SIKU MOJA BAADA YA KUSUSIA
VIKAO VYA BUNGE MAALUMU LA KATIBA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI BUNGENI
(UKAWA) UMETANGAZA RASMI KUWA UNAKWENDA KWA WANANCHI KUWASHITAKI WAJUMBE WA
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KUHUSIANA NA KILE KINACHOENDELEA BUNGENI IKIWA NI
PAMOJA NA KUUELEZA UMMA MSIMAMO WAO DHIDI YA BUNGE HILO.
WAZEE WA UKAWA WAKIJADILIANA JAMBO.
UMOJA HUO UMEDAI KUWA BUNGE
HILO LIMEKUWA LIKIPUUZA KILA KILICHOPENDEKEZWA NA WATANZANIA KUPITIA TUME YA
KATIBA ILIYOUNDWA NA JAJI WARIOBA.
WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA HAPO JANA WAMESEMA KUWA KAMWE HATOHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE HILO MPAKA PALE RASIMU YA KATIBA YENYE MAONI YA WANANCHI ITAKAPOKUBALIWA NA KUANZA KUJADILIWA BUNGENI.
WAKATI HUO HUO VIONGOZI WA UKAWA WAMEGOMEA MIKUTANO YA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUMU LA KATIBA LILILOPO CHINI YA MWENYEKITI WAKE NI SAMUEL SITTA AMBAYE ALIITISHA MKUTANO HUO ULIOKUWA NA LENGO LA KUSAKA MARIDHIANO.
NAYE MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF PROFESA IBRAHIMU LIPUMBA AMESEMA KUWA WAPO TAYARI KUACHANA MKUTANO HUO ENDAPO WAJUMBE WALIO WENGI WATAENDELEA KUDHARAU RASIMU YENYE MAONI YA WANANCHI, AMBAYO KISHERIA NDIYO INAYOTAKIWA KUJADILIWA KATIKA BUNGE HILO NA SI VINGINEVYO.
MNAMO APRIL 16 UMOJA HUO
UNAUNDWA NA JUMLA YA WAJUMBE 190 WALITOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE NA KUTANGAZA
KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE HILO VINAVYOENDELEA
MJINI DODOMA.
MWISHO........
0 comments:
Post a Comment