`

Home » » ENDELEA KUFUATILIA MKASA WA KIJANA FABBY KUTOKA MTWARA SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA.

ENDELEA KUFUATILIA MKASA WA KIJANA FABBY KUTOKA MTWARA SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA.

MKASA SEHEMU YA PILI...............




FABI ALIPOTAKA KUINGIA NDANI GHAFLA ALISIKIA KAMA KUNA MTU ANAMGUSA BEGANI LAKINI ALIPOGEUKA NYUMA HAKU HAKUONA MTU KISHA AKASIKIA TENA KAGUSWA BEGA JINGINE ALIPOGEUKA ALIMUONA YULE KIUMBE ANAYEVAA KAMA MASISTA HALI ILIYOMFANYA KUOGOPA KIASI AMBACHO YALE MAJI ALIYOKUWA AMEYABEBA KWAAJILI YA KWENDA KUOGA KUMWAGIKA LAKINI HATA HIVYO KUONEKANA KWA HUYO SISTA HAKUKUWA KWA KUSHIRIA SHARI KWANI ALIKUWA KIMTAZAMA KIJANA HUYO KWA HURUMA KUBWA NA HIVYO KUMFANYA KUDUWAA KWA DAKIKA KASHAA HIVI HUKU AIJUE NINI CHA KUFANYA.

AKIWA NAENDELEA KUMTAZAMA YULE SISTA GHAFLA ALITOA KITU NA KUMUONESHA NA ALIPOTAZAMA KWA UMAKINI ALIONA KAMA NOTI TATUI ZIKIWA NA RANGI TOFAUTINA ALIPOZITAZAMA KAMA HELA HIZO NI ZA WAPI HAKUWEZA KUZITAMBUA KUWA ZILIKUWA NI ZA NCHI GANI MAANA HATA HAZIKUWA ZA TANZANIA JAPO KWA KUZITAZAMA ALIZIONA KUWA ZILIKUWA NI HELA LAKINI PAMOJA NA FABBY KUENDELEA KUZICHUNGUZA YULE SISTA ALIENDELEA KUMUONESHA TU ZILE NOTE PASIPO HATA KUMUONGELESHA JAMBO LOLOTE KISHA AKATOWEKA KAMA KAWAIDA YAKE, HUKU AKISINDIKIZWA NA MWANGA MKALI.

WAKATI FABBY AKIWA AMESIMAMA KATIKA MLANGO WA BAFU KWA MUDA HUKU AKIJIULIZA JUU YA JAMBO LILILOJITOKEZA NA HAYO YANAYOMTOKEA PASI NA KUPATA MAJIBU HUKU AKIENDELEA KUTAFAKARI KICHWANI KWAKE GHAFLA AKAANZA KUTOKWA NA MACHOZI KUTOKANA NA MAMBO HAYO BASI AKAINAMA NA KUCHUKUA NDOO YAKE TUKUMBUKE KUWA WAKATI ANAMUONA YULE MTU ALIYEVALIA VAZI LA KISISTA MAJI ALIYOKUWA ANAENDA NAYO BAFUNI YALIMWAGIKA HIVYO AKAAMUA KURUDI TENA BOMBANI ILI AKACHOTE YTENA MAJI ILI AKAOGE WAKATI ANASHUKA NGAZI ZA BAFU AKASIKIA SAUTI YA MWANAMKE INAMUITA NA ALIPOTAZAMA TU AKAKUTA NI BINTI AMBAYE YEYE ANAMFAHAMU KAMA NI JIRANI YAKE PALE ANAPOISHI.

BINTI YULE ALIMSOGELEA KISHA AKAMPATIA KIASI CHA SHILINGI ELFU THELATHINI NA ZILIKUWA NOTI TATU ZA ELFU KUMI NA BINTI HUYO AKAMWAMBIA MAMA KANITUMA NIKULEE.

FABBY AKAPOKEA KIASI HICHO CHA FEDHA PASIPO NA SWALI LA ZIADA KWANI ALIKUWA AKIFAHAMU FIKA FEDHA HIYO LILIKUWA NI ALILOKUWA AKIMDAI MAMA WA MTOTO HUYO WAKATI MAMA HUYO ALIPOKWENDA KUKOPA NGUO.

