kwa upande wangu hali sio poa sana. Naa kwa nafasi
hii naomba leo nikupe mwendelezo wa stori ya fabi kwa wale wanaofuatilia
mkasa huu
BAADA YA FABI KUWASHA TAA KWELI ALIMUONA YULE BINTI
AKIWA AMECHUCHUMAA NA BAADA YA MUDA AKASIMAMA HUKU AKIWA KAMA KABANWA
VICHEKO..NA MUDA WOTE HUU BABA YAKE JAMAA KAJIBANANISHA KWA KIJANA YAANI
YALE MAMBO ALIYOKUWA ANAYASIKIA KWA KIJANA WAKE AKAWA KAMA HAAMINI SASA
SIKU HIYO NDO IKAWA LIVE
YULE BINTI ALIYEKUWA KAMA AMEBANWA
SANA VICHEKO GHAFLA AKABADIRIKA NA KUONEKANA KAKASIRIKA SANA, KISHA
AKAMWANGALIA AKAMKAZIA MACHO BABA'KE FABI AKAONEKANA ANAKUJA KWA KASI
UPENDE ULE WA KITANDA KAMA KAWAIDA YAKE ANATEMBEA KWA HATUA TATU NA HII
NDO ISHARA YAKE YA KUTOWEKA. KWAHIYO ALIONEKANA HAPA KULE AKIWA
AMEKARIBIA KARIBU NA KITANDA..FABI ANASEMA HATA HAKUONA TENA
KILICHOENDELEA MAANA ALIFICHA SURA NA KUPIGA KELELE HUKU KICHWA KINATAKA
KUPOTELEA KWENYE MAGOTI.
ANASEMA ALIKAA KIMYA HUKU CHUMBA
CHOTE KILISIKIKA KIMYA SANA HAKUNA MOVEMENT YA KITU CHOCHOTE, WAKATI HUO
HUO BILA KUFUNUA KICHWA ALINYOOSHA MKONO KUPAPASA SEHEMU ALIYOKUWA
AMELALA BABA'KE AKAMGUSA. LAKINI AKASHTUKU MZEE YUKO KIMYA, FABI AKAITA "
BABA"..... MZEE KWA MBALI AKAITIKA "MMMMMM". FABI ANASEMA SAUTI HII
ILIMFARIJI KIDOGO MAANA ALIPATA WASI WASI KWAMBA LABDA BABA YAKE KASEPA.
BAADA YA MUDA FABI ALIFUNGUA MACHO NA KUANZA KUANGAZA ANGAZA CHUMBANI
LAKINI HAKUONA KITU NDIPO ALIGUNDUA YULE KIUMBE KATOKA. ALIMUAMSHA BABA
YAKE NA KUMWAMBIA HAKUNA KITU..NA WAKATI WOTE HUO MZEE ANATETEMEKA YAANI
IKAWA KAMA FABI NDO MZAZI NA BABA NDIYO MTOTO..MAANA MZEE ALIKUWA MPOLE
MPAKA BASI. ALIKAA KIMYA KWA MUDA NA WAKATI HUO HAKUNA ALIYELALA TENA
WALA ANAYEHISI USINGIZI YAANI WOTE WAMEKAA TU KITANDANI.
BAADAYE KIDOGO FABI ALIMUONA MZEE ANAAMKA KITANDANI AKAENDA AKACHUKUA
SHATI LAKE AKAVAA, BAADAE AKACHUKUA VIATU AKAVAA KISHA AKAMWAMBIA FABI
"MIMI NAENDA LAKINI ASUBUHI KUKICHA NAOMBA UJE NYUMBANI"..AKAAGA KISHA
AKAFUNGUA MLANGO AKATOKA NJE, FABI ANACHOSEMA ALISIKIA KISHINDO TU CHA
MZEE ANAVYOTOKA MBIO HUKO NJE.
FABI ALIAMKA AKAFUNGA MLANGO
KISHA AKAWA AMEJIEGESHA TU PALE KITANDANI MAANA HATA USINGIZI HAKUNA
TENA NA WAKATI HUO AKIWA ANAHISI MUDA WOWOTE YULE KIUMBE ATARUDI LAKINI
HAIKUTOKEA NA ILIPOFIKA ASUBUHI ALIENDE KWAO KAMA BABA'KE ALIVYOAGIZA.
ALIFIKA AKAWAKUTA WAZAZI WANAONGEA NA WALIKUWA WANAONGELEA MAMBO HAYO
HAYO YANAYOMHUSU JAMAA, ALIFIKA AKAJUMUIKA NAO KATIKA MAZUNGUMZO NA
WAKATI HUU SASA BABA NDO ALIONEKANA KUZINGATIA SANA MAANA AMESHUHUDIA
KWA MACHO YAKE MAANA MUDA MWINGI ALIPOKUWA ANAPATA HABARI ZA FABI NI
VITU AMBAVYO HAKUVIAMINI KATIKA MAISHA YAKE ALICHUKULIA KAMA STORY TU
AKAHISI LABDA JAMAA PENGINE AMEANZA KUVUTA BANGI SASA LABDA HIZO NI GIA
TU ZA KUTOKEA.FABI ANASEMA NI KWA MARA YA KWANZA ALIMUONA BABA'KE
ANAONGEA HUKU ANAMWANGALIA FABI KWA HURUMA HADI MACHOZI YANAMLENGA
LENGA.
KWELI WALIONGEA MENGI SANA NA KUTAFUTA UFUMBUZI NA
MIONGONI MWA MANENO YAO JAMAA APELEKWE KWA WAGANGA WA KIENYEJI MARA
MATAMBIKO YA UKOO WAO, YAANI MANENO MENGI TU YASIYO NA JIBU LA MOJA KWA
MOJA. BAADA YA MJADALA WA MUDA MREFU BAADAE WALIFIKIA HITIMISHO LA
MJADALA WAO WAKAENDELEA NA MAJUKUMU MENGINE AMBAPO SIKU HIYO FABI
ALILALA PALE NYUMBANI KWAO NA KESHO YAKE NA SIKU ILIYOFUATA ALIRUDI GETO
KWAKE.
ALIPOINGIA ROOM ALIKUTA CHUMBA KINANG'AA YAANI
KIMEPAMBWA MPAKA BASI, JAMAA ALIKITAZAMA BAADAYE AKATOKA NJE AKAWAAMBIA
WENZAKE ANAOISHI NAO HAPO. ANASEMA KWANZIA TUKIO HILO WALE WAPANGAJI
WAKAANZA KUMUITA " BABA AGNES MAUA". KWAHIYO LIKIFANYIKA JAMBO LOLOTE
LISILO LA KAWAIDA KATIKA ULE MJI UTASIKIA " HAYO NI MAMBO YA BABA AGNES
MAUA" HIVYO HIVYO MAISHA YANAENDA
FABI ANASEMA ALIKUWA
ANAMAZOEA YA KUFANYA MAZOEZI KILA ALFAJILI NA MIDA YA JIONI ANAPOTOKA
KAZINI. SIKU MOJA ALIAMKA ALFAJILI SANA KWA AJILI YA MAZOEZI IKIWA KAMA
SAA KUMI NA MOJA KASORO, AKIWA NJE AMECHUCHUMAA GHAFLA ALISIKIA KUNA
KITU KAMA DUARA LIMEMZUNGUKA LIKIWA LINANG'AA SANA YAANI LINATOA MWANGA
MKALI SANA.FABI ALISIMAMA KWA HOFU LAKINI KUMBUKA LILE DUARA LIMEMUWEKA
KATIKATI AMBAPO ANASEMA KATIKA DUARA LILE KULIJIGAWA MARA MBILI,
LILIANZA DUARA DOGO LIKIWA NI JEUSI SANA LIKIFUATIWA NA HILO DUARA
LINALONG'AA.
FABI ALIOGOPA LAKINI HAKUWEZA KUTOKA KATIKATI
MAANA JINSI LILE DUARA LILIVYO HATA ALISHINDWA KUJUA PENGINE LINAWEZA
KUMFANYA NINI KAMA AKILIKARIBIA...ANASEMA ALISIMAMA TAKRIBANI DK 10 BILA
KUFANYA CHOCHOTE LAKINI KADRI MUDA ULIVYOKUWA UNAENDA ILIONEKANA KAMA
MNG'AO WAKE UNAPUNGUA....AKIWA AMESIMAMA HIVYO HIVYO ALISIKIA KUNA WATU
WANAKUJA KUTOKA UPANDE MWINGINE WA NYUMBA YAO MAANA KULIKUWA NA NJIA
INAYOPITA HAPO KARIBU NA NYUMBA YAO.
KWA HIYO ALIANZA KUSIKIA
KWA MBALI WATU WANAKUJA HUKU WANAONGEA NA KWA JINSI ALIVYOSIKIA ZILIKUWA
NI SAUTI ZA WATOTO WA KIKE NA BAADHI YAO AKAWATAMBUA AMBAPO KWA HARAKA
ALIJUA WANATOKA DISCO. BAADA YA HAWA BINTI KUCHOMOZA KWENYE USAWA WA
NYUMBA PALE UWANJANI WALIPIGA YOWE WAKAKIMBIA KURUDI WALIKUTOKA HUKU
WANAPIGA KELELE. HAPO NDIPO FABI AKAJUA ANACHOKIONA SI YEYE PEKEE HATA
WENGINE WANAWEZA KUKIONA.
SASA KUTOKANA NA ZILE KELELE WATU
WENGINE WAKAAMKA NA KWA MUDA HUO FABI SASA ILIBIDI ACHUNGUZE HICHO
KINACHOTOA MWANGA NAMNA HIYO NI NINI, SO ALIBIDI ACHUCHUMAE CHINI ILI
ACHUNGUZE VIZURI. ALIPELEKE MKONO KATIKA LILE DUARA LINALING'AA KUONA NI
NINI, WAKATI HUO ANAFANYA KWA UWOGA MKUBWA YAANI ANAPOPELEKA MKONO
KISHA ANASITA MWISHO AKAJIKAKAMUA AKASEMA KAMA KUFA BASI ACHA
AFE..AKANYOOSHA MKONO AKAGUSA PALE KATIKA DUARA LAKINI CHA AJABU ALIONA
ANAGUSA MCHANGA WA KAWAIDA TU AKAJARIBU KUUNUSA AKASIKIA HARUFU KAMA
MCHANGA WA BAHARI
LAKINI KINGINE NI KWAMBA HATA VILE VIDOLE
VIKAWA KAMA VINANG'AA ALIJIFUTIA KWENYE BUKTA YAKE NAYO AKIWA KAMA
AMEIPAKA VITU VYA KUMETAMETA. KUMBE KIPINDI WALE MABINTI WANAKIMBIA HUKU
WANAPIGA YOWE KUFIKA BARABARANI WALIKUTANA WA VIJANA WENGINE KUULIZWA
KUNA NINI WAKAELEZA SASA IKABIDI WALE VIJANA NA WALINZI KATIBA MADUKA YA
HAPO JIRANI WAONGOZANE KUJA KUONA NINI KIMETOKEA
WALIKUJA
MPAKA PALE NAO KUFIKA TU KIDOGO WATOKE MBIO ILA KWA SABABU WALIKUWA
WENGI WAKAJIKAKAMUA. FABI AKAWAMBIA "MSIOGOPE NJOO TU". KUMBUKA KULIKUWA
NA MWANGA MKALI KWAHIYO ILIKUWA NI RAHISI KUMUONA NA KUMTAMBUA FABI.
YAANI KILA MTU AKAWA NA LAKE HAKUNA ALIYETAKA HATA KUSOGEA TOFAUTI NA
KUHAMAKI TU NA JINSI WANAVYOSHANGAA NDIVYO WATU WENGINE WALIVYOKUWA
WANAZIDI KUAMKA NA KUONGEZEKA. KWAHIYO WATU WALIJAA SANA KATIKA ULE MJI
LAKINI CHA AJABU NI KWAMBA KILA PALIVYOKUWA PANAENDELEA KUPAMBAZUKA
NDIPO MWANGA UNAFIFIA KWAHIYO ILIFIKIA HATUA MWANGA UKAWA WA KAWAIDA NA
ULE MCHANGA NDO UKAANZA KUONEKANA VIZURI.
KILA MTU ALIZUNGUMZA
YAKE KATIKA TUKIO HILI NA MWISHO YA SIKU LIKATOKA WAZO LA KUWAITA
USTADHI TOKA MSIKITI ULIOKUWA JIRANI NA BAADA YA KUJA NAYE ALIFIKA
AKAELEZA MAMBO MENGI HUKU KUBWA AKISEMA HAKUNA JAMBO BAYA NA HIYO
INAWEZA KUWA NI SEHEMU YA BARAKA. BAADA YA HAPO ALICHOTA ULE MCHANGA
KIDOGO NA KUWAAMBIA KAMA KUNA MTU ANAAMINI BASI ANAWEZA KUCHUKUA TU.
BAADHI YA WATU WAKAONA KUMBE NI DILI BASI WAKAUZOA WAKAENDA KUMWANGA
KATIKA VIWANJI MWAO YAANI KILA MTU KWA JINSI ALIVYOAMINI.
MIONGONI MWA WALIOUCHUKUA MCHANGA HUO NI PAMOJA NA MPANGAJI MMOJA WA
PALE NYUMBANI AMBAYE ALICHUKUA MCHANGA NA AKAENDA KUUWEKA KATIKA CHUMBA
FLANI CHA STOO KILICHOKIWA KINATUMIKA KWA KUWEKA MKAA. LAKINI BAADA YA
KUUWEKA KILE CHUMBA KILING'AA UTADHANI UMEWEKA BALBU 50, YAANI ULE
MCHANGA ULIKUWA UNAWAKA AJABU..HADI WAPANGAJI WENGINE WAKAPATA HOFU
WAKAMWAMBIA AUTOE NJE. BASI ALIENDA AKAUCHUKUA BAADAE AKAENDA AKAUWEKA
NJE
BASI BAADA YA MUDA WATU WAKAANZA KUSAMBAA MAJUMBANI MWAO,
AMBAPO FABI NAYE AKAINGIA CHUMBANI MWAKE ALKINI ALIPOKAA TU KITANDANI
KWAKE GHAFLA UKATOKEA MWANGA MKALI MLANGO KISHA AKAMUONA YULE KIUMBE
MWINGINE ANAYEVAA KAMA SISTER KAMA ANAHARAKA FLANI HIVI " AKAMWAMBIA
TOKA NJE HARAKA" KISHA YEYE AKATOWEKA.
FABI ANASEMA HATA BILA
KUKAWIA ALIAMKA KWA HARAKA KUTOKA NJE LAKINI KABLA YA KUUFIKIA MLANGO
ALISHTUKIA MLANGO UNAJIFUNGA KWA NGUVU SANA "BAAAAAAA" KISHA AKASIKIA
KICHEKO CHA MTOTO WA KIKE KIKITOKEA UPANDE WA KITANDANI ALIKUKUWA
AMEKAA....... NINI KINAENDELEA BASI USIKOSE MWENDELEZO WA STORI HII
Najua wengi wanauliza stori ni lini lakini hata mimi nashindwa
kukuhakikishia kwasababu ya majukumu mengine maana kuanzia jtatu hadi
jpili nina kipindi so sina siku ya kupumzika by then katika simulizi
nakuwa na-deal zaidi na mkasa ulio redioni.
So kwa mazingira hayo hadi
napopata muda ambao niko free walau niandike kadri navyoweza na
ukizingatia c mwandishi mzuri ila ilimradi ujumbe ufike so i will try my
best within this week niweze kupost mwendelezo huu
Home »
» MKASA WA FABB SEHEMU YA TATU SAMAHANI KWA KUTOKUWA NA HADITHI KWA MAJUMA MATATU
0 comments:
Post a Comment