
Huenda ukashangaa sana kuhusu watangazaji Kate Kulo aka double K na Peter Mukabi aka masai moja wanavyofanya vyema katika tasnia ya habari na utangazaji hususan kwa watu wa kenya kwa haraka zaidi.
Kutaka kulifahamu hilo jicho la mdadis kama ilivyokawaida yake lilifunga safari mpaka nchini kenya jijini Nairobi ili kufahamu uwezo na jinsi wanavyofanya kazi ya kuelimisha jamii ya kenya kupitia taaluma zao.
Awali wakati naanza kuwatambulisha waandishi hawa ambao Peter yeye akiwa ni mzaliwa wa Musoma Mara Tanzania na Kate Kulo ni mzaliwa wa mwambao wa kenya lakini kalelewa mkoani magharibi ambako ni jimbo la kakamega watangazaji hawa ni wakenya halisi licha ya kule walikozaliwa.
Lakini chakushangaza ni pale tulipoona historia ya kujirudia ya kazi kwa watangazaji hawa vipenzi kwa wasikilizaji wengi jijini Nairobi ni baada ya kugundua kuwa wameshafanya kazi kwa takriban radio tatu nchini kenya hali iliyopelekea kudumisha upendo na ushrikiano na hata baadhi ya watu kuwabatiza jina etiiii ni mapacha lakini kingine ni uzoefu mkubwa sana kwenye fani hii ya utangazaji.
Mara nyingi wawili hawa huwa wanakuwa na ushauriano wa wenyewe kwa wenyewe na kuchangiana mawazo na jinzi ya kukiendesha kipindi chao ambayo imepata mpangilio ufaao sana yenye mvuto.
Mbali na uchapa kazi wao lakini pia ubunifu wao umechangia mafanikio makubwa katika kipindi chao na hivyo kuwafanya kuwa maarufu kivutio kwa waliowengi.
Katika mahojiano yao na jicho la mdadisi walielezea kuwa mbali na kuifanya kama sehemu ya taaluma na sehemu ya kuwaingizia kipato lakini pia wanaipenda sana kazi yao na hivyo huifanya kwa moyo wote bila kusukumwa licha ya ugumu wa maisha pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo ya habari.
Nyota fm ni miongoni mwa radio kumi bora nchini kenya kutokana na uwezo wa vijana hawa wachapakazi ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na imeendelea kujizolea wasikilizaji wengi na umaarufu uliotukuka kutokana na mchango mkubwa unaotokana na ushirikiano wa wafanyakazi wake.
PETER MUKA NA KATE KULO Wawili hawa kila wote wanafamilia na kila mmoja ana mtoto wenye umri wa miaka miwili.
Usikose kufuatilia hapa maanake jicho la mdadisi liko macho kuwafuatilia mienendo na ukuaji wao.
0 comments:
Post a Comment