MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU EDWARD HOSEAH AKIINGIA
JENGO JIPYA LA TAKUKURU MKOANI MARA.
PICHA NA BINDA BLOG:
MUSOMA:
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA MKOANI MARA,
LEO IMEZINDUA RASMI
JENGO LAKE
LILLILOPO KATIKA MAENEO YA BARUTI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA.
AKIZUNGUMZA KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA JENGO HILO
MKURUGENZI MKUU YA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NCHINI, DKT EDWARD
HOSSEAH AMESEMA MIKAKATI YA KUDUMU NA ENDELEVU AMBAYO IMEWEKWA NA TAASISI HIYO
NI PAMOJA KUJENGA OFISI TATU KWA KILA
MWAKA NA KUONGEZA KUWA HADI SASA TAASISI HIYO IMEJENGA JUMLA YA MAJENGO 13 KATIKA MIKOA MBALIMBALI HAPA NCHINI.
KATIKA HOTUBA YAKE HOSSEAH AMESEMA TAASISI HIYO BADO
INAENDELEA NA UJENZI WA OFISI ZAKE KATIKA MIKOA YA MBEYA, KIGOMA, NA KATIKA
WILAYA MKINGA YA MKOANI PWANI HUKU AKIWATAKA WATUMISHI WA TAKUKURU NCHINI KOTE
KUTUNZA MAJENGO HAYO VIZURI ILI YAWEZE KUHUDUMIA VIZAZI VIJAVYO NA KUAHIDI
KUTOA SAMANI NA VITENDEA KAZI VITAKAVYOENDANA NA MAJENGO HAYO.
HATA HIVYO DKT HOSSEAH AMEONGEZA KUWA TAKUKURU
IMEAZIMIA KUONGEZA KASI KATIKA VITA YA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA KUSHIRIKIANA NA
MIHIMILI YOTE MITATU YA DOLA AMBAYO NI SERIKALI, BUNGE, NA MAHAKAMA KATIKA
KUDHIBITI VITENDO VISIVYO VYA UADILIFU NA RUSHWA.
AIDHA DKT HOSSEAH AMEBAINISHA KUWA KATIKA JITIHADI
AMBAZO ZIMEFANYWA NA TAKUKURU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KWA KIPINDI CHA
MWEZI JANUARI HADI DESEMBA MWAKA 2013, TAASISI HIYO IMEFANIKIWA KUFUNGUA KESI
MPYA ZAIDI YA 370 KUPITIA UCHUNGUZI WAKE
NA KUFANIKIWA KUOKOA KIASI CHA SHILINGI BILIONI NNE MILIONI MIA MBILI
THELATHINI NA TANO LAKI NNE NA ELFU KUMI NA MOJA MIATANO TISINI NA MOJA.
MWISHO.....
0 comments:
Post a Comment