FABBY AKATEMBEA HATUA KADHAA LAKINI KABLA YA KUINGIA NDANI AKAAMUA KUKAA KWENYE NGAZI ZA KUINGILIA NDANI, HUKU AKIJWA NA MAWAZO JUU YA MATUKIO HAYO YA HARAKA KIASI HICHO KISHA AKAANZA KUZIANGALIA ZILE FEDHA TENA  NA KUJIULIZA IWEJE YULE KIUMBE AMTOKEE NA HUKU AKIWA AMESHIKA NOTI TATU NA MUDA SI MREFU AKALETEWA FEDHA HUKU ZIKIWA NI NOTI TATU INGAWA NI TOFAUTI NA ZILE ZA YULE SISTA? ALIENDELEA KUJIULIZA.

LAKINI WAKATI BADO AKIWA MLANGONI MAMA YAKE ALITOKA NJE NA KUMKUTA PALE MLANGONI AKAMUULIZA KULIKONI MBONA HATA HUJAOGA, FABBY AKAAMUA KUMJIBU KWA JIBU LENGINE TU WALA WALA SI KAMA ALIVYOOULIZWA AKIWA NA MAANA YA KUMZUGA MAMA YAKE ASIJUE JUU YA KILICHOMTOKEA KWANI ALIHISI KAMA ANGEMJIBU BASI ANGEWEZA KUMSTUA SANA MAMA YAKE NA KISHA KUMPATIA MAMA YAKE ZILE HELA ZOTE ILI AZITUMIE KAMA NAULI KWA LENGO LA KUMSAIDIA MAMAAKE KULE MSIBANI.

BASI BAADA YA MAMA YAKE KUPATIWA FEDHA ALIANZA MAANDALIZI YOTE YA SAFARI KISHA AKAONDOKA KWENDA MSIBANI, NA SIKU INAYOFUATA NAYE KESHO YAKE AKAFANIKIWA KUPATA FEDHA TOKA KWA RAFII YAKE NA KISHA KUUNGANA NA FAMILIA YAKE MSIBANI.

BAADA YA SHUGHULI ZOTE ZA MSIBA KUMALIZIKA HUKU MAJIRANI, MARAFIKI NA WAGENI WENGINE WALIOFIKA MSIBANI MAMA YAKE MZAZI ALIAMUA KUWAITA BAADHI YA NDUGU WALIOKUWA PALE MSIBANI AKAANZA KUWASIMULIA YANAYOMTOKEA KIJANA WAKE AKIMAANISHA FABBY NA HATA NAMNA ALIVYOWEZA KUMJULISHA KUHUSIANA NA TUKIO LA HUO MSIBA.

BAADHI YA NDUGU WALISHANGAA SANA NA KILA MTU AKAWA NA LAKE KUHUSIANA NA MAMBO YANAYOMTOKEA FABBY HUKU WENGINE WAKISHAURI ETII! APELEKWE KWA WAGANGA WA KIENYEJI, WENGINE WALISHAURI APELEKWE KANISANI NA KWINGINEKO KWA AJILI YA MAOMBEZI YAANI KILA MTU AKAWA NA LAKE HATA KUFIKIA WAKATI KUHUSISHA MATUKIO HAYO KUWA YANAENDANA NA BAADHI YA MILA ZA UKOO WAO WAKIAMBATANISHA MATUKIO MBALI MBALI YA KIPINDI CHA NYUMA YALIYOWAHI KUTOKEA KWENYE HUO.

BASI BAADA YA MSIBA FABBY AKAREJEA NYUMBANI KWAO SIKU MOJA MIDA YA MCHANA AKIWA HANA CHA KUFANYA ALIAMUA KUCHUKUA KITI AMABCHO KWA WATU WAKUSINI HUKIITA KITI CHA MALIMBA NA  AKATOKA NACHO NJE NA KWENDA KUKAA KIVULINI KWENYE MTI MMOJA WA MWEMBE HAPO HAPO NYUMBANI KWAO.

ALIKAA HAPO KIVULI KWA MUDA KWA KADHAA LAKINI MWISHOWE AKAPITIWA NA USINGIZI GHAFLA AKASIKIA KICHEKO NYUMA YAKE YAANI KAMA KUNA MTU AMESIMAMA NYUMA YAKE AKIWA ANACHEKA, NA ALISHTUKA AKAONA AGEUKE NA AANGALIE KUNANI ALIPOGEUKA NYUMA ALIMUONA KICHAA MMOJA AKIWA AMEVALIA MAVAZI MACHAFU SANA HUKU AKICHEKA CHEKA OVYO HUKU AKIMTAZAMA FABBY NA HII ILIKUWA IKIMAANISHA KUWA KICHAA HUYO ALIKUWA ANAMCHEKA FABBY.

BAADA YA KUONA HALI HIYO FABBY NAYE AKAANZA KUMTAZAMA YULE KICHAA HUKU AKIJIULIZA HUYU KICHAA ANATOKA WAPI MAANA ALIKUWA MGENI SANA MACHONI PAKE YAANI HAJAWAHI KUMUONA HATA MARA MOJA.

FABBY ANASEMA PAMOJA NA UENYEJI WAKE WOTE PALE MTWARA HAJAWAHI KUMUONA YULE KICHAA HATA MARA MOJA LAKINI ALIPOENDELEA KUMTAZAMA VIZURI ALIMUONA YULE KICHAA AKIWA AMEBEBA  MFUKO WA NAILONI HUKU AKIWA AMEUHIFADHI KATIKA MAZINGIRA YA USAFI TOFAUTI NA ILIVYO KWA KWA WATU WA AINA HIYO.

WAKATI KICHAA AKIWA ANAONDOKA HUKU AKIRUDI NYUMA KICHAA HUYO ALITOA KITABU KIMOJA KWENYE ULE MFUKO, KITABU AMBACHO KILIKUWA KIMETUNZWA VIZURI MNO BAADA YA FABBY KUKIONA KILE KITABU ALIAMUA KUMUOMBA KILE KITABU KWA MAZINGIRA YA KUMTANIA TANIA CHA KUSHANGAZA YULE KICHAA KWA CHEKO ZAKE HICHO HICHO ALIMSOGELEA NA KISHA KUMPATIA FABBY KILE KITABU, NA BAADA YA KUPATIWA KILE KITABU ALIKITIZAMA KWA UMAKINI KILE KITABU LAKINI HAKUKIELEWA MANENO YAKE  NA KILIKUWA KIMEANDIKWA KWA MAANDISHI YA LUGHA YA KILATIN HIVI, NA KUISHIA KUKIFUNUA FUNUA TU NA KISHA AKAAMUA KUMUOMBA KITABU KINGINE.

YULE KICHAA AKATOA KITABU KINGINE NA KUMPATIA FABBY AMBAPO KITABU HIKO KILITOFAUTIANA RANGI NA KILE KITABU CHA MWANZO, NA ALIPOKITAZAMA PIA HAKUKIELEWA JAPO KINAONEKANA NI KITABU SAFI KINA MAANDISHI NA PICHA PICHA ILA LUGHA ILIYOTUMIKA ILIENDELEA KUWA KITENDAWILI KWAKE KUTOKANA NA KUTOIELEWA LUGHA ILIYOTUMIKA.

AKIWA BADO ANATAMANI KUTAZAMA KITABU KINGINE NINI IKIMEANDIKWA NDANI YA KITABU HIKO ALIAMUA KUMUOMBA TENA AMUONESHE KITABU KINGINE KILICHOSALIA YAANI AKAWA ANAMUOMBA LAKINI KWA AWAMU HII YULE KICHAA HAKUONESHA KUJALI AKAWA ANACHEKACHEKA TU NA BAADAYE AKAMKATALIA KABISA KUMUONESHA KITABU HICHO CHA TATU NA KISHA KICHAA HUYO AKAAMUA  KUONDOKA POLE POLE HUKU ANACHEKA BAADA YA KUFIKA HATUA KADHAA NYUMA ALIKITOA KILE KITABU NA AKAMUONESHA FABI YAANI KAMA ANAMRINGISHIA NA FABBY ALIPOKIONA KITABU HICHO KILICHOKUWA NA RANGI NYEKUNDU TOFAUTI NA VITABU VINGINE LAKINI NACHO KAMA KAWAIDA JINSI ALIVYOKUWA ANAKITAZAMA AKASHINDWA KABISA KUIELEWA LUGHA ILIYOTUMIKA KAMA ILIVYOKUWA KWA VITABU VINGINE.

