Na Ahmad Nandonde,
Musoma.
JESHI la Polisi mkoani mara limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wawili waliojulikana kwa majina ya Vicent Range Magesa umri 19 na
Erick Abbas Anthony (21) kwa kosa la kumteka nyara mtoto Diana Meshaki mwenye
umri wa miezi 7 mtoto wa bi. Gaudioza Meshaki (27) kabila mhaya mkazi wa mtaa
wa nyamiongo kata ya makoko wilayani muisoma mkoani mara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 09/
01/ 2015 kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa bw. Phillip Kalangi alisema
kuwa mnamo tarehe 3 january mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi katika mtaa wa
nyamiongo kata ya makoko mjini musoma nyumbani kwa bi. Gaudioza Meshaki, binti
wa kazi aliyejulikana kwa jina la Paulina Sobe (17) kabila mkurya mwenyeji wa getabwega nchini
Kenya alimtorosha mtoto Diana na kutyokomea naye nchini Kenya.
Kamanda Kalangi alisema kuwa yalipofika majira ya
saa kumi na mbili kamili jioni mama mzazi wa mtoto huyo alipokuwa kaityokea
kazini kwake alikuta mfanyakazi wake na mtoto wake hawapo nyumbani aliamua
kutoa taarifa kwa majirani ambao waliwatafuta bila mafanikio na ndipo uamuzi wa
kutoa taarifa katika kituo kikubwa cha polisi cha musoma.
Aidha Kalangi alisema ilipofika tarehe 4 January
mama wa mtoto huyo alipigiwa simu na watu wasiojulikana wakimtaka awape kiasi
cha shilingi miloni tatu na kama asipotoa kiasi hicho cha fedha basi wangemuuza
mtoto huyo kwa watu wanaotafuta watoto.
Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa jeshi la polisi
bado linaendelea kumsaka Paulina Sobe kwa tuhuma za kumtorosha mtoto huyo
pamoja watu wengine waliohusika na uhalifu huo ili wakamatwe na kufikishwa
katika vyombo vya dola huku akiwataka wazazi kuwa makini pindi wanapoajiri
wafanyakazi za ndani kwa kuwa na kumbukumbu za wanapotoka, pamoja na
kuwatambulisha kwa viongozi wa maeneo husika wakiwamo wamiliki wa nyumba
wanazoishi ili iwe rahisi kuwafahamu ndugu zao na mahala wanapoishi ili
iwerahisi kuwapata pindi kunapotokea matataizo kama hayo.
Mama mzazi wa mtoto huyio bi. Gaudioza amesema
alilishukuru jeshi la polisi mkoani mara na jeshi polisi kanda maalumu Tarime/Rorya
kwa kushirikiana na jeshio la polisi nchini kenya kwa kufanikisha kumpata mtoto
wake.
Aidha alielezea namna watekaji hao walivyuompigia
simu huku wakimtaka awapatie fedha shilingi milioni tatu na mama huyo
alipowauliza wanazitaka hizop pesa kwaajili gani wakamjibu ili wamerejeshe
mtoto wao na asipotoa basi watamuuza kwa watu wengine ambao wanahitaji watoto
kwani wapom wengi wanaohitaji watoto.
Kwa hatua hiyo na ujasiri mkubwa mama huyo alityoa
taarifa kwa jeshi la polisi mkioani mara kwa kushirikiana na kanda maalumu
tarime/rorya na kasha kuzifuatilia namba hizo ambazo tariifa za za mwisho kabla
simu hiyo haijazima mawasiliano yaliishia sirari kwamaana kuwa watu hao
walikuwa wakitorokea nchini Kenya.
“Baada ya kufuatilia mawasiliano tuligundua watuhumiwa
hao walielekea nchini Kenya na hivyo nikaamua kumpigia simu ndgu yangu aliyeko
sirari ili awasiliane na jeshi la polisi la Kenya kwa kushirikiana na jeshi la
polisi kanda maalumu tarime /rorya amabao nao walifanikisha kuwakamata wakiwa
na mtoto wangu na hivyo wakawachukuliwa na jeshi la polisi mkoani
hapa,”alimizia Bi. Gaudioza.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliofurika katika kituo kikubwa cha polisi mjini musoma
Bi. Ghati Msamba alilishukuru jeshi la polisi kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto
huyo na kuongeza kuwa tabia za wasichana wakazi kufanya ukatili unaofanana na
huo unawanyima amani wazazi hali inayopelekea wakati mwengine wazazi kushindwa
kufanya kazi zao za kujiingizi akipato nyuimbani.
Pia alizungumzia tabia ya baadhi ya majirani kuwa
ndiyo sababu ya kuwapa viburi wafanyakazi wa ndani huiku wakiwapa maneno ya
uongo ili watoto hao warubunike na kukimbia na hata kufanya vitendo viovu.
Mwishoo….
KAMANDA PHILIP KALANGI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI
KAMANDA PHILP KALANGI AKIWA AMEMBEBA MTOTO DIANA
KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA PHILP KALNGI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
MTOTO NA MAMA YAKE PICHANI W
MAMA WA MTOTO ALIYETEKWA NA MWANANE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
MASHUHUDA WALIOFURIKA KITUO KIKUBWA CHA POLISI MJINI MUSOMA
0 comments:
Post a Comment