WAKAZI WA MKOA WA DODOMA LEO WANAUAGA MWILI WA ALIY
EKUWA MKUU WA MKOA WA MARA JOHN G.TUPPA KABLA YA KUELEKEA AMJINI KILOSA MKOANI MOROGORO KWAAJILI YA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA KESHO KIJIJINI KWAKE KILOSA.
INAELEZWA SABABU INAYOFANYA MWILI HUO KUPITIA DODODMA NI KWAMBA KWAKUA MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI KWA KIPINDI KIREFU MKOANI ODODMA AKIWA KAMA MKUU WA WILAYA BASI WAKAZI WA MJINI DODOMA WAKAONA NI BORA NA WAO WAPATE FURSA YA KUUAGA MWILI WA MPENDWA WAO JOHN TUPA.
JANA WAKAZI WA MKOA WA MARA NA VITONGOJI VYA JIRANI WALIJITOKEZA KUUAGA MWILI HUO NYUMBANI KWAKE IKULU NDOGO YA MUSOMA.
MPAKA ANAFARIKI MACH 25 ALIKUWA KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI WILAYANI TARIME AMABAPO ALITAKIWA KWENDA KUFUNGA MAFUNZO YA MGAMBO YALIYOKUWA YAKIFANYIKA HUKO NYAMONGO.
KABLA YA KUIANZA SAFARI YAKE YA KUELEKEA NYAMONGO MAREHEMU ALIKUWA AKIPOKEA TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA TOKA KWA MKUU WA WILAYA YA TARIME BW. JOHN HENJEWELE LAKINI ALIUGUA GHAFLA NA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA TARIME NA AKAFARIKI MUDA MCHACHE ALIPOKUWA AKIPATIWA MATIBABU.
MAREHEMU JOHN TUPA ATAKUMBUKWA KWA KUKEMEA MASUALA YA RUSHWA NA UCHAPAJI KAZI WAKE KWANI HAKUTAKA KABISA KUWAONA WATU WAKIZEMBEA KATIKA MAJUKUMU YAO.
MWILI WA MAREHEMU TUPA UNATARAJI KUONDOKA MAJIRA YA SAA SITA ZA MCHANA BAADA YA KUAGWA NA WAKAZI WA MJI HUO KUELEKEA MJINI KILOSA AMBAPO UTAKABISHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU NA KESHO TAREHE 29 MWILI HUO UTAAGWA KWA MARA YA MWISHO AMBAPO ZOEZI HILO LITAAMBATA NA IBADA MAALUMU YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU NA KISHA KUELEKEA KATIKA MAKABURI KWAAJILI YA KUUHIFADHI MWILI WA MAREHEMU TUPPA.
MAREHEMU TUPA ALIZALIWA JANUARI MOSI MWAKA 1950 NA AMEACHA MKE NA WATOTO WA TANO.
WAISLAMU TUNASEMA "SISI SOTE NI WA MOLA NA KWAKE TUTAREJEA"
0 comments:
Post a Comment