YULE KICHAA AKAONDOKA HUKU AKIMWAMBIA HIKI HUTOKIPATA MPAKA UTAKAPOTIMIZA MAMBO MATATU FABBY ALIONESHA KUSHANGAZWA MNO NA MWISHOWE IKABIDI AANZE KUVITAZAMA VILE VITABU LAKINI JINSI ANAVYOVITAZAMA NDO HAELEWI KABISA NA AKAONA HAKUNA HAJA AKAAMUA KUJILAZA TENA KATIKA KILE KITI CHAKE CHA MALIMBA NA GHAFLA AKASIKIA KAMA HALI YA HEWA IMEBADILIKA GHAFLA YAANI KUKAWA NA HARUFU NZURI NA UPEPO UNAOVUMA TOFAUTI NA AWALI.

FABBY ANASEMA MWANGA ULIOONGEZEKA, HALI ILIYOMPELEKEA KUKAA VIZURI MBELE YAKE AKAMUONA YULE KIUMBE TENA (YULE SISTA) NA AKAMWAMBIA JAMBO FUPI TU KISHA AKATOWEKA, AKAMWAMBIA "FABBY KILA KINACHOTOKEA KWAKO KINA MAANA KWA HIYO ZINGATIA MAMBO MATATU HUKU AKIJIULIZA JAMBO HILO LINA MAANA GANI KATIKA MAISHA YAKE, AKAVITAZAMA TENA VILE VITABU KISHA AKAJIULIZA NI KWANINI YULE KICHAA HAKUMPA KITABU CHA TATU.

BAADA YA MUDA ALITAFAKARI JAMBO FLANI LAKINI HAKUPATA JIBU YAANI KUHUSU HIVI VITATU, AKIANZIA ZIOLE FEDHA MAANA MWANZONI ALIONESHWA NOTI TATU, LAKINI BAADA YA MUDA ALILETEWA DENI LAKE LA HELA IKIWA NI NOTI "TATU" LAKINI PIA HUYU KICHAA KAJA NA VITABU VITATU NA KUMPA VIWILI JAPO CHA TATU ALIKATALIA.

BASI SIKU ZIKAENDA ZIKARUDI NA BAADHI YA VITENDO KUTOKA KWA HUYO SISTA ALIANZA KUVIZOEA KWA KIASI FLANI NA KWA MUDA WOTE HUU FABBY ALIKUWA BADO YUKO KWAO LICHA YA KUWA ANAFANYA BIASHARA ZAKE, LAKINI ILIFIKIA WAKATI AKAONA AMEKUA KIJANA MKUBWA NA AKAONA NI BORA SASA AJITEGEMEE, KWELI ALIONDOKA PALE KWAO AKAENDA KUPANGA MTAA MWINGINE HUKO HUKO MTWARA.

MAISHA YALIENDELEA KAMA KAWAIDA BAADA YA "KAZI " ANARUDI KWAKE KILA ANAPOPATA PESA ANAFIKIRIA NINI AFANYE KWA MAENDELEO YA "CHUMBANI KWAKE " NA HARAKATI NYINGINE ZA KIMAISHA LAKINI KATIKA MUDA WOTE HUO HAKUWEZA KUTAMBUA BAADHI YA MABADILIKO YALIYOKUWA YANATOKEA PALE KWAKE HADI WATU WENGINE HASA MARAFIKI WAKAWA WANAMSIFIA KUHUSIANA NA MAENDELEO YA GHAFLA.

SIKU MOJA FABBY AKIWA KAZINI KICHWA KILIANZA KUUMA ALIVUMILIA BAADAYE YAKAMSHINDA IKABIDI "AFUNGE BANDA LAKE LA MITUMBA AMABAPO VIJANA WA MJINI WANAITA "GOLI LAKE LA MITUMBA" KISHA AKAONDOKA KWENDA NYUMBANI KWAKE NA WAKATI HUO ILIKUWA NI MAJIRA YA SAA 11 JIONI.

ALITEMBEA KUELEKEA NYUMBANI LAKINI BAADA YA MWENDO KIDOGO ALIPOFIKA NJIANI ALISIKIA MUUNGURUMO KAMA RADI KUTOKA JUU ANGANI AKASIMAMA NA KUANGALIA JUU NA WAKATI ANAANGALIA JUU AKAONA WINGU JEUSI SANA KLIMETANDA KATIKATI YAKE KAMA KUNA KITU FLANI KINAWAKA ILA SI JUA.

SASA WAKAKTI ANASHAANGAA HALI HIYO GHAFLA KATIKA KATI YA LILE WINGU AKAONA SURA KAMA YA YULE KIUMBE AKIWA ANANG'ANG'ANA KWENDA KWENYE ULE MWANGA NA UPANDE MWINGINE LILE WINGU JEUSI NALO KAMA LINAZUIA ASIENDE KWENYE ULE MWANGA FABBY AKAJIKUTA ANAZUBAA KUANGALIA LILE TUKIO LA AJABU...WAKATI ANASIMAMA ILI KUSHAANGAA VYEMA ANATOKEA MPITA NJIA MWINGINE NAYE AKIANGALIA KULE ANAPOANGALIA FABBY NAYE AKAUNGANA NA FABBY NA KUANZA KUANGALIA KUNA NINI JAMAA ANACHOSHANGAA LAKINI HAKUWEZA KUONA KITU.

FABBY ANASEMA MWANZONI ALISIKIA YOTE ALIYOKUWA ANAULIZWA NA YULE JAMAA LAKINI GHAFLA HAKUWEZA TENA KUSIKIA CHOCHOTE IKAWA KAMA KAHAMISHWA KIFIKRA.

FABBY ANASEMA AKIWA ANATAZAMA KINACHOENDELEA ANGANI, WAKATI YULE SISTA ANANG'ANG'ANA KUPITA KATIKA LILE DUARA LINALOONEKANA KAMA WINGU JEUSI SANA KULIKO KAWAIDA GHAFLA KATIKA LILE WINGU KUNA VITU VILIFYATUKA VIKAMGONGA YULE SISTA AKAONEKANA KUTUPWA MBALI, YULE SISTA NA HIVYO KUMLAZIMU SISTA KULIA KWA SAUTI AMBAYO FABBY ANASEMA ILISIKIKA KAMA ANALILIA KWENYE UBONGO WAKE HAPO HAPO AKASIKIA MAUMIVU MAKALI KISHA AKADONDOKA CHINI CHALI HUKU MACHO YAKIWA BADO YANATIZAMA YANAYOENDELEA KULE JUU (UKWELI NI KWAMBA KATIKA TUKIO HILO MPAKA YEYE ANADONDOKA CHINI HAKUJITAMBUA ILA ALIAMBIWA BAADAYE.

BASI KATIKA TUKIO HILO ALIMUONA YULE SISTA AKIWA AMEKASIRIKA SANA NA ANALILITAZAMA LILE DUARA GHAFLA KUTOKA ULE UPANDE WA SISTA ALITOKEZA YULE NDEGE TUMBUSI ALIYEMUONA PALE KWAO SIKU ILE YA KWANZA (NI NDEGE JAMII YA MWEWE), YULE NDEGE ALIONEKANA KWENDA KWA KASI KAMA MSHALE KUELEKEA KATIKA LILE DUARA NA SISTA ALIKUWA ANAFUATA NYUMA YAKE MITHILI YA  YA RISASI ALILICHANA LILE DUARA LIKATAWANYIKA KATIKATI NA SISTA AKASOGEA KWENYE ULE MWANGA ULIOKUWA UMEKINGWA NA HILO DUARA AKANYOOSHA MKONO KISHA ULE MWANGA ULING'AA ZAIDI KISHA SISTA NA YULE NDEGE WAKATOWEKA.

BAADA YA KUTOWEKA TU HAPO HAPO FABI AKASHTUKA KAMA ANATOKA USINGIZINI, ANASHANGAA KUKUTA WATU WAMEMZINGIRA KILA MTU AKIONGEA LAKE WENGINE WALISEMA WALIMUONA AMESIMAMA AKIANGALIA JUU KAMA DAKIKA 15 KILA MTU AKAANZA KUJIULIZA HUYU KIJANA VIPI NA KILA WALIPOKUWA WANAMUONGELESHA ALIKUWA AMEGANDA KAMA SANAMU, SO ALIPODONDOKA WENGINE WAKAHISI WENDA ANAKIFAFA LAKINI KILA WALIPOKUWA WAKIMTAZAMA WALA HAKUONSEHSA KUWA NA DALILI ZOZOTE ZA KUWA NA UGONJWA HUO.

FABBY ALIAMKA KUTOKA PALE CHINI LAKINI CHA AJABU ZAIDI KICHWA KILIKUWA KIMEPONA YAANI HATA DALILI ZA MAUMIVU HAZIKUWAPO NA KUJIKUTA AKIINGIWA NA SHAUKU YA KUTAKA KUREJEA TENA KAZINI ILI AKAMALIZIE KAZI YAKE LAKINI AKAONA BASI TU ACHA AENDE ZAKE NYUMBANI AKAJIPUMZISHE.

ALIPOFIKA NYUMBANI KWAKE, AKAFUNGUA MLANGO LAKINI KABLA HATA HAJAINGIA NDANI ALISIKIA HARUFU NZURI SANA, NA ALIPOINGIA NDANI  GHAFLA KWENYE KITANDA CHAKE AKAMKUTA BINTI AMELALA, HEEE!!! AKASTUKA NA KUJIKUTA AKIMUULIZA WEWE NANI NA UMEFIKAJE HUMU" ? BINTI HUYO ALIKUWA AMELALA KIFUDIFUDI KICHWA KIMETIZAMA CHINI ALIONEKANA AKIWA ANAAMKA KWENYE KITANDA HUKU AKIWA KAMA AMEBANWA SANA NA KICHEKO.

BINTI HUYO AMBEYE FABBY ANAMUELEZEA KUWA ALIKUWA NA UZURI USIOELEZEKA BINTI HUYO ALIINUKA NA KISHA KUSIMAMA KARIBU NA KITANDA KISHA AKAMTAZAMA FABBY NA BINTI HUYO AKAMWAMBIA "WALA USIWE NA HARAKA YA KUNIJUA UTANIFAHAMU UKIKAMILISHA MASHARTI MATATU".

FABBY ALIVYOSIMAMA KWA JINSI ALIVYOKUWA ANAONEKANA AKAHISI SIYO BINTI WA KAWAIDA HADI NYWELE KICHWANI ZIKASISIMKA GHAFLA YULE BINTI AKATEMBEA HATUA TATU ZA MBALI MBALI YAANI AKAWA ANAONEKANA AKIPIGA HATUA HAPA NA PALE KULE KISHA AKATOWEKA NA HIVYO KUMUACHA FABBY AKIBAKIA NA UOGA USIO KIFANI NA KUAMUA KUTOKA NDANI FASTA HUKU AKIUBAMIZA MLANGO  KWA NGUVU ALITOKA NA KUKAA NJE YA MLANGO HUKU JASHO LIKIMTIRIRIKA NA ASIJUE NI WAPI KIUMBE HUYO ANATOKEA MAANA MUONEKANO NA MATENDO YAKE NI TOFAUTI KABISA NA YULE KIUMBE MWINGINE ANAYEVAA MAVAZI YA KISISTA.

JE! UNATAKA KUMJUA KIUMBE HUYO MWINGINE AMBAYE ANAMTAJA KUWA NI MTATA KUPITA MAELEZO NA MWENYE MAAJABU MENGI JE! NI WAPI ANATOKEA NA KIPI ANAKUJA NACHO JE! UJIO WA HUYO KIUMBE MPYA UNAKUJA NA SULUHU YA MAISHA YA FABBY AU NDO ANAKUJA NA MAJANGA ZAIDIIII?

KUJUA JUU YA KINACHOENDELEA NDANI YA MKASA HUU SEHEMU YA TATU ENDELEA KUTEMBELEA JICHOLAMDADISI.BLOGSPOT.COM KILA SIKU YA JUMANNE NA IJUMAA... www.jicholamdadisi.blogspot.com



0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK