NA
AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
IMELEEZWA KUWAUPUNGUFU WA WALIMU
WA MASOMO YA ALAMA KWAAJILI YA KUFUNDISHA WATOTO WENYE ULEMAVU WAKUONGEA NA KUSIKIA NDIYO CHANGAMOTO KUBWA INAYOPELEKEA WATOTO KUTOHITIMU ELIMU YA
SEKONDARI.
HAYO YAMESEMWA NA MTOTO SALMA
ALLY KUTOKA SHULE YA MSINGI AZIMIO ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WANAFUNZI WENZAKE WAKATI WA UFUNGWAJI WA MAFUNZO YA BARAZA LA WATOTO WENYE ULEMAVU NA WASIO NA
ULEMAVU MKOANI MARA AMBAYO YAMEENDESHWA NA KANISA LA FREE PENTECOSTAL CHURCH OF
TANZANIA (FPCT) HAPA NCHINI.
SALMA ALLY
AMESEMA KUWA KATIKA MAISHA YAO WATOTO WENYE ULEMAVU WAMEKUWA WAKIKABILIWA NA
UKOSEFU WA USAWA, KUBAGULIWA, KUTOKUWA NA HAKI YA KUISHI HUSUSAN KWA WALIEMAVU
WA NGOZI AMBAO HUKABILIWA NA VITISHO VYA KUKATWA VIUNGO VYAO IKIWA NI PAMOJA NA
MIUNDO MBINU ISIYO RAFIKI KWAO HALI INAYOPELEKEA KUACHA MASOMO.
NAYE MEYA WA
MANISPAA MUSOMA AMESEMA KUWA ILI KUHAKIKISHA WANAWAJALI WATOTO HAO AMESEMA KUWA
HAMLMASHAUR YA MANISPAA YA MUSOMA INAJITOLEA KWA NAMNA YOYOTE KATIKA KUWALINDA
NA KUWAJALI WATOTO HAO NA HIVYUO AMEAHIODI KUENDELEA KUTIOA USHIRIKIANO WA
KUTOSHA KWA WATOTO HAO.
KWA UPANDE WAKE MