`

Home » » MKASA WA FABBY SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA USOME.

MKASA WA FABBY SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA USOME.



MKASA WA FABBY SEHEMU YA KWANZA.

FABIANI AU MAARUFU KAMA FABBY NI MKAZI NA MZALIWA WA MKOANI MTWARA KATIKA MAISHA YAKE YOTE TANGU ANAZALIWA HADI MAISHA YAKE YA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI HAKUWAHI KUKUTANA NA JAMBO LOLOTE AMBALO LINGETATANISHA NA KUOGOFYA KATIKA MAISHA YAKE, BALI YOTE HAYO YALIMTOKEA MIAKA KADHAA BAADA YA KUHITIMU KIDATO CHA NNE.

AKIWA NYUMBANI KWA KIPINDI CHOTE HICHO CHA MIAKA 13 TANGU ALIPOHITIMU ELIMU YAKE YA KIDATO CHA NNE  MAISHA YAKE YALIANZA KUWA YA WASI WASI NA KUMUWEKA KATIKA HALI YA SINTOFAHAMU NA HOFU TELE NA HII NI PALE ALIPOANZA KUTOKEWA NA VIUMBE WAWILI WA AJABU LICHA YA UZURI USIO KIFANI MACHONI MWAKE KWA ILIKUWA NI MARA YAKE YA KWANZA KUONANA NA WANAWAKE HAO AMBAOP ILIKUWA NI NADRA SANA KUZOELEKA.


NA HAPA SASA NDIPO PICHA LENYEWE LINAVYOANZA… NA ILIKUWA HIVIIIIIIIIIIIIII……….

SIKU MOJA AKIWA ANACHIMBA JALALA YEYE NA WENZAKE HUKU WAKATI HUO IKIWA NI ZAMU YAKE KUCHIMBA HUKU AKIWA NDANI YA SHIMO HILO GHAFLA JEMBE LAKE LIGONGA JIWE AMBALO KATIKA HALI YA KUSTAAJABISHA JIWE LILE LILIANZA KUTOA DAMU AMBAPO HAIKUCHUKUA MUDA MREFU AKIWA NDANI YA SHIMO HILO ULITOKEA MWANGA MKALI SANA HALI ILIYOPELEKEA KUANGUKA NA KISHA KUPOTEZA FAHAMU HALI ILIYOPELEKEA WENZAKE KUANZA KUJIULIZA KUNANINI NDANI YA SHIMO ALILOKUWAPO MWENZANO KWANI WALISHANGAA BAADA YA KUTOSIKIA MSHINDO WA UCHIMBAJI WA SHIMO HILO NDIPO WALIPOCHUNGULIA WALIMUONA MWENZAO AKIWA AMEANGUKA NA NDIPO WALIPOMCHUKUA NA KISHA KUMPELEKA CHUMBANI KWAKE.

FABBY AKIWA USINGIZINI  GHAFLA AKASHTUSHWA NA MWANGA MKALI AMBAPO KWA WAKATI HUO ALIKUWA AMEZUNGUKWA NA BAADHI YA NDUGU MARAFIKI PAMOJA NA MAMA YAKE MZAZI WALIOKUWA WAKIULIZANA JUU YA KILICHOMSIBA MARA GHFALA AKIWA ANAUTAZAMA MWANGA ULE UNATOKEA WAPI ILI HALI WATU WALIKUWA NDANI YA CHUMBA CHAKE WAKI HAWAUONI FABBY ALIMUONA KIUMBE AU BINTI AKIWA AMEVAA MAVAZI MITHILI YA MASISTA WA KIDINI NA MKONONI AKIWA AMEBEBA KITABU (BIBLE) KIKIWA NA MAANDISHI AMBAYO HAKUWEZA KUTAMBUA NI LUGHA ILIYOTUMIKA KATIKA MAANDISHI YALE.

WAKATI ANAMUANGALIA YULE KIUMBE ALISOGEA MPAKA PALE KITANDANI NA KISHA KUNYOOSHA MKONO NA KUMSHIKA FABBY KATIKA PAJI LA USO NA KUANZA KUMUOMBEA  LAKINI CHA AJABU NI LUGHA ALIYOKUWA AKIITUMIA YULE KIUMBE  ALIYEVALIA MAVAZI YA KISISTA AMBAPO FABBY ANASEMA HAKUIELEWA LUGHA HIYO LICHA YA KUMSIKIA JINSI ALIVYOKUWA BUSY KATIKA MAOMBI.

KIJANA FABBY ANASEMA MAOMBI HAYO YALIKUWA NI YA MUDA MFUPI SANA NA SISTA HUYO ALIPOMALIZA MAOMBI HAYO ALIMWITA KWA JINA LAKE " FABI AMKA". NA KISHA YULE KIUMBE AKATOWEKA VILE VILE HUKU AKISIDIKIZWA NA MWANGA UPANDE WA MLANGONI NA KUTOWEKA NA PAPO HAPO FABBY ALIJIKUTA AKIINUKA KWA MSHTUKO MITHILI YA MTU ALIYESIKIA MLIPUKO WA BOMU NA GHAFLA AKAROPOKA KWA SAUTI MOJA TU "WAAAAAAAAAAAAAA"

BAADA MSHTUKO WA GHAFLA  ALISHANGAZWA BAADA YA KUONA WATU WAMEMZUNGUKA HUKU WAKIMSHANGAA.

NA IKUMBUKWE KUWA TANGU ALIPOTOLEWA JALALANI ALIKUWA HAJAPATA FAHAMU KIASI KWAMBA BAADHI YA WANANDUGU KUANZA KUHISI KUWA HUIENDA NDUGU YAO ALIKUWA ANAKATA ROHO NA KWA JINSI WALIVYOMUONA AKIAMKA KWA YOWE WATU WOTE WALISTUKA KWA KIASI KIKUBWA.

BAADA YA FAHAMU KUMRUDIA FABBY ALIWAULIZA WATU WALIOKUWA WAMEMZINGIRA KUWA “ETII JAMANI HUYO DADA ANATOKA WAPI"? LAKINI HAKUWEZA KUPATA JIBU NA BADALA YAKE ALIWAONA WATU WALIOKUWA WAMEMZINGIRA WAKIMSHANGAA, LAKINI HAKUISHIA HAPO ALIWAULIZA TENA JAMANI MBONA KIMYA? INAMAANA HAMJAMUONA HUYO DADA?.

LAKINI MAJIBU YA SWALI LAKE YALIENDELEA KUWA KIMYA NA WALA HAKUPATA JIBU TOFAUTI NA KUONA WATU WANAZIDI KUMSHANGAA, BAADA YA MASWALI HAYO YENYE UTATA YALIYOKOSA MAJIBU MAMA YAKE ALIANZA KULIA AKIJUA KUWA MWANAE TAYARI AMESHACHANGANYIKIWA NA HII NI KUTOKANA NA MAZINGIRA YAKE BAADA YA KUANGUKA GHAFLA NA KUPOTEZA FAHAMU KWA MUDA MREFU NA BAADAE KUAMKA HUKU AKIROPOKA MANENO AMBAYO HAWAKUYAELEWA.

KWA JINSI FABBY ALIVYOENDELEA KUULIZA MASWALI YASIYO NA MAJIBU NDIPO HAPO ALIPOGUNDUA KUWA HATA HAO NDUGU ZAKE HAWAKUMUONA NA KUSEMA KIMOYO MOYO HUENDA YEYE NDIYE MTU PEKEE ALIYEMUONA HUYO DADA.

BASI BAADA YA KUPUMZIKA KWA KIPINDI KIREFU HUKU NDUGUZE WAKIJIULIZA JUU YA MSWALI YA FABBY JUU YA KILICHOTOKEA NDIPO FABBY ALIPOANZA KUWASIMULIA KILA KITU ALICHOKIONA KUANZIA KULE KATIKA UCHIMBAJI WA JALALA LA TAKA MPAKA TUKIO LA KUJA KWA YULE DADA ALIYEVALIA VAZI LA KISISTA NA KISHA KUMFANYIA MAOMBI NDANI MWAKE HALI YAKUWA WENZAKE WALIKUWA HAWAMUONI.

BAADA YA KUSIKIA HIVYO NDUGU HAO WALIBIDI WAENDE KUANGALIA MLE JALALANI LAKINI HAWAKUONA CHOCHOTE BASI WAKAWA WAMEACHANA NA MAONGEZI HAYO NA KUENDELEA NA HABARI NYINGINEZO, KAMA UJUAVYO “MTOTO KWA MAMA HAKUI NA UCHUNGU WA MAMA AUJUAE MZAZI” LAKINI KWA MAMA YAKE LAKINI WASI WASI ULIENDELEA KUKISUMBUA KICHWA CHAKE NA KUENDELEA KUMTIA WASI WASI BI. MKUBWA HUYO HALI ILIYOPELEKEA MAMA YAKE KUTOMRUHUSU MWANAE JAMAA KUTOKA NYUMBANI KWAO ILI YASIJE YAKATOKEA MENGINEYO ILIHALI HAYUPO NA MAMA YAKE AU AKIWA MBALI NA NYUMBANI KWAO.

ZIKIWA ZIMEPITA SIKU MBILI TANGU TUKIO LA KUANGUKA JALALANI  HUKU AKIFUATA NMAAGIZO YA MAMA YAKE YA KUTOTOKA NYUMBANI.

SIKU MOJA AKIWA NYUMBANI PAMOJA NA MARAFIKI ZAKE WALIOKUWA AKICHIMBA NAO SHIMO LA TAKA SIKU ILE YA TUKIO GHAFLA ALIONA NDEGE MMOJA AITWAYE "TUMBUSI" ANASEMA HANA UHAKIKA JUU YA JINA HALISI LA NDEGE HUYO LAKINI UKWELI NI KWAMBA JINA HILO MIMI NDIYE NIMEMPATIA NDEGE HUYO KWANI NILIKUWA NIKIMFAFANANISHA NA MWEWE” NASEMA FABBY…...

YULE NDEGE ALIWAPITA PALE WALIPOKUWA WAMEKAA NA ALIPITA KATIKA MAZINGIRA AMBAYO SI YA KAWAIDA KIASI KWAMBA LAZIMA MTU UPATE WASI WASI TU KWA NAMNA ALIVYOPITA NA KWAKUWA NDUGU HUYO HUWA NA  ASILI YA UOGA LAKINI CHA AJABU ALIPITA KARIBU NAO KISHA AKAWA AKAZUNGUKA NYUMA YA NYUMBA.

FABBY ALIWAULIZA RAFIKI ZAKE " VIPI MMEMUONA HUYO NDEGE?" LAKINI CHA AJABU RAFIKI ZAKE WAKASHANGAA HILO SWALI WAKAMWAMBIA HAKUNA NDEGE ALIYEPITA, FABI ANASEMA KWA JINSI ALIVYOKUWA AKIONGEA NAO NA MARAFIKI ZAKE KUONEKANA KUKATAA JUU YA KUMUONA NDEGE HUYO AIKAMLAZIMU KUZUNGUKA NYUMA YA NYUMBA ALIPOELEKEA NDEGE ILI AJIHAKIKISHIE LAKINI ALIPOZUNGUKA HAKUMUONA NDEGE HUYO NA HATA ALIPOJITAHIDI KUTAZAMA HUKU NA KULE LAKINI HAKUWEZA KUMUONA KISHA AKARUDI KUKAA PALE ALIPOKUWA NA RAFIKI ZAKE NA ALIPOKAA TU GHAFLA AKAMUONA YULE NDEGE TENA AMBAPO SAFARI HII SASA ALIFIKA MPAKA MPAKA WALIPOKAA NA KUTUA KATIKA MTI ULIOKUWA KARIBU NAO.

