MUSOMA.
WANANCHI MKOANI MARA NA
MAENEO MENGINE YA JIRANI WAMEOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UFUNGUZI WA WIKI
YA MZIWA INAYOANZA LEO KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MKENDO ILIYOPO
MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA.
KWA MUJIBU WA TAARIFA
ILIYOTOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MARA IMESEMA KUWA SHEREHE HIZO ZA WIKI
YA MAZIWA MWAKA HUU ZINAANZA LEO TAREHE 29 MAY HADI JUNE MOSI AMBAPO MGENI
RASMI KATIKA UFUNGUZI WA WIKI YA MAZIWA NI MKUU WA MKOA WA MWANZA AMBAYE PIA
ANAKAIMU MKOA WA MARA BW. EVALIST NDIKIRO.
MBALI NA UFUNGUZI HUO HII LEO
PIA TAREHE 30 MWEZI MAY KUTAKUWA NA KONGAMANO LA KUMI LA TAIFA LA KUENDELEZA
TASNIA YA MAZIWA LITAKAYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MWEKEZAJI ULIOPO OFISI YA
MKUU WA MKOA WA MARA NA TAREHE 31 MAY KUTAKUWA NA MKUTANO WA BARAZA LA WADAU WA
MAZIWA LITAKALOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MWEKEZAJI OFISI YA MUU WA MKOA.
AIDHA TAARIFA HIYO IMEENDELEA
KUSEMA KUWA JUNE 1 MWAKA HUU NDIYO KUTAKUWA MWISHO WA MAADHIMISHO HAYO AMBAPO
MGENI RASMI ANATARIWA KUWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MH, DK. TITUS
KAMAN KATIKA SHSREHE HIZO ZITAKAZOFANYIKA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MKENDO ULIOKO
MANISPAA YA MUSOMA.
SHEREHE HIZO ZINAZOANZA LEO
NA KUMALIZIKA SIKU YA JUMAAPILI ZINALENGO
LA KUWASAIDIA WANANCHI MKOANI HAPA KUJIJENGEA TABIA YA KUNYWA MAZIWA IKIWA NI
PAMOJA NA KUTOA MWANYA KWA WAFUGAJI WA NGO’MBE WA MAZIWA KUJITANGAZA ILI KUINUA
KIPATO CHAO.
KATIKA MAADHIMISHO HAYO
VIKUNDI MBALI MBALI NA WASANII WA MUZIKI WANATARAJIA KUPAMBA SIKU HIYO MUHIMU
HUKU KAULI MBIU YA WIKI YA MAZIWA MWAKA HUU NI ‘‘FUGA NG’OMBE WA MAZIWA BORESHA KIPATO NA LISHE BADILIKA SASA’’
MFUGAJI AKIKAMUA MAZIWA
0 comments:
Post a Comment