MUSOMA.
WAUGUZI WA
HOSPITALI KUU YA MKOA ILIYOPO MANISPAA YA MUSOMA WAMEFANYA KIKAO MAALUMU
KWAAJILI YA KUUMBA UONGOZI WA HOSPITALI HIYO KUWAPA UFAFANUZI SAHIHI JUU YA
KISI CHA MALIPO WANACHITAKIWA KULIPWA KWA MUDA WAO WA ZIADA KATIKA KIPINDI CHA
MIEZI MITANO TOFAUTI NA HAPO AWALI.
HAYO YAMESEMWA
NA BI. JESCA AJENGO AMBAYE NI MUUGUZI NGAZI YA UUGUZI MSAIDIZI WA HOSPITALI
HIYO MARA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WAUGUZI WA HOSPITALI HIYO BAADA YA
KIKAO CHAO KILIKUWA NA LENGO LA KUPATA KUJADILI MALIPO YAO KIKAO CHAO CHA
KUJADILI NI NAMNA GANI WATALIPWA MALIPO YAO HAYO.
BI. JESCA
AMESEMA KUWA MALIPO HAYO AMBAYO MUHUDUMU WA KAWAAIDA HULIPWA KIASI CHA SHILINGI
15,000 NA WAUGUZI 20,000 HADI 30,000 LAKINI CHA KUSHANGAZA WAMEKUWA WAKILIPWA
KWA KIWANGO CHA CHINI NA HATA WAKATI MWINGINE WANALIMBIKIZIWA MADENI YAO HAYO
YA MUDA WA ZIADA TOFAUTI NA MADAKTARI AMBAO WAO HUPATIWA FEDHA ZAO KWA WAKATI.
AMESEMA KUWA
KUTOKANA NA NA HALI HIYO ILIYOPO HIVI SASA WAMEUOMBA UONGOZI WA HOSPITALI HIYO
KUWAPATIA MAJIBU SAHIHI ILI WAWEZE KUFANYA KAZI ZAO KAMA KAWAIDA KWANI
INASHANGAZA KUONA KUWA DAKTARI AKILIPWA KWA WAKATI TOFAUTI NA WAO AMBAO NDIYO
WANAOTOA MSAADA WA KUKAA NA MGONJWA KWA KIPINDI KIREFU.
NAYE MGANGA
MFAWIDHI WA HOSPITALI HIYO BW. ILAGI NGEREGEZA AMESEMA WAO KAMA UONGOZI WA
HOSPITALI HIYO TAYARI WAMESHAFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI
WA HOSPITALI (TUGHE) NA KUGUNDUA KUWA KULIKUWA NA TATIZO KWA WAUGUZI NA
WAHUDUMU KUTOELEWA VYEMA JUU YA MFUMO ULIOTUMIKA KATIKA KUHESABU MASAA YA KAZI
YA ZIADA.
HATA HIVYO
AMESEMA KUWA KWA HIVI SASA HAKUNA TENA TATIZO LOLOTE KATI YA UONGOZI WA
HOSPITALI NA WAFANYAKAZI HAO KWANI KILA KITU KIMESHAMALIZKA NA KAZI ZA
KUHUDUMIA WAGONJWA ZIANAENDELEA KAMA KAWAIDA.
MWISHOO.....................
0 comments:
Post a Comment