FABBY KAMA KAWAIDA YAKE AKAWAULIZA TENA RAFIKI ZAKE “JAMANI EEEH”  YULE NDEGE NINAYEWAAMBIA SI HUYU HAPA? HUKU AKIWAONESHA KWA KIDOLE LAKINI KILA ALIPOKUWA AKIWAONESHA WAKAWA WANAMWAMBIA KUWA HAWAONI KITU CHOCHOTE NA BAADAYE WAKAMBEZA KABISA WAKAENDELEA NA STORI ZINGINE HUKU WAKIMUACHA FABBY AKIWA AMEKODOLEA MACHO JUU YA MTI HUO.

FABBY ALIJIKUTA AKIMUANGALIA YULE NDEGE HUKU NDEGE HUYO NAYE AKIMKODOLEA MACHO FABBY
NA IKAWA NI FULL KUANGALIANA HUKU NDEGE AKIWA HATIKISHI KICHWA WALA JICHO KWA TAKRIBANI DAKIKA TANO HIVI NA GHAFLA YULE NDEGE ALIPOKUWA AMEKAA KILITOKEA KITABU KIKUBWA SANA KIMERUSHWA KANA KWAMBA KULIKUWA NA MTU ALIYEKIRUSHA KUELEKEA UPANDE ALIOKUWA AMEKAA FABBY.

CHA AJABU BADALA YA FABI KUSHTUKA NDO AKAJIKUTA KAZUBAA ZAIDI KWA JINSI KILE KITABU KILIVYOONEKANA KWA JINSI KILIVYOKUWA KIKISOGEA KIKAWA KINAZIDI KUONGEZEKA UKUBWA ZAIDI, KITABU KILE KILIENDELEA KUSOGEA KIKIWA KINAFUNUKA FUNUKA KARATASI KAMA UNAVYOJUA KITABU KITAKAPORUSHWA ANGANI NI MITHILI YA NDEGE ANAVYORUSHA MBAWA ZAKE WAKATI WA KURUKA AU KUTUA.

KILA KITABU HICHO KILIVYOKUWA KIKIFUNUKA KILIKUWA KIKIONESHA PICHA MBALIMBALI KAMA SINEMA NA KIKAFIKIA WAKATI KIKAWA KINAONEKANA KURASA ZOTE MBILI KATIKATI HUKU KATIKA KURASA HIZO AMBAZO ZILIONEKANA KATIKA KURASA MBALI MBALI NA KATIKA UKURASA WA KUSHOTO WALIONEKANA WATU WENGI SANA WAKIWA MSIBANI WANALIA KATIKA MJI ALIOUFAHAMU HUKU MIONGONI MWA WATU HAO WALIOKUWA WAKILIA ALIKUWA AKIWAFAHAMU NA UPANDE WA PILI ALIMUONA MWANAMKE MMOJA AKIWA KAJITANDA KHANGA AKIWA ANATEMBEA HUKU ANALIA SANA NA ALIPOMTAZAMA VIZURI ALIMGUNDUA KUWA NI MKE WA MJOMBA WAKE” WENGINE WANAMUITA SHANGAZI NA KULE KWETU SISI TUNAITA MKAZA MJOMBA.

HUKU AKIWA BADO ANAENDELEA KUKIDURUSU KITABU KILE KWA HALI YA MSHANGAO HUKU WENZAKE NAO WAKIWA WANAMSHANGAA KWAKUWA WALIMUONA KAWA KAMA SANAMU KWA JINSI ALIVYOKUWA AMEGANDA NA WALA  HATIKISIKI WALA KOPE HAZICHEZI GHAFLA KILE KITABU KIKAJIFUNGA NA KISHA KIKATOWEKA MACHONI MWAKE.

FABBY BAADA YA KUONA HAYO ALIKURUPUKA TENA KWA SAUTI YA JUU HUKU AKIITA “MAMA MAMA MAMA” HADI JIKONI KWA MAMA YAKE AMBAYE ALIKUWA ANAPIKA, NA ALIPOFIKA TU AKAMWAMBIA MAMA YAKE MAMA MJOMBA AMEKUFA".

BAADA YA KUSIKIA KAULI ILE TOKA KWA MWANAE MAMA ALISHTUKA KWA MSHANGAO NA AKILI ZIKAMJIA KUWA NI SASA MWANAE NI WAZI ATAKUWA AMECHEZEWA AKILI, AKAMWAMBIA, "HIVI WEWE MUDA WOTE ULIKUWA HAPO UMEJUAJE MJOMBA WAKO AMEFARIKI?" KATIKA HALI YA KUROPOKA FABBY ALIJIKUTA AKIMJIBU MAMA YAKE KUWA  SHANGAZI YUKO NJIANI ANAKUJA HUKU LAKINI KABLA HAJAMALIZA TU KUMUELEZEA IKASIKIKA SAUTI YA MWANAMKE KWA MBALI IKILIA SAUTI AMBAYO HATA MAMA YAKE ALIWEZA KUITAMBUA KUWA NI SAUTI YA WIFI YAKE, YAANI HAPO HAPO MAMA YAKE NAYE AKAANGUA KILIO "JAMANI KAKA YANGUUU...."

BASI BAADA YA TAARIFA HIZO ZA MSIBA WAKAANZA KUJADILI NAMNA YA KWENDA MSIBANI AMBAPO SUALA KUBWA LILIKUWA NI NAULI NI WAPI WANAPATA NAULI.

KWA KIPINDI HICHO CHOTE FABBY AMABAYE SHUGHULI YAKE KUBWA ILIKUWA NI UUZAJI WA MITUMBA KATIKA MOJA YA MADUKA MJINI MTWARA NA WAKATI HUO MSIBA HUO UNATOKEA YEYE HAKUWA HATA NA KIASI CHOCHOTE CHA FEDHA IKAMLAZMU AANGALIA NAMNA YA KUWATAFUTIA WAZAZI NAULI NA NI WAPI ATAPATA FEDHA ALIAMUA KWENDA KUOGA ILI AKIMALIZA NDIPO AKAHANGAIKIE SUALA HILO LA FEDHA.


FABBY AMBAYE MARA ZOTE NI NADRA KUMKUTA AKIWA AMEKUNJA SURA KWA MWENDO WAKE WA UPOLE NA WENYE HAIBA ALICHOTA MAJI YAKE TARATIIBU NA KISHA KUBEBA NDOO YAKE NA KISHA KUELEKEA BAFUNI LAKINI KABLA HAJAINGIA BAFUNI ALISIKIA KUNA MTU ANAMGUSA BEGA LA KUSHOTO ALIPOGEUKA HAKUMUONA, ALIPOKUWA ANASHANGAA JUU YA HICHO KILICHOMGUSA BEGANI GHAFLA AKAHISI KAGUSWA TENA BEGA LAKE NA SAFARI HII NI BEGA LA KULIA NA ALIPOGEUKA TU AKASHTUKA SANA KWA ALICHOKIONA KWA ALICHOKIONA.

…....JE! NINI ALICHOKIONA NA JE! UNATAKA KUJUA NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO NA VIPI KUHUSU SAFARI YA MAZISHI NA MIPANGO YAKE YA KUTAFUTA FEDHA ILI AWAPATIE WAZAZI WAKE? BASI USIKOSE MWENDELEZO WA STORI HII YA KUSISIMUA NA KUHUZUNISHA KUHUSIANA NA MASIHA HAYO MAPYA YA KIJANA FABBY KUTOKA MKOANI MTWARA HAPA HAPA KATIKA BLOG HII HII YA JICHO LA MDADISI KILA IJUMAA USIKOSE SEHEMU YA PILI .

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK