`

Home » »
Na mwandishi wetu,

MUSOMA.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) umewataadhalisha wastafu kujiepusha ujumbe wa simu wanaotumiwa kuhusiana na michango yao na kuwataka kutuma fedha ili waweze kurekebishiwa kile kinachodaiwa kuwa ni mapunjo.

Tahadhari hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoani Mara Sudi Hamza wakati akizungumza na wafanyakazi wa idara mbalimbali za Serikali na watu binafsi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari(PSS).

Alisema katika siku za hivi karibuni kumeibuka watu wanaosadikiwa kuwa ni matapeli wakiwatumi wastafu na baadhi ya ujumbe kudai kuna mapunjo kwenye mafao yao hivyo watume kiasi cha fedha ili waweze kurekebishiwa mapunjo yao.

Sudi alisema hakuna ujumbe wa namna hiyo unaotumwa kutoka PSPF na tayari makao makuu umeshatoa taarifa kwa vyombo vya habari hivyo wasikubaliane na ujumbe unaotumwa.

Alisema tayari alishapokea taarifa kuhusiana na kutumwa kwa ujumbe huo na kuwasisitizia wastafu iwapo watapokea ujumbe wa namna hiyo kuwasiliana ofisi za PSPF Mara ama kumpigia simu yake ya mkononi ambayo wanachama wengi tayari alishawapatia.

Akizungumzia fursa zilizopo katika mfuko wa uchangiaji wa hiari(PSS)alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa benki.
mwisho..........

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK