MUSOMA.
ZAIDI YA WATOTO 255
KUTOKA MADHEHEBU MBALI MBALI WAMEPATIWA CHUJIO LA KISASA ILI KWAAJILI YA KUTIBU
MAJI ILI KUKABILIANA NA MARADHI YATOKANAYO NA MATUMIZI YA MAJI YASIYO SALAMA.
AKIZUNGUMZA
WAKATI WA KUKABIDHI CHUJIO HIZO MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTECOST ASEMBLESS OF
GOD PAG KAMNYONGE BW. DEUS KIJETH AMESEMA UONGOZI WA KANISA HILO UMEAMUA KUTOA
MSAADA HUO ILI KUONDOKANA NA HOMA ZA MATUMBO AMBAZO WAHANGA WAKE WAKUBWA NI
WATOTO.
AIDHA MCHUNGAJI
KIJETH AMESEMA MBALI NA MSAADA HUO KUONDOPKANA NA MARADHI YA TUMBO KWA MATUMIZI
YA MAJI YASIYO SAFI NA SALAMA LAKINI PIA MSAADA HUO UTASAIDIA WAZAZI KUPUNGUZA GHARAMA
ZA MAFUTA YA TAA, GESI NA KUNI NA HIVYO KUPUNGUZA KIASI CHA SHILINGI MIL. 90
KWA MWAKA ENDAPO KAYA ZOTE HIZO ZITATUMIA MAFUTA YA SHILINGI 500 KWA SIKU.
MCHUNGAJI KIJETH
AMETOA WITO KWA WAZAZI WA WATOTO WALIONUFAIKA NA MSAADA HUO KUHAKIKISHA
WANAZITUNZA CHUJIO HIZO ILI WAWEZE KUNUFAIKA KWA KIPINDI KIREFU KWANI CHUJIO
HILO HUWEZA KUDUMU KWA KIPINDI CHA MIAKA MIA MOJA.
NAYE MAKAMU
KATIBU MKUU WA KANISA HILO NCHINI BW. CHARLES KANYIKA AMEWAOMBA WAZAZI WALIOPATA CHUJIO HIZO KUWASAIDIA WENZAZO KUCHUJA
MAJI ILI ILI KUONDOKANA NA MARADHI HAYO HUSUSAN KIPINDU PINDU KWANI WASIPOFANYA
HIVYO NI WAZI KUWA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA YATAWEZA KUMPATA HATA MWENYE CHUJIO.
KWA UPANDE WAO
WAZAZI WA WATOTO WALIOPATIWA CHUJIO HIZO WAMEUSHUKURU UONGOZI WA KANISA HILO
KWA KITENDO CHAO CHA KIUNGWANA KWANI KWASASA NI WAZI KUWA MAGONJWA YALIYOKUWA
YAKIWAKABILI KIPINDI CHA NYUMA YATAKUWA YAMEKWISHA.
MWISHO...........
0 comments:
Post a Comment