NIWAOMBE RADHI WASOMAJI WA MKSA HUU KUWA HAUKUWEZA KWENDA HEWANI JANA IJUMAA KUTOKANA NA TATIZO LA KIUFUNDI KIDOGO LAKINI KWA SASA MAMBO YAKO SAFI
ENDELEAKUBURUDIKA
SEHEMU YA TATU
YA FABBY
BAADA YA TUKIO HILO LA
FABI KUONANA NA KIUMBE HUYO WA PILI KWELI ILIMSHTUA SANA LAKINI AKAWA HAELEWI
KUHUSU HAWA VIUMBE KWAMBA WAPO PAMOJA AU LAA.
ANASEMA SIKU HIYO
ILIPITA PASIPO KUONANA NAYE TENA JAPO MUDA WOTE AKIWA CHUMBANI FABBY ALIHISI
YULE KIUMBE ATARUDI LAKINI HAIKOTOKEA KWA SIKU HIYO.
BAADA YA KUPITA SIKU
KADHAA AKIWA NJE MIDA YA SAA TANO USIKU AMBAPO ANASEMA ALIKUWA NA MAZOEA YA
KUFANYAFANYA MAZOEZI NYAKATI ZA JIONI KABLA YA KUOGA NA KULALA SASA KWA SIKU
HII BAADA YA MAZOEZI KIDOGO AKAWA AMEPUMZIKA PALE NJE YA NYUMBA NA BAADAE
AKATAKA KWENDA NDANI LAKINI ALIPOAMKA TU ANATAKA KUINGIA NDANI GHAFLA ALISIKIA
KUNA SAUTI INAMUONGELESHA NA ILE SAUTI ALIITAMBUA KUWA NI YA YULE KIUMBE MTATA
JAMAA ANASEMA ALISIKIA
INAMWAMBIA WAONANE SEHEMU FLANI (JINA NITALIHIFADHI) AMBAPO NI UFUKWENI MIDA YA
USIKU FABI ANASEMA ALIJIKUTA TU ANAMJIBU KUWA HATAKI LAKINI SAUTI ILE ILIMSIHI
NA KUMWAMBIA HAKUNA LOLOTE BAYA LITAKALOMTOKEA KWANI ITAKUWA KARIBU NAYE
IKIMWEKEA ULINZI LAKINI JAMAA ALIKATAA NA KUINGIA NDANI.
FABBY ANASEMA SIKU HIYO
WALIKUWEPO NA RAFIKI ZAKE WENGINE AMBAO NI WAPANGAJI WENZAKE WALIKUWA WANAPIGA
STORI NDANI MWAKE NA ALIVYOINGIA NDANI AKAWAAMBIA KUHUSIANA NA SUALA HILO
AMBAPO WALE RAFIKI ZAKE WAKAMTAKA KUTOKWENDA KWENDA HUKO AMBAPO BAADA YA
MAONGEZI YAO KILA MMOJA AKAONDOKA KWENDA KWENYE CHUMBA CHAKE KWAAJILI YA
KUJIPUMZISHA.
USIKU HUO HUO MAJIRA YA
SAA SABA FABBY AKIWA AMELALA GHAFLA AKASIKIA SAUTI YA MELI KANA KWAMBA YUKO
BANDARINI GHAFLA AKASHTUKA NA KUJIKUTA NDANI YA MELI AMBAYO HAJAWAHI KUIONA
KATIKA MAISHA YAKE NA ALIPOJARIBU KUITAZAMA VIZURI GHAFLA AKAJIKUTA YUKO KATIKA
KATI YA BAHARI NA ALIPOJARIBU KUANGALIA MBELE AKAMUONA YULE KIUMBE MWINGINE
(AMBAYE MWENYEWE AMEZOEA KUMUITA MTATA) KWA MARA YA PILI BAADA YA KUMUONA HUYO
DADA MTATA HUKU AKIWA ANATAZAMA MBELE MELIINAPOELEKEA HUKU AKIWA AMEMPA MGONGO
KAMA KAWAIDA AKAJIKUTA ANABANWA NA KICHEKO AMBACHO ALIJARIBU KUJIZUIA ILI YULE
DAD ASIJUE KAMA ANACHEKA.
LAKINI YOTE TISA LAKINI
AKAMUONA YULE DADA AKIWA AMEVAA MAVAZI YANAYOMFANANISHA NA MSANII FLANI MKUBWA
KAMA BEYONCE AKIPANDA JUKWAANI KWA AJILI YA SHOO HUKU KICHWANI AKIWA AMEVALIA
KOFIA NYEUSI YA ROUND AMBAZO WENGI HUPENDA KUZIITA "COW BOY' AU MARLIBORO.
FABBY ALIPOJARIBU
KUMUONGELESHA GHAFLA TU ALIJIKUTA YUKO KWENYE JENGO KUBWA SANA LINALOFANANA NA
MAJENGO YA KALE AU MAGOFU FLANI WAKATI HUO YULE KIUMBE ALIKUWA AKITEMBEA HUKU
FABBY AKIMFUATA NA MARA BAADAYE YULE KIUMBE ALIAMUA KUMSUBIRI FABBY NA
ALIPOFIKA AKAANZA KUMUONESHA SEHEMU NYINGI NA ZA KUTISHA SANA NA VINGINE VYA
THAMANI SANA HUKU AKIMWAMBIA KUWA "HUU NI
UTAWALA AMBAO UTAKUWEPO MUDA UKIFIKA" .
BAADA YA KUSIKIA MANENO
YALE FABBY ANASEMA ALIJIKUTA ANAMTAMKIA "HIVI MIMI NIMEWAKOSEA NINI MPAKA MNANITESA NAMNA HII" LAKINI
YULE KIUMBE ALIMWAMBIA WALA USIWE NA HARAKA SIKU MOJA UTAJUA TU ENDAPO UTAKAMILISHA
YALE MASHARTI MATATU FABBY ALIMUULIZA NI MASHARTI GANI HAYO LAKINI YULE KIUMBE
HAKUJIBU ALIANGUA KICHEKO AMBACHO KILITOA KELELE YA AJABU AMBACHO HAJWAHI
KUKISIKIA TANGU KUZALIWA KWAKE.
LAKINI BAADA YA KICHEKO
KILE KUMALIZIKA GHAFLA FABBY AKAJIKUTA AKIWA CHUMBANI KWAKE HUKU AKIWA
AMESIMAMA WIMA KATIKA KATI YA CHUMBA.
KUFUATIA TUKIO HILO HAPO HAPO AKAJIKUTA AKIBUBUJIKWA NA MACHOZI NA NDIPO
IMANI YA KUWA TUKIO HILO
HALIKUWA NDOTO LIKAMJIA.
KITENDO HICHO PIA
KILIMFANYA AWE NA RTAFAKARI NYINGI SANA JUU YA ALICHOKIONA KATIKA ILE SAFARI
YAKE NA KUANZA KUJIULIZA NI BORA BASI ANGEJIKUTA KITANDANI AMELALA MAANA WAKATI
HUO YEYE ALIKUWA BAADA YA KUJIULIZA MASWALI MENGI BILA MAJIBU AKAAMUA KUTEMBE
MPAKA KITANDANI KWAKE NA KUKAA NA ALIPOANGALIA SAA YAKE YA UKUTANI AKAKUTA NI
SAA KUMI NA MOJA KASORO ALFAJILI.
ANASEMA USINGIZI
HAKUUPATA TENA NA KULIPOPAMBAZUKA AKAAMUA KUWASIMULIA WENZAKE JUU YA TUKIO HILO
NA SAFARI YAKE HIYO AMBAYO HAKUITARAJIA HALI ILIYOPELEKEA WENZAKE HAO KUANZA
KUMSIKITIKIA NA KUMWAMBIA "SASA HIYO NI
HATARI KAMA INAFIKIA HATUA YA KUPELEKWA MAENEO KAMA HAYO? BASI UNASHIDA YANI
LICHA YA KUMWAMBIA HAUTAKI LAKINI HAIKUWEZEKANA"
MAISHA YALIENDELEA NA
MAMBO YA KUTOKEWA NA HAO VIUMBE YAKAWA NI MOJA YA SEHEMU YA MAISHA YAKE.
LAKINI KWA UPANDE MWENGINE
AKAWA ANATOKEWA NA YULE KIUMBE MWINGINE MWENYE MAVAZI YA KISISTA ALIPATA
AHUWENI KIDOGO KULIKO ANAPOTOKEWA NA YULE MTATA BASI AMANI HUMPOTEA KUTOKANA NA
JINSI ANAVYOTOKEZA NA KUPOTEA KITU AMBACHO HUMUOGOPESHA SANA HALI INAYOMFANYA
KUTOZOEA YAANI NGUMU KUZOEA LICHA YA KUWA ALIANZA KUZOEA MAONGEZI YAKE.
JAMAA ANASEMA MAISHA
YALIENDELEA LAKINI KUMBE KUNA BAADHI YA VITU AMBAVYO VILIKUWA VINAENDELEA
AMBAVYO HAKUWEZA KUVITAMBUA AMBAPO ALIKUJA KUVIGUNDUA BAADAYE ALIPOPATA MPENZI.
ANASEMA ALIPATA DADA
MMOJA MBAYE WALIPENDANA SANA AMBAPO KILA NAFASI ILIPOKUWA INA PATIKANA WALIKUWA
WANASHINDA WOTE PALE HOME YAANI WANAPIKA, WANAKULA NA STORI ZINGINE KIBAO
LAKINI INAPOFIKA JIONI YULE DADA ANAONDOKA KURUDI KWAO.
BASI HII IKAWA NI MAZOEA
YA YULE DADA YAANI KATIKA SIKU ZILE AMBAZO JAMAA HAENDI KAZINI BASI HUYU DADA
ALIKUWA ANAENDA KUSHINDIA KWAKE. LAKINI TABIA NI MATOKEO YA MAZOEA KWA MSINGI
HUO BASI DADA HUYU ALIJIKUTA WAKATI MWINGINE JAMAA ANAPOONDOKA ANAMUACHA PALE
HOME NAYE ANAONDOKA KWA MUDA WAKE.
LAKINI IKAENDA MBELE
ZAIDI HATA WAKATI MWINGINE AKAWA ANAENDA PALE "GHETO" HATA KAMA JAMAA
HAYUPO NA ANAMSAIDIA MAJUKUMU MENGINE KAMA KUPIKA NA USAFI WA MAZINGIRA PALE
HOME.
LAKINI KUMBE KUNA BAADHI
YA MAMBO YALIKUWA YANAENDA NDIVYO SIVYO PALE NYUMBANI AMBAYO HUYU DADA YALIKUWA
YANAMCHANGANYA AMBAPO KWA HATUA ZA KWANZA HAKUWEZA KUZITAMBUA LAKINI ILIFIKA
WAKATI YAKAMSHINDA.
JAMAA ANASEMA SIKU MOJA
ANASHANGAA MPENZI WAKE HUYU ANAMWAMBIA "
MIMI HAPA KWAKO SIPAELEWIELEWI YAANI KUNA MATUKIO YA AJABU AJABU NA MARA NYINGI
YANATOKEA UKIWA HAUPO KWAHIYO MIMI SITAWEZA TENA KUKAA HAPA KWAKO KAMA WEWE
HAUPO".
JAMAA AKAMUULIZA KUNA
SHIDA GANI?. YULE DADA ALIANZA KUMSIMULIA BAADHI YA MATUKIO YANAYOTOKEA PALE
NYUMBANI.
AKASEMA " UNAJUA
KUANZIA SIKU YA KWANZA NAFIKA HAPA KWAKO NA KUKUTA JINSI ULIVYOKUWA UMETANDIKA
KITANDA CHAKO KWELI NILIVUTIWA SANA MAANA KILIKUWA KIMEPENDEZA SANA, KWAHIYO
SIKU ZOTE NIMEKUWA NIKIKUAMINIA JINSI UNAVYOTANDIKA KITANDA LAKINI ILIFIKIA
WAKATI BAADA YA KUKUZOEA NA TUNAPOKUWA PAMOJA TUKITOKA KITANDANI UKITANDAKA NI
TOFAUTI SANA NA VILE AMBAVYO HUWA NAKIKUTA.
ANASEMA NIKAHISI KUWA
LABDA HUWA UNAFANYA BLABLA LAKINI BAADAE NILIKUJA KUGUNDUA HATA SUALA LA
KUTANDIKA KITANDA WEWE NI MZITO SANA".
ALIENDELEA KUMWAMBIA JAMA KUWA SIKU
MOJA ALIFIKA PALE NA KUMKUTA JAMAA AKIWA BADO AMELALA NA BAADA YA MUDA JAMAA
ALIAMKA NA KUMUAGA MPENZI WAKE KUWA YEYE ANAKWENDA AMBAPO DADA HUYU ANASEMA
ANAKUMBUKA KABISA JAMAA ALIAMKA KITANDANI AKAJIANDAA NA KUONDOKA.
HUYU DADA AKIWA PALE
NYUMBANI ALIANZA KUFANYA SHUGHULI NYINGINE AMBAPO ALITOA VYOMBO NJE ILI AVIOSHE NA KISHA NDIO AANZE USAFI WA NDANI.
ALIPOMALIZA KUOSHA VYOMBO NA KUINGIA NDANI ALIKUTA KITANDA KIMETANDIKWA TENA
VIZURI SANA.
HUYU DADA ALISHTUKA KIDOGO LAKINI BAADAE AKAWAZA LABDA JAMAA KABLA YA KUONDOKA
ALITANDIKA, BASI TUKIO HILI NALO LIKAPITA
SIKU NYINGINE HUYU DADA
ALIKUWA PALE NYUMBANI AKIMSAIDIA JAMAA SHUGHULI ZA USAFI NA KUMUANDALIA MSOSI
WAKATI HUO JAMAA ALIKUWA AMEENDA KAZINI NA KAMA UNAVYOJUA WANAWAKE, YAANI
WANAFANYA KAZI NYINGI KWA WAKATI MMOJA.
SASA DADA HUYU ALIKUWA AMEINJIKA MBOGA
JIKONI KISHA AKAENDA NJE KUFUA LAKINI AKAWA AMEPITIWA BAADAE ALIKURUPUKA KWENDA
NDANI KUITOA MBOGA JIKONI AMBAPO ALIJUA MOJA KWA MOJA ITAKUWA IMEUNGUA VYA
KUTOSHA.
LAKINI CHA AJABU
ALIPOFIKA JIKONI ALIKUTA MBOGA AMEEPULIWA NA JIKO LIMEZIMWA.
TUKIO HILI LILIMSHTUA
SANA HUYU DADA AKAANZA KUWAZA ALIINGIA
KUEPUA KASAU, LAKINI KILA ANAPOJIULIZA ANAONA SIO KAMA UNAVYOJUA MAWAZO YAKIWA
MBALI HUWEZI UKAPATA MSHTUKO HUU MAPEMA BASI SIKU HIYO NAYO IKAPITA.
LAKINI KESHO YAKE TENA
HUYU DADA ALIKUWA AMEBAKI PALE HOME.
WAKATI MMOJA AKIWA SEBULENI MEZANI
KULIKUWA NA BIRIKA LA MAJI YA KUNYWA BASI ALIENDA AKACHUKUA KIKOMBE ILI ANYWE MAJI
LAKINI WAKATI ANAMIMINA
MAJI KWENYE KIKOMBE ASEMA KIASI ALICHOKUWA ANAMIMINA SI SAWA NA MAJI YALIYOKUWA
YANAINGIA KWENYE KIKOMBE.
ANASEMA MAJI YALITOKA
KAMA YANAMWAGWA YAANI KIKOMBE KIKAJAA NA MAJI KIBAO YAKAMWAGIKA. HAPO NDO
ALIJUA MAMBO HAYAENDI SAWA.
BASI KIMYA KIMYA ALIAMKA
AKARUDISHIA MLANGO AKASEPA YAANI HATA MAJI HAKUNYWA WALA HAKUFUTA YALE YALIYOMWAGIKA.
KWA MATUKIO HAYA BASI
ALIFIKIA UAMUZI WA KUMWAMBIA JAMAA “YAANI HAPA HUNIACHI TENA UKIONDOKA TU
KWENDA KAZINI NA MIMI NASEPA”
JAMAA ANASEMA WALIPIGA
STORI NYINGI SANA AMBAPO ILIBIDI AMSIMULIE KILA KITU KINACHOENDELEA KATIKA
MAISHA YAKE KUANZIA MAMBO YALIVYOANZA NA AKAMWAMBIA KUWA MWANZONI ALITAKA
KUMUELEZA LAKINI AKAHISI ATAOGOPA NA ATASHINDWA KUKAA KARIBU NA JAMAA.
LAKINI
TOFAUTI JAMAA ALIVYOMDHANIA, HUYU DADA
ALIHUZUNIKA SANA
HATA MACHOZI YAKAWA YANAMTOKA TU BILA KIKOMO.
ENDELEA KUFUATILIA KISA CHA FABBY KWENYUE JICHO LA MDADISI.BLOGSPOT.COM
KILA JUMANNE NA IJUMAA
0 comments:
Post a Comment