WANANCHI WAOMBWA KUCHANGIA UJENZI WA MAABARA.
MJUMBE WA
HALMASHAURI KUU YA UMOJA WA VIJANA UVCCM WILAYANI BUTIAMA BW. MGINGI MHOCHI AKIZUNGUMZA NA MWALIMU MKUU WA SHULE YA SEKONDAR KYANYARI MWL. ANOLD SASI.
NA AHMAD NANDONDE,
BUTIAMA.
WANANCHI WAISHIO
KATIKA KATA YA KYANYARI WILAYANI BUTIAMA WAMEOMBWA KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KATIKA UCHANGIAJI
WA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KYANYARI ILIYOPO WILAYANI HUMO ILI KUTEKELEZA AGIZO LILILOTOLEWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
AKIZUNGUMZA KATIKA
ZIARA YAKE ALIYOFANYA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KYANYARI MJUMBE WA
HALMASHAURI KUU YA UMOJA WA VIJANA UVCCM WILAYANI BUTIAMA BW. MGINGI MHOCHI AMESEMA
PAMOJA NA HALI MBAYA KIUCHUMI LAKINI NI WAJIBU WA KILA KIONGOZI NA MWANANCHI MWENYE
UWEZO HUSUSANI AMBAO HAWAJACHANGIA KUJITOKEZE ILI KUSAIDIA KUKAMILIKA KWA UJENZI HARAKA.
AKIONESHA
KUGUSWA KWAKE NA UMUHIMU WA UPATIKANAJI WA MAHABARA BW. MHOCHI AMETOA
MSAADA WA MIFUKO MITANO YA SARUJI PAMOJA MCHANGA LORI TATU ILI UJENZI HUO WA MAABARA UWEZE KUKAMILIKA KWA MUDA ULIOKUSUDIWA.
NAYE MWALIMU
MKUU WA SHULE HIYO BW. ANOLD SASI AMEKIRI KUWAPO KWA TATIZO HILO LA UKOSEFU WA LA MAABARA HALI INAYOWALAZIMU KUTUMIA DARASA DOGO LENYE VIFAA VICHACHE
AMBAVYO HAVIKIDHI MAHITAJI YA WANAFUNZI HAO HALI INAYOPELEKEA WANAFUNZI KUFANYA MITIHANI
YAO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
AKIZUNGUMZA KWA
NIABA YA WANAFUNZI WENZAKE SHULENI HAPO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU A (MCHEPUO WA SAYANSI) SPRINA JOSEPH AMESEMA KUWEPO
KWA UFINYU WA MAABARA KUMEPELEKEA KUVUNJIKA MOYO KWA BAADHI YA WANAFUNZI HIVYO
KUYAKIMBIA MASOMO HAYO KWENDA KATIKA MASOMO YA MCHEPUO WA ARTS KITU AMBACHO AMESEMA
KAMA KITAENDELEA BASI UPO UWEZEKANO WA TAIFA KUPOTEZA WANASAYANSI WENGI HUSUSANI WATAALAMU
WA TIBA HAPA NCHINI.
ITAKUMBUKWA KUWA
MNAMO MWEZI JULAI MWAKA HUU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA
KIKWETE ALITOA AGIZO KWA WAKUU WOTE WA MIKOA NA WILAYA HAPA NCHINI KUHAKIKISHA
WANASHIRIKIANA NA WANANCHI ILI KILA SHULE YA SEKONDARI KATIKA MAENEO YAO, INAKUWA
NA MAABARA KWA AJILI YA MASOMO YA SAYANSI.
MWISHO......
0 comments:
Post a Comment