Je, umewahi kufikiri kitu kama hiki katika maisha yako? Kila mtu ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia wewe tu, kila mtu hakutendei haki, mmhh kila mtu anakasoro.
Na je wewe ndivyo unaishi hivi? Mara ooh ebana mimi wananichukia mara oohh mimi hawanitendei haki, mbona mim wananitenga? Kama haya ndo maisha yako ua pengine unaishi na mtu mwenye hali kama hii lazima utambue kuwa unaishi na mtu mwenye matatizo makubwa sana.
Maana kutokana na uumbaji wamwenyezi Mungu ni dhahiri kuwa siyo rahisi watu kufanana, yaani kwa maana kuwa haiwezekani watu wote wakawa na mtazamo au mawazo yanayofanana kwamba akikuchukia huyu lazima na mwingine akuchukie au pengine asipokupenda huyu lazima na mwingine apoteze upendo juu yako,
Na pia kwanini wote wawe na tabia ya aina moja ya kuweza kukuchukia.?
Kwa maana hiyo ni dhahiri kuwa siku zote mlalamikaji wa namna hiyo lazima atakuwa na matatizo ambalimbali kama ya kisaikolojia, ufikirishaji akili na mengine kadha wa kadha kama wanavyobainisha wataalamu wa mambo ya asili ya uumbaji wa mwanadamu pamoja na wataalamu wa mambo ya saikolojia.
Aidha, kwa kuwa watu hawalingani kimwenendo, kimawazo na kitabia na niwazi kuwa ukiona watu wote hao wanakuchukia basi ujue kuwa tatizo halilo kwao kwa sababu hawawezi kuwa na mkabala wa aina moja, na hii itaonekana kuwa wewe ndo hujipendi na kutojipenda kwako kunaonekana kwa watu hao .
Kadhalika tunaposhindwa kujipenda sisi wenyewe basii hasira dhidi yetu huzitolea kwa watu wengine wanaotuzunguka, basi kama unahisi kuwa kunawatu wanakuchukia huo utakuwa siyo mtazamo wa kweli na ningependa uondoe wazo hilo kwa maana huwezi kuchukiwa na watu wote, na kama tatizo siyo wao basi tatizo ni wewe na watu hao ni kioo cha tabia yako.
Kama kila unapopita iwe nyumbani, au kazini na umeacha watu wengi wanakuchukia kadhalika umehama mtaani huku wakisema “mmhh bora ameondoka” basi ujue wewe ndiye mwenye kasolo, kwani haiwezekani watu wakae kikao cha kukuchukia, vinginevyo watu wanaweza kukerwa na tabia au vitendo vyako hadi inaonekana kuwa wanakula njama za kuweza kukuchukia kwa tabia zako ambazo tayari zishatengeneza chuki na kutopendwa na watu hao, na hapo ndipo utasikia sauti za maneno kama haya zikisikika, “ aaah we humjui huyo, ndivyo alivyo” na maneno mengine zaidi yenye kudhihaki.
Ni vyema tukatambua kwamba kila mtu anapenda kuonwa akipendwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa ingawa vinaweza visiwe vitu vya muhimu sana kwake, na unashindwa kumfanyi hivyo anaingia mahali ambapo anaona kuwa huenda kuwa karibu na wewe ni hatari au haipendezi.
Naomba nikwambie ukweli kuwa usithubutu kusema kuwa mtu au kikundi cha watu Fulani wanakuchukia, kwa kuona hivyo wataalamu wanaojua tabia za binadamu watajua kuwa wewe ndiye mkorofi sana kuliko unavyodhani.
Ukiona mtu anathubutu kusema wanafunzi wenzake, wafanyakazi wenzake, majirani zake, ndugu zake, wanae, wazazi wake au kikundi chochote cha watu Fulani kuwa wanamchukia kwa kiasi kikubwa basi mtu huyo ndiye mkorofi.
Tafadhali kama imetokea hivyo kwamba watu wanakuchukia au hawakupendi inabidi uanze kujiuluza wewe kama wewe bila kujipendelea kuwa chanzo cha chuki hizo, kadhalika ukiwa na upendo ndani ya moyo wako ile taswira itakuwa inaonekana kwa watu na utahisi kupendwa na kila mtu wala huta hangaika kusema Fulani ananichukia.
Na kila mtu mwenye kusema hivyo basi mwenyewe anatatizo au pengine hajipendi furahia maisha uliyonayo na hata kama unadharauliwa, lakini kumbuka msamaha si lazma isipokuwa ni muhimu!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Imeandaliwa na mwandishi wa blog ya jicho la mdadisi........ Bosco Robert.
Home »
» KUJITAMBUA, HESHIMA NA BUSARA NDIYO SABABU YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO......NI KATIKA TAFAKARI YA WIKI www.jicholamdadisi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment