`

Home » » WATAALAMU WA KILIMO NA MIFUGO WAPEWA SOMO.

WATAALAMU WA KILIMO NA MIFUGO WAPEWA SOMO.

NA MWANDISHI WETU,

TARIME.

WATAALAMU WA KILIMO NA MIFUGO MKOANI MARA WAMETAKIWA KUTOA TAKWIMU SAHIHI KUTOKA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI KWA LENGO LA KUBORESHA UFANISI WA KAZI.

KAULI HIYO IMETOLEWA NA AFISA KILIMO NA UMWAGILIAJI BW. SILVANUS GWIBOHA ALIPOKUWA AKIFUNGUA KIKAO CHA WATAALAMU HAO KWAKUSHIRIKIANA NA WATAALAMU KUTOKA HALMASHAURI MBILI IKIWEMO HALMASHAURI YA MJI WA TARIME KATIKA UKUMBI WA MRONI GARDEN HOTEL MJINI TARIME.


AFISA KILIMO HUYO AMETOA RAI HIYO BAADA YA BAADHI YA TAKWIMU KUJAZWA KINYUME NA TARATIBU SUALA AMBALO LIMEKUWA LIKIWAPA CHANGAMOTO KATIKA UTENDAJI WA KAZI HUKU AKITOA ONYO KWA BAADHI YA WATUMISHI WANAOTOKA KATIKA ENEO LA KAZI BILA KUTOA TAARIFA YEYOTE NI WAZI KUWA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

AIDHA AFISA HUYO AMEWATAKA WATALAAMU HAO KUHAKIKISHA WANASIMAMIA MIRADI MBALI MBALI ILIYOAINISHWA NA DASIP KATIKA MAENEO HUSIKA.

NAYE AFISA KILIMO WA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME BW. HASHIM BALONGO AMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA KUWAPATIA PEMBEJEO WAKULIMA ILI KUHAKIKISHA KILIMO KINABORESHWA WILAYANI HUMO IKIWA NI PAMOJA NA KUWATAKA WATAALAMU HAO KUTAMBUA MAMLAKA HUSIKA PAMOJA NA UWAJIBIKAJI WAO KATIKA KAZI KWA LENGO LA KUBORESHA MAHUSIANANO MEMA.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK