUKU AKIWAONESHA KWA KIDOLE LAKINI KILA ANAVYOWAONESHA JAMAA WANASEMA HAWAONI CHOCHOTE NA BAADAYE WAKAMBEZA KABISA WAKAENDELEA NA STORI ZINGINE WAKAMUACHA JAMAA KAKODOA JUU YA MTI.

FABI ANASEMA ALIJIKUTA YULE NDEGE ANAMUANGALIA SANA NA FABI KWA UPANDE WAKE MACHO YOTE KAMKODOLEA YULE NDEGE..YAANI IKAWA NDEGE HATA HATIKISI KICHWA JICHO KWA FABI NA UPANDE MWINGINE FABI MACHO YOTE MTINI AKIMWANGALIA YULE NDEGE AMBAPO WALITAZAMANA KAMA DK 5 LAKINI GHAFLA UPANDE WA YULE NDEGE KIKATOKEA KITABU KIKUBWA SANA NA KIKAWA KAMA KUNA MTU KAKIRUSHA KUELEKEA UPANDE WA FABI..

LAKINI CHA AJABU BADALA YA FABI KUSHTUKA NDO AKAJIKUTA KAZUBAA ZAIDI ANASEMA KILE KITABU KILIONEKANA KIKUWA NA KWA JINSI KINAVYOSOGEA NDO KINAZIDI KUWA KIKUWA ZAIDI.

KITABU KILE KILIENDELEA KUSOGEA KIKIWA KINAFUNUKA FUNUKA KARATASI KAMA UNAVYOJUA KITABU KITAKAPORUSHWA ANGANI. LAKINI CHA AJABU KILA KINAVYOFUNUKA KIKAWA KINAONESHA PICHA MBALIMBALI KAMA SINEMA NA KIKAFIKIA WAKATI KIKAONEKANA KURASA ZOTE MBILI YAANI KATIKATI.

NA KATIKA KURASA HIZO KUKAWA KUNAONEKANA KAMA SINEMA MABAPO UKURASA WA KUSHOTO WALIONEKANA WATU WENGI SANA WAKO MSIBANI WANALIA KATIKA MJI ALIOUFAHAMU NA BAADHI YA WATU WALIOONEKANA WANALIA ANAWAFAHAMU NA UPANDE WA PILI ALIMUONA MWANAMKE MMOJA AMEJITANDA KHANGA AKIWA ANATEMBEA HUKU ANALIA SANA NA ALIPOMTAZAMA VIZURI ALIMGUNDUA KUWA NI MKE WA MJOMBA WAKE.

FABBY ANASEMA AKIWA BADO KAZUBAA NA WENZAKE SASA WANAMSHANGAA MAANA WALIMUONA KAMA SANAMU YAANI HATIKISIKI WALA KOPE HAZICHEZI GHAFLA KILE KITABU KIKAJIFUNGA NA KIKATOWEKA.

JAMAA ALIKURUPUKA MBIO HADI JIKONI KWA MAMA YAKE AMBAYE ALIKUWA ANAPIKA, NA ALIPOFIKA TU AKAMWAMBIA MAMA YAKE " MAMA MJOMBA AMEKUFA". MAMA YAKE ALISHTUKA KWA MSHANGAO BAADAE AKAONA KWELI MWANANGU KACHEZEWA AKILI, AKAMWAMBIA, "HIVI WEWE MUDA WOTE ULIKUWA HAPO UMEJUAJE MJOMBA WAKO AMEFARIKI?" FABI AKAMWAMBIA SHANGAZI YUKO NJIANI ANAKUJA HUKU LAKINI KABLA HAJAMALIZA TU KUMUELEZEA AKASIKIKA SAUTI YA MTU ANAKUJA HUKU AKILIA AMBAPO MAMA YAKE ALIITAMBUA KUWA NI SAUTI YA WIFI YAKE, YAANI HAPO HAPO MAMA YAKE AKAANGUA KILIO "JAMANI KAKA YANGUUU...."

BASI BAADA YA TAARIFA ZOTE ZA MSIBA NA WIFI YAKE KUFIKA WAKAANZA KUJADILI NAMNA YA KWENDA KULE MSIBANI AMBAPO SUALA KUBWA LILIKUWA NI NAULI. FABI ANASEMA KWA MUDA HUO WOTE YEYE ALIKUWA ANAJIHUSISHA NA UUZAJI WA MITUMBA KATIKA DUKA FLANI LAKINI KWA WAKATI HUO HAKUWA NA HELA YOYOTE BASI ILIMBIDI AFANYE MPANGO WA KUWATAFUTIA WAZAZI NAULI AMBAPO KWANZA ALIHISI KWENDA KUOGA NA MCHAKATO UANZE

ALICHOTA MAJI KWENYE NDOO NA KISHA ALIYABEBA KUELEKEA BAFUNI LAKINI KABLA HAJAINGIA BAFUNI ALISIKIA KUNA MTU ANAMGUSA BEGA LA KUSHOTO ALIPOGEUKA HAKUMUONA, ALIPOKUWA ANASHANGAA KISHA AKAHISI KAGUSWA BEGA LA KULIA KUGEUKA ALISHTUKANA SANA KWA ALICHOKIONA...JE, UNATAKA KUJUA NINI KILITOKEA? BASI USIKOSE STORI HII KATIKA BLOG YA JICHO LA MDADISI

SEHEMU YA PILI (2)

FABI ALIPOTAKA KUINGIA BAFUNI GHAFLA ALISIKIA KAMA KUNA MTU ANAMGUSA BEGANI LAKINI ALIPOGEUKA NYUMA HAKUONA MTU KISHA AKASIKIA TENA KAGUSWA BEGA JINGINE ALIPOGEUKA ALIMUONA YULE KIUMBE ANAYEVAA KAMA MASISTA...ANASEMA ALIOGOPA SANA HADI MAJI ALIYOKUWA ANAENDA KUOGA YAKAMWAGIKA. LAKINI KWA JINSI ALIVYOKUWA ANAMTAZAMA YULE DADA ALIMUONA KAMA KIUMBE ASIYE NA JAMBO BAYA YAANI KAMA ANAMHURUMIA FLANI HIVI JAMBO AMBALO LILIPELEKEA FABI KUZUBAA

LAKINI FABI AKIWA ANATIZAMANA NA YULE KIUMBE GHAFLA YULE DADA ALITOA NA KUMUONESHA NOTI TATU ZIKIWA NA RANGI TATU TOFAUTI. KATIKA KUZITIZAMA FABI HAKUZITAMBUA NI NOTI (HELA) ZA NCHI GANI MAANA HATA SI ZA TANZANIA JAPO KWA KUZITAZAMA ALIZIONA KUWA NA HELA. YULE KIUMBE ALIMUONESHA TU ZILE NOTE PASIPO HATA KUMUONGELESHA JAMBO LOLOTE KISHA AKATOWEKA KAMA KAWAIDA YAKE, YAANI KWA MWANGA MKALI

FABI ALISIMAMA PALE KATIKA MLANGO WA BAFU KWA MUDA HUKU AKIJIULIZA NI MAMBO GANI HAYO YANAYOMTOKEA HATA ASIELEWE, LAKINI PIA AKIFIKIRIA HICHO KIUMBE KINATAKA NINI HATA HANA MAJIBU..AMBAPO KATIKA MAMBO HAYO YALIMFANYA HATA MACHOZI KUANZA KUMTOKA. ALIINAMA AKACHUKUA NDOO YAKE (KUMBUKA MAJI YALIMWAGIKA) KISHA AKAWA ANARUDI NDANI LAKINI AKIWA ANASHUKA NGAZI KUTOKA BAFUNI ALISIKIA MTU ANAMUITA, KUTIZAMA ALIMKUTA BINTI FLANI JIRANI YAKE

BINTI YULE ALIKUJA AKAMPATIA SHILINGI ELFU THELATHINI (ZILIKUWA NOTI TATU ZA ELFU KUMI) AKAMWAMBIA MAMA YAKE AMEMTUMA ALETE. BASI FABI ALIIPOKEA ILE PESA BILA SWALI LOLOTE MAANA ILIKUWA NI YA DENI LAKE LA NGUO KISHA YULE BINTI AKAONDOKA. FABI ALITEMBEA LAKINI KABLA HAJAINGIA NDANI AKAKAA KWENYE NGAZI ZA KUINGIA NDANI, ALIANZA KUFIKIRIA JUU YA HAYA MATUKIO, ALIZITAZAMA SANA ZILE HELA NA KISHA AKAJIULIZA IWEJE YULE KIUMBE ALIMUONESHA NOTI TATU NA BAADAYE AMELETEWA NOTI TATU NA MDENI WAKE....HII KITU ILIMPA KUWAZA SANA

LAKINI AKIWA MLANGONI MAMA YAKE ALITOKA NJE NA KUMKUTA PALE MLANGONI AKAMUULIZA KULIKONI MBONA HATA HAJAOGA, FABI ALIMJIBU STORI ZINGINE TU KWA KUZUGA WALA HAKUMWAMBIA KUHUSU HILO TUKIO AKAHISI NI JAMBO AMBALO LINAWEZA KUMSITUA SANA MAMA YAKE. ALITOA ZILE HELA AKAMPATIA MAMA YAKE KAMA NAULI ILI WATANGULIE MSIBANI

BASI MAMA YAKE ALIFANYA MAANDALIZI YOTE KISHA AKAONDOKA KWENDA MSIBANI, FABI NAYE KESHO YAKE AKAWA AMEPATA PESA NYINGINE KUTOKA KWA RAFIKI YAKE NAYE AKAENDA KULE MSIBANI, NA BAADA YA SHUGHULI ZOTE ZA MSIBA AMBAPO MAJIRANI, MARAFIKI NA WAGENI WENGINE KUWA WAMETAWANYIKA MAMA YAKE MZAZI ALIWAITA BAADHI YA NDUGU WALIOKUWA PALE MSIBANI AKAANZA KUWASIMULIA YANAYOMTOKEA KIJANA WAKE (YAANI FABI) NA HATA TUKIO LA HUO MSIBA. BAADHI YA NDUGU WALISHANGAA SANA NA KILA MTU AKAWA NA LAKE KUHUSIANA NA MAMBO YANAYOMTOKEA FABI
.
WAPO WALIOSHAURI APELEKWE KWA WAGANGA WA KIENYEJI, WENGINE WALISHAURI APELEKWE KANISANI NA KWINGINEKO KWA AJILI YA MAOMBEZI. YAANI KILA MTU AKAWA NA LAKE HATA KUFIKIA KUHUSANISHA HATA BAADHI YA MILA ZA UKOO WAO NA MATUKIO FLANI FLANI YALIYOKWISHA KUTOKEA KWENYE HUO UKOO LAKINI MWISHO WA YOTE HAPAKUWA NA JIBU LA MOJA KWA MOJA

BASI BAADA YA MSIBA FABI AKAWA AMERUDI NYUMBANI. SIKU MOJA MIDA YA MCHANA ALICHUKUA KITI CHA MALIMBA AKATOKA NACHO NJE AKAENDA KUKAA KWENYE KIVULI CHA MTI MMOJA WA MWEMBE PALE NYUMBANI KWAO.

FABBY ALIKAA KWA MUDA KISHA KA-USINGIZI KAKAANZA KUMPITIA PITIA, MUDA FLANI KAUSINGIZI KAKIWA KAMEMPITIA GHAFLA ALISIKIA KICHEKO NYUMA YAKE YAANI KAMA KUNA MTU AMESIMAMA NYUMA YAKE AKIWA ANACHEKA, ALISHTUKA NA ALIPOGEUKA NYUMA ALIMUONA KICHAA FLANI MCHAFU SANA AKIWA ANACHEKA OVYO HUKU ANAMTAZAMA FABI YAANI KANA KWAMBA YULE KICHAA ALIKUWA ANAMCHEKA FABI...

FABI NAYE ALIANZA KUMTIZAMA YULE KICHAA LAKINI AKAJIULIZA HUYU KICHAA ANATOKA WAPI MAANA ALIKUWA MGENI SANA MACHONI PAKE YAANI HAJAWAHI KUMUONA HATA MARA MOJA (NA KAMA UNAVYOJUA VICHAA MARA NYINGI WANAFAHAMIKA MFANO HAPA MUSOMA KUNA BAADHI YA VICHAA UKIWAONA HAUSHTUKI SANA MAANA WANAFAHAMIKA) SASA KWA FABI ANASEMA PAMOJA NA UENYEJI WAKE PALE MTWARA HAJAWAHI KUMUONA YULE KICHAA JAPO KWA MUONEKANO HUWEZI KUSITA KUMTAMBUA KUWA NI KICHAA.

LAKINI KUMTAZAMA VIZURI CHA AJABU YULE KICHAA ALIKUWA AMEBEBA MFUKO FLANI WA NAILONI AKIWA AMEUHIFADHI KWA USAFI SANA

NA BAADA YA MUDA YULE KICHAA AKIWA KAMA ANAONDOKA ANARUDIRUDI NYUMBA ALITOA KITABU FLANI KWENYE ULE MFUKO, KITABU AMBACHO KILIKUWA KIMETUNZWA VIZURI YAANI MPAKA BASI. FABI AKAMUOMBA KILE KITABU NAYE YULE KICHAA KWA CHEKO ZAKE HIZO HIZO ALISOGEA AKAMPA FABI KILE KITABU, FABI ALIKITIZAMA KILE KITABU LAKINI HAKUKIELEWA YAANI KIMEANDIKWA MAANDISHI NA LUGHA KAMA KILATINI, KWAHIYO ALIISHIA KUKIFUNUAFUNUA TU. BAADAE AKAMUOMBA TENA KINGINE.

YULE KICHAA NAYE ALITOA KITABU KINGINE NA KUMPATIA FABI AMBAPO KITABU HIKI KILITOFAUTIANA RANGI NA KILE KITABU ALICHOMPA MWANZONI, FABI ALIPOKITAZAMA NACHO PIA HAKUKIELEWA JAPO KINAONEKANA NI KITABU SAFI KINA MAANDISHI NA PICHA PICHA ILA LUGHA ILIYOTUMIKA NDO NGENI SANA KWAKE.

BAADA YA HAPO FABI ALIMTAKA YULE KICHAA AMUONESHE KITABU KINGINE KILICHOSALIA YAANI AKAWA KAMA ANAMUOMBA. LAKINI KWA AWAMU HII YULE KICHAA HAKUONESHA KUJALI AKAWA ANACHEKACHEKA TU NA BAADAYE ALIONESHA KUKATAA KABISA KUMUONESHA KILE KITABU.

YULE KICHAA ALIANZA KUONDOKA POLE POLE HUKU ANACHEKA NA BAADA YA KUFIKA HATUA FLANI NYUMA ALIKITOA KILE KITABU NA AKAMUONESHA FABI YAANI KAMA ANAMRINGISHIA. FABI ANASEMA KITABU HICHO KILIKUWA NA RANGI NYEKUNDU TOFAUTI NA VITABU VINGINE LAKINI NACHO KAMA KAWAIDA JINSI ALIVYOKUWA ANAKICHEKI MAANDISHI KATIKA LILE JARADA LUGHA YAKE HAKUIELEWA

YULE KICHAA ALIONDOKA VILE VILE HUKU AKICHEKA MPAKA AKAFIKA MBALI BASI FABI NAYE IKABIDI AANZE KUVIANGALIA VILE VITABU ALIVYOKUWA AMEBAKI NAVYO LAKINI JINSI ANAVYOVITAZAMA NDO HAELEWI KABISA SO AKAONA KAMA HAINA MAANA AKAEGEMEA KWENYE KILE KITI CHA MALIMBA.

LAKINI GHAFLA ALISIKIA KAMA HALI YA HEWA IMEBADILIKA GHAFLA YAANI KUKAWA NA HARUFU NZURI NA UPEPO UKAVUMA TOFAUTI NA AWALI NA MWANGA UKAONGEZEKA, ALIACHA KUEGEMEA AKAKAA VIZURI LAKINI MBELE YAKE ALIMUONA YULE KIUMBE TENA (YULE SISTA) NA AKAMWAMBIA JAMBO FUPI TU KISHA AKATOWEKA, AKAMWAMBIA "FABI KILA KINACHOTOKEA KWAKO KINA MAANA KWAHIYO ZINGATIA"

FABI ANASEMA JAMBO HILI LILIANZA KUMSHANGAZA LINA MAANA GANI KATIKA MAISHA YAKE, ALIVITIZAMA VILE VITABU KISHA AKAJIULIZA NI KWANINI YULE KICHAA HAKUMPA KITABU CHA TATU. LAKINI BAADA YA MUDA ALITAFAKARI JAMBO FLANI LAKINI HAKUPATA JIBU YAANI KUHUSU NA HIZI TATU TATU, MAANA MWANZONI ALIONESHWA NOTI TATU, LAKINI BAADA YA MUDA ALILETEWA DENI LAKE LA HELA IKIWA NI NOTI "TATU" LAKINI PIA HUYU KICHAA KAJA NA VITABU VITATU NA KUMPA VIWILI JAPO CHA TATU ALIKATALIA.

BASI SIKU ZIKAWA ZINAENDA NA BAADHI YA VITENDO KUTOKA KWA HUYO SISTA AMBAVYO ALIANZA KUVIZOEA KWA KIASI FLANI. NA KWA MUDA WOTE HUU FABI ALIKUWA ANAISHI KWAO LICHA YA KUWA ANAFANYA BIASHARA ZAKE, LAKINI ILIFIKIA WAKATI AKAONA AMEKUA KIJANA MKUBWA NA AKAONA NI BORA SASA AJITEGEMEE. KWELI ALIONDOKA PALE KWAO AKAENDA KUPANGA MTAA MWINGINE HUKO HUKO MTWARA.

MAISHA YALIENDELEA KAMA KAWAIDA BAADA YA "JOB" ANARUDI KWAKE. KILA ANAPOPATA PESA ANAFIKIRIA NINI AFANYE KWA MAENDELEO YA "GETHO " LAKE NAMISHE ZINGINE.....LAKINI KATIKA MUDA WOTE HUU FABI ANASEMA HAKUWEZA KUWA ANATAMBUA BAADHI YA MABADIRIKO YALIYOKUWA YANATOKEA PALE KWAKE HADI WATU WENGINE HASA MARAFIKI WAKAWA WANAMSIFIA KUHUSIANA NA MAENDELEO NA MABADIRIKO MENGINE.

SIKU MOJA FABI AKIWA KAZINI KICHWA KILIANZA KUUMA ALIVUMILIA BAADAYE YAKAMSHINDA IKABIDI "AFUNGE GOLI LAKE LA MITUMBA" AONDOKE KWENDA "HOME" ILIKUWA KAMA SAA 11 JIONI. ALITEMBEA KUELEKEA NYUMBANI LAKINI BAADA YA MWENDO KIDOGO ALIPOFIKA NJIANI ALISIKIA MUUNGURUMO KAMA RADI KUTOKA JUU ANGANI ALISIMAMA NA KUANGALIA JUU.

ALIPOKUWA ANAANGALIA JUU ANASEMA ALIONA WINGU FLANI JEUSI SANA NA KATIKATI YAKE KAMA KUNA KITU FLANI KINAWAKA ILA SI JUA.

LAKINI ALIPOKUWA ANASHANGAA HILO GHAFLA HUKO HUKO KUPITIA LILE WINGU ALIONA SURA KAMA YA YULE KIUMBE AKIWA ANANG'ANG'ANA KWENDA KWENYE ULE MWANGA NA UPANDE MWINGINE LILE WINGU JEUSI NALO KAMA LINAZUIA ASIENDE KWENYE ULE MWANGA.

FABI ANASEMA ALIJIKUTA AMEZUBAA KUANGALIA LILE TUKIO. KUMBE KATIKA ILE HALI YA KUSIMAMA KAANGALIA JUU MTU MWINGINE NAYE KUONA FABI KAANGALIA JUU NAYE AKALIUNGA KUANGALIA KUNA NINI JAMAA
ANACHOSHANGAA...

FABI ANASEMA MWANZONI ALISIKIA JAMAA ANAMUULIZA "KUNA NINI" LAKINI BAADAYE HAKUWA ANASIKIA TENA CHOCHOTE IKAWA KAMA KAHAMISHWA KIFIKRA.

FABI ANASEMA AKIWA ANATAZAMA KINACHOENDELEA ANGANI, WAKATI YULE SISTA ANANG'ANG'ANA KUPITA KATIKA LILE DUARA LINALOONEKANA KAMA WINGU ILA NI JEUSI SANA KULIKO KAWAIDA GHAFLA KATIKA LILE WINGU KUNA VITU VILIFYATUKA VIKAMGONGA YULE SISTA AKAONEKANA KUTUPWA MBALI, YULE SISTA ALILIA SAUTI AMBAYO FABI ANASEMA ILISIKIKA KAMA ANALILIA KWENYE UBONGO WAKE HAPO HAPO AKASIKIA MAUMIVU MAKALI KISHA AKADONDOKA CHINI.

ALIANGUKA CHALI HUKU MACHO YAKIWA BADO YANATIZAMA YANAYOENDELEA KULE JUU (UKWELI NI KWAMBA KATIKA TUKIO LA MPAKA YEYE ANAANGUKA CHINI HAKUJITAMBUA ILA ALIAMBIWA BAADAYE)

BASI KATIKA TUKIO HILI ALIMUONA YULE SISTA AKIWA AMEKASIRIKA SANA NA ANALITAZAMA LILE DUARA, GHAFLA KUTOKA ULE UPANDE WA SISTA ALITOKEZA YULE NDEGE TUMBUSI ALIYEMUONA PALE KWAO SIKU ILE YA KWANZA (NI NDEGE JAMII YA MWEWE), YULE NDEGE ALIONEKANA KWENDA KWA KASI KAMA MSHALE KUELEKEA KATIKA LILE DUARA NA SISTA ALIKUWA ANAFUATA NYUMA YAKE.

YULE NDEGE MITHILI YA RISASI ALILICHANA LILE DUARA LIKATAWANYIKA KATIKATI NA SISTA ALISOGEA KWENYE ULE MWANGA ULIOKUWA UMEKINGWA NA HILO DUARA AKANYOOSHA MKONO KISHA ULE MWANGA ULING'AA ZAIDI KISHA SISTA NA YULE NDEGE WAKATOWEKA

BAADA YA KUTOWEKA TU HAPO HAPO FABI ANASHTUKA KAMA ANATOKA USINGIZINI, ANASHANGAA KUKUTA WATU WAMEMZINGIRA KILA MTU ANAONGEA LAKE. WENGINE WALISEMA WALIMUONA AMESIMAMA AKIANGALIA JUU KAMA DAKIKA 15 KILA MTU AKAANZA KUJIULIZA HUYU KIJANA VIPI NA KILA WALIPOKUWA WANAMUONGELESHA ALIKUWA AMEGANDA KAMA SANAMU, SO ALIPODONDOKA WENGINE WAKAHISI WENDA ANAKIFAFA LAKINI KILA WALIPOKUWA WANAMTAZAMA WALA HAENDANI NA UGONJWA HUO

FABI ALIAMKA KUTOKA PALE CHINI LAKINI CHA AJABU ZAIDI KICHWA KILIKUWA KIMEPONA YAANI HATA DALILI ZA KUHISI MAUMIVU KWA MBALI HAKUNA. ALIJIKUTA ANAHISI HATA KURUDI KAZINI LAKINI AKAONA BASI TU AENDE HOME KUPUMZIKA. NJIANI ALIJIULIZA SANA KUHUSU HILO TUKIO LAKINI PIA KUHUSU HATIMA YAKE.

ALIENDA AKAFIKA NYUMBANI KWAKE, AKAFUNGUA MLANGO LAKINI KABLA HATA HAJAINGIA NDANI ALISIKIA HARUFU NZURI SANA, KUINGIA NDANI GHAFLA KWENYE KITANDA CHAKE ANAMKUTA BINTI AMELALA, HEEE!!! FABI ALISHTUKA NA AKAJIKUTA TU ANAMUULIZA " WEWE NANI NA UMEFIKAJE HUMU" ?

BINTI HUYO ALIKUWA AMELALA KIFUDIFUDI KICHWA KIMETIZAMA CHINI ALIONEKANA AKIWA ANAAMKA KWENYE KITANDA HUKU AKIWA KAMA AMEBANWA SANA NA KICHEKO...FABI ANASEMA HUYU BINTI ALIKUWA MZURI KULIKO KAWAIDA. HUYU BINTI ALIINUKA AKASIMAMA KARIBU NA KITANDA KISHA AKAMTAZAMA FABI AKATABASAM KISHA AKAMWAMBIA "WALA USIWE NA HARAKA YA KUNIJUA UTANIFAHAMU TU MUDA UKIFIKA NA UKIKAMILISHA MASHARTI MATATU

FABI ANASEMA ALIVYOSIMAMA KWA JINSI ALIVYOKUWA ANAONEKANA AKAHISI SIYO BINTI WA KAWAIDA HADI NYWELE KICHWANI ZIKASISIMKA...GHAFLA YULE BINTI ALITEMBEA HATUA TATU ZA MBALIMBALI YAANI AKAONEKANA HAPA PALE KULE AKAPOTEA. FABI ANASEMA ALISHTUKA AKAOGOPA NA KURUDI NJE FASTA AKAUBAMIZA ULE MLANGO. ALITOKA AKAKAA NJE YA MLANGO AKAJIKUTA JASHO LINATIRIRIKA NA ASIJUE HUYU KIUMBE NAYE ANATOKEA WAPI MAANA MUONEKANO NA MATENDO YAKE NI TOFAUTI SANA NA YULE KIUMBE MWINGINE ANAYEVAA MAVAZI KAMA YA SISTAM

KIUFUPI HUYU KIUMBE NDIYE ANAKUJA NA MAMBO YA AJABU AMBAYO BADO HAYANA MAJIBU

SEHEMU YA TATU (3)


BAADA YA JAMAA KUMUONA HUYU BINTI WA PILI ANASEMA KWA HARAKA ALISHTUKA NA AKAJIKUTA TU AMEPATA UJASIRI WA KUMUULIZA "WE NANI"....WAKATI HUO HUYO KIUMBE AKIWA ANAAMKA KATIKA KITANDA AKIWA KAMA KABANWA SANA NA KICHEKO.


ALISIMAMA AKAMWAMBIA "HAINA HARAKA YA KUNIJUA ILA UKIFIKA WAKATI UTANIJUA TU" NA BAADAYE ALITEMBEA HATUA TATU ZA MBALIMBALI SANA KISHA AKATOWEKA

JAMAA ANASEMA ALISHTUKA AKAFUNGA MLANGO KWA HARAKA NA KUTOKA NJE, NA BAADAE ALIKAA KATIKA MSINGI WA NYUMBA HIYO AKITAFAKARI NDIPO ALIGUNDUA KUNA UTOFAUTI MKUBWA KATI YA KIUMBE HUYU WA PILI NA YULE WA KWANZA ALIYEMTOKEA SIKU YA KWANZA...

MOJA YA TOFAUTI ZAO NI KWAMBA HUYU MUONEKANO WAKE KAMA NI MABINTI BASI HUYU NI WALE MASISTA DUU LAKINI PIA UPOTEAJI WAKE NA KWA YULE WA KWANZA YEYE ANAANZA KAMA MWANGA MKALI NA UPOTEAJI WAKE NI HIVYO HIVYO..

JAMAA ANASEMA ALIFIKIRI SANA KUHUSU TUKIO HILI JAPO KWA WAKATI MWINGINE KUTOKANA NA KUKUTANA MARA KWA MARA NA YULE MWINGINE KIDOGO ILIANZA KUMFANYA KUZOEA KIDOGO LAKINI HUYU ALIANZA KUMUONGEZEA UWOGA TENA...ANASEMA SIKU HIYO ALIENDA KULALA KWAO AMBAPO ALIMWAMBIA MAMA YAKE SUALA HILI

BASI BAADA YA SIKU KAMA MBILI ILIBIDI ARUDI KWAKE..LAKINI ANASEMA KILA SIKU ALIKUWA ANALALA ILA HAONI KAMA KUNA MABADILIKO YOYOTE. LAKINI KUNA MUDA FLANI DEMU WAKE ALIKUWA ANAFIKA PALE MARA KWA MARA NA WAKATI MWINGINE JAMAA ALIKUWA ANAMUACHA HUYU MPENZI WAKE PALE HOME

LAKINI SIKU MOJA GHAFLA HUYO MPENZI WAKE AKAMWAMBIA JAMAA "SASA HIVI UKIWA UNATOKA TU NA MIMI NATOKA MAANA HAPA KWAKO HATA SIPAELEWI YAANI UKIWA HAOPO KUNA MAZINGIRA AMBAYO MIMI SIYAELEWI"

AKAMWAMBIA SIKU MOJA ALIKUWA HAPO HOME KAMA UNAVYOJUA WANAWAKE KAZI NYINGI KWA WAKATI MMOJA..ANASEMA JIKONI ALIKUWA AMEACHA MBOGA YUKO NJE ANAFUA LAKINI KURUDI NDANI ALIKUTA MBOGA IMEEPULIWA..ANASEMA ALISHANGAA KIDOGO BAADAE AKAJIFARIJI KUWA LABDA ALIEPUA ILA KASAHAU, HIYO SIKU IKAPITA.

SIKU NYINGINE ALIKUWA NJE LAKINI KURUDI NDANI ALIKUTA KITANDA KIMETANDIKWA VIZURI SANA...........NDIPO ALIPOGUNDUA KUNA UTOFAUTI MAANA MARA NYINGI ALIPOFIKA PALE HOME ALIKUWA ANAKUTA KITANDA KIMETANDIKWA VIZURI KAMA HIVYO NAYE KWA MARA YA KWANZA ALIANZA KUMSIFIA MPENZI WAKE LAKINI CHA AJABU JAMAA ANAPOKUWEPO WALA HANA MUDA WA KUTANDIKA KITANDA NA AKITANDIKA BASI NI KAWAIDA SANA..SO SIKU HII NDO AKAJUA TOFAUTI

LAKINI MBALI NA YOTE FABI HAKUWAHI KUMWAMBIA YANAYOMSIBU KWAHIYO SIKU HIYO ALIBIDI AMWAMBIE KILA KITU...

ANASEMA BINTI HUYU ALISHANGAA SANA NA KISHA AKAANZA KULIA KWA KUMHURUMIA. KWELI KITU CHA AJABU KUTOKA KWA YULE DADA ALIMWAMBIA ITABIDI SOMETIMES AWE ALALA HAPO

BASI SIKU MOJA USIKU KAMA SAA SABA JAMAA KABLA HATA USINGIZI HAUJAMPITIA WAKATI HUO MPENZI WAKE ALIKUWA AMELALA GHAFLA ALISIKIA KITU KINAKIMBIA KIMBIA NJE YA NYUMBA KIKIZUNGUKAZUNGUKA..LAKINI KILA ANAPOSIKIA KISHINDO HICHO NI MITHILI YA KITU CHENYE KWAKO AMBAPO UNGEWEZA KUSEMA NI KWATO ZA NG'OMBE AU FARASI

BAADA YA MUDA MFUPI ALISIKIA SAUTI INAMUONGELESHA DIRISHANI..SAUTI HIYO HAITAJI MANENO YAANI INAZUNGUMZA KAMA BUBU MMMMM MMMM MMMMM, KUMBE MUDA HUO HUYO MPENZI WAKE ALIKUWA HAJALALA AKASIKIA MPENZI WAKE ANAMKUMBATIA KWA UWOGA HUKU ANATETEMEKA

CHA AJABU NI KWAMBA MBALI NA ILE SAUTI KUMUONGELESHA KAMA BUBU YEYE KWA UPANDE WAKE ALIKUWA ANASIKIA..NA ALICHOSIKIA NI KWAMBE ILE SAUTI ILIKUWA INAOMBA CHAKULA...KUMBUKA MUDA WOTE YULE MPENZI WAKE KAMNG'ANG'ANIA YAANI HATAKI KUBANDUKA.....................

JAMAA ANASEMA SIKU HIYO WALIKUWA WAMEPIKA WALI MAHARAGE NA BAHATI NZURI NI KWAMBA CHAKULA KILIKUWA KIMEBAKI..BASI JAMAA ALIAMKA KITANDANI NA KWENDA MOJA KWA MOJA HADI KILIPOKUWA CHAKULA AKAPAKUA WALI KWENYE SAHANI AKATIA NA MAHARAGE KISHA AKASOGEA MLANGONI HUKU ANATETEMEKA MAANA NI KIUMBE CHA NAMNA GANI HAJUI ILA ILICHOSIKIA KISHINDO CHAKE AMBACHO KILISIKIKA KAMA MNYAMA MWENYE KWATO NA JINSI KILIVYOKUWA KINAKIMBIA KIMBIA HUKO NJE

ANASEMA ALIFUNGUA MLANGO SEHEMU NDOGO SANA INAYOTOSHA KUPITISHA ILE SAHANI TU NA AKACHUCHUMAA AKAIWEKA ILE SAHANI KWA NJE KISHA AKAFUNGA MLANGO BAADAE AKARUDI KITANDANI NA PUNDE SI PUNDE ALISIKIA KAMA KUNA KITU KINAKULA KILE CHAKULA..

LAKINI MUDA MFUPI TU ALISIKIA SAHANI INATOA MLIO KUASHIRIA CHAKULA KIMEISHA..ALIANZA KUFIKIRIA NI KIUMBE GANI HUYO ANAYEKULA MSOSI CHAPU CHAPU NAMNA HIYO LAKINI HAKUPATA JIBU

PUNDE SI PUNDE ALISIKIA TENA HIYO SAUTI INAMUONGELESHA HAPO DIRISHANI..KIUKWELI YULE MPENZI WAKE JINSI ALIVYOJIBANA KWA FABI HUKU ANATETEMEKA HADI HURUMA LAKINI KWA UPANDE WAKE YEYE HAKUWEZA KUELEWA KILE KIUMBE KINAONGEA NINI TOFAUTI NA HUO MGUNO NA SWAGA ZA KIBUBU LAKINI CHA AJABU FABI ALIELEWA KILIKUWA KINASEMA NINI...FABBY

ANASEMA ALISIKIA KINAMUAGA NAYE AKAJIKUTA AMEPATA UJASIRI NA KUITIKIA "SAWA ASANTE KARIBU TENA" NA BAADAYE ALISIKIA KAMA KINAONDOKA LAKINI SI KWA KISHINDO KILE KAMA CHA MWANZO

TUKIO HILI LILISABABISHA USIKU HUO HAWAKULALA NA KWA MUDA WOTE YULE DADA ALIKUWA KIMYA.........YAANI PALIPOANZA KUPAMBAZUKA TU YULE DADA AKAOMBA KUSINDIKIZWA KWAO..KWELI FABBY  ALIFANYA HIVYO KISHA NAYE AKAONA KAMA PALE HAPALIPI TENA SIKU HIYO ALIONDOKA KWENDA KULALA KWAKO...

KAMA KAWAIDA AKAWASIMULIA WAZAZI WAKE LAKINI KWA MUDA WOTE MATUKIO MENGI YANATOKEA BABA YAKE ALIKUWA HAYUPO KWAHIYO ALIKUWA ANASIKIA TU STORI KUTOKA KWA MKEWE NA NI MAMBO AMBAYO ALIKUWA HAAMINI...NA SIKU HIYO AKAMWAMBIA ITABIDI KESHO YAKE WAENDE KULALA HUKO KWA JAMAA

JAMAA ALIKUBALI NA SIKU ILIYOFUATIA BAADA YA CHAKULA WALIENDA KULALA KWA JAMAA..

BASI ILIPOFIKA USIKU KAMA SAA SABA JAMAA AKIWA AMEPITIWA USINGIZI GHAFLA ALISIKIA BABA YAKE ANAMVUTA KWA NGUVU TENA KWA UWOGA HUKU AKIMHISI ANATETEMEKA SANA..

JAMAA ALIPOSHTUKA ALISIKIA KUNA SAUTI KAMA YA KITU KINAUNGURUMA NDANI YA CHUMBA CHAO KWENYE KONA UPANDE ALIOKUWA BABA YAKE..

SAUTI ILISIKIKA KAMA YA MNYAMA ILA ILIKUWA NI NGENI SANA KAMA NI MNYAMA BASI NI ASIYEMFAHAMU..LAKINI KWENYE KONA HIYO KULIONEKANA KUNA KITU KINANG'AA MACHO

ALISOGEZA MKONO AKAWASHA TAA NA BAADA YA MWANGA BASI ALIMUONA YULE DADA AKIWA AMECHUCHUMAA PALE NA MUDA HUO AKAONEKANA MZURI SANA KULIKO ALIVYOMUONA MARA YA KWANZA.

FABBY ANASEMA TOFAUTI NA YULE ANAYETOKEA NA MAVAZI KAMA MASISTA, HUYU ANAONEKANA NI MTATA SANA NA JINSI ANAVYOKUJA MARA NYINGI INAMTISHA...

KIUMBE HUYU AKIWA AMECHUCHUMAA BAADA YA TAA KUWASHWA AKASIMAMA NA KAMA KAWAIDA ANAONEKANA KAMA KABANWA SANA KICHEKO, ALIWATAZAMA PALE KITANDANI WOTE WAWILI AKIWA ANATABASAMU NA MUDA WOTE HUU BABA YAKE AKIWA KAMSHIKA FABI KWA NGUVU.

AADAYE AKABADILIKA GHAFLA YAANI AKAONEKANA KUKASIRIKA NA AKAMTIMA BABA YAKE FABI KWA HASIRA...........JE NINI ATAFANYA BASI USIKOSE MWENDELEZO WA MKASA HUU.

JE, UNATAKA KUJUA MWENDELEZO WA MKASA HUU? BASI ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YA "JICHO LA MDADISI"......KILA JUMATATU NA ALHAMISI..


0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK