MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA BI. ANGELINA MABULA AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YALIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA.

KUSHOTO NI KAIMU MKURUGENZI HALMASHAURI YA BUTIAMAANAYEFUATA NI MENEJA WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC BW. FRANK MAMBO ANAEFUATA MWENYE VAZI LA KITENGE NI MKUU WA WILAYA BUTIAMA BI ANGELINA MABULA.
Na Ahmad Nandonde,
BUTIAMA.
VIONGOZI WA
HALMASAHAURI YA BUTIAMA MKOANI MARA WAMESHAURIWA KUWATUMIA VIJANA WALIOHITIMU
MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA UFYATUAJI WA MATOFALI YA MFUNGAMANO KWAAJILI YA UJENZI
WA MAABARA, MADARASA NA ZAHANATI ILI KUONDOKANA NA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA.
HAYO
YAMESEMWA JANA NA MGENI RASMI AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA BI.
ANGELINA MABULA ALIPOKUWA AKIFUNGA MAFUNZO YA SIKU 13 KWA VIJANA 40 YALIYOTOLEWA
NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KWAAJILI YA KUTOA FURSA KWA VIJANA NA UBORESHAJI
WA MAKAZI YALIYOFANYIKIA ENEO LA KIABAKARI.
BI.
MABULA AMESEMA KUFUATIA MAFUZO YALIYOTOLEWA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA BASI
IPO HAJA KWA HALMASHAURI KUWATUMIA VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO HAYO KATIKA
UJENZI WA MIRADI MBALIMBALI YA SERIKALI NA HII NI KUTOKANA NA UJENZI HUO KUWA
NI GHARAMA NAFUU.
AMESEMA
KUTOKANA NA KUENDELEA KUKUA KWA WILAYA HIYO HUSUSANI KATIKA UJENZI WA CHUO
KIKUU CHA KILIMO PIA HIYO INAKUWA NI FURSA KWAO KUPATA TENDA ZA KUJENGA MAKAZI
YA WATUMISHI WA CHUO HICHO ILI KUJIKWAMUA KIMAISHA.
NAYE
MENEJA WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA BW. FRANK MAMBO AMEWATAKA VIJANA KUITUMIA
VYEMA FURSA HIYO YA MAFUNZO WALIYOIPATA NA KUISAMBAZA TEKNOLOJIA HIYO MPYA YA
MATOFALI YA KUFUNGAMANA
KWA
VIJANA WENZAO ILI KUINUFAISHA JAMII NZIMA KWANI ENDAPO WATAWEZA KUIFANYA KWA
UMAKINI NI WAZI KUWA ITASIADIA KATIKA KUJIKWAMUA KIMAISHA.
HATA
HIVYO BW. MAMBO AMESEMA KUWA MAFUNZO HAYO NI MOJA WAPO YA SERA INAYOTOLEWA NA
SHIRIKA HILO NA HII NI KUTOKANA NA KUPUNGUZA GHARAMA ZA KIFEDHA TOFAUTI NA
MATOFALI YA KUCVHOMA AMBAYO HUTUMIA MUDA MWINGI MPAKA KUKAMILIKA HALI
INAYOPELEKEA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.
MWISHO..............................
0 comments:
Post a Comment