BUTIAMA:
KUFUATIA KUWAPO KWA MATUKIO YA MAUAJI NA YA
KIKATILI AMBAYO YANAYOWALENGA ZAIDI WANAWAKE KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI,
WILAYANI BUTIAMA MKOANI MARA, MKUU WA JESH
I LA POLISI NCHI IGP ERENEST MANGU
AMETUMA TIMU YA WATALAAM MKOANI HAPA KWA AJILI YA KUCHUNGUZA KIINI CHA MAUAJI
HAYO. MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI, IGP ERNEST MANGU AMETUMA TIMU MAALUM YA WATAALAMU ITAKAYOONGOZWA NA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI NCHINI, DCI ISSAYA MNGULU ILI KUONGEZA NGUVU KWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAM WALIOPO MKOANI HAPA, ILI KUHAKIKISHA WOTE WANAOJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
AIDHA JESHI LA POLISI LIMETOA SHUKURANI KWA WANANCHI WANAOENDELEA KUTOA USHIRIKIANO UTAKAOSAIDIA WATUHUMIWA HAO KUENDELEA KUKAMATWA NA LINATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MARA NA MAENEO YA JIRANI KUWA WATULIVU WAKATI UPELELEZI UKIENDELEA.
AIDHA, JESHI LA POLISI NCHINI LIMEENDELEA KUWAOMBA WANANCHI WENYE TAARIFA ZA WAHALIFU HAO KUTOA TAARIFA HIZO KUPITIA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAYO; 0715 009930, 0754 785557 NA KATIKA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI ILI WAHUSIKA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
MWISHO.....
0 comments:
Post a Comment