NA MWANDISHI WETU,
TARIME:
WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA WILAYANI TARIME WATAKIWA KUBORESHA KILIMO CHA ZAO KWA KUFUATA KANUNI ZA KILIMO BORA WALIZOFUNDISHWA KWA LENGO LA KUZALISHA KAHAWA YENYE TIJA IKIWA NI PAMOJA NA KUONDOKANA UMASIKINI WA KIPATO.
KAULI HIYO ILITOLEWA HIVI KARIBUNI NA MENEJA WA TAASISI YA UTAFITI WA KAHAWA TANZANIA TACRI BI: SHEIRA MDEMU KATIKA SEMINA YA MAFUNZO JUU YA UTUMIAJI WA SITAKABADHI GHALANI KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI NA USHIRIKA.
AIDHA AMESEMA WANAZALISHA MICHE CHOTARA ISIYOSHAMBULIWA NA MAGONJWA KWA LENGO LA KUPUNGUZA GHALAMA ZA UTUMIAJI WA DAWA UKU AKIDAI ASILIMIA KUBWA WAKULIMA HAWATUMIA DAWA KATIKA MASHAMBA YAO KWA LENGO LA KUUA WADUDU WAHARIBIFU KWANI WADUDU HAO UHARIBU UBORA WA KAHAWA HIZO.
KWA UPANDE WAKE AFISA KILIMO, USHIRIKA NA UMWAGILIAJI BW SILIVANUS GWIBOHA AMEWATAKA VIONGOZI KUWA NA SHAMBA LA MFANO KWA LENGO LA KUMSHAWISHI MKULIMA WA KAWAIDA.
KWA HATUA NYINGINE GWIBOHA AMEKEMEA VIKALI BAADHI YA TABIA ZA WAKULIMA KUUZA KAHAWA KWA KUTUMIA VIPIMO VISIVYO RASMI KISHERIA JAMBO AMBALO AMESEMA KUWA MNUNUZI ANAKUWA ANAMNYONYA MKULIMA AMBAPO AMEWATAKA WOTE WENYE TABIA KAMA HIYO KUACHA MARA MOJA.
HATA HIVYO GWIBOHA AMETOA WITO KWA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA KUTHAMINI ZAO ILI WAWEZE KUONDOKANA NA CHANGAMOTO ZA GHARAMA ZA MAISHA IKIWA NI PAMOJA NA KUONGEZA USHINDANI KWA WAFANYABIASHA WA ZAO HILO
HATA HIVYO SEMINA HIYO IMEANDALIWA NA BENK YA NMB TAWI LA TARIME NA KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA GOLDLAND HOTEL ILIYOPO WILAYANI TARIME MKOANI MARA.
Home »
» WAKULIMA WA KAHAWA WILAYANI TARIME WATAKIWA KUBORESHA KILIMO CHA ZAO KWA KUFUATA KANUNI ZA KILIMO BORA.
0 comments:
Post a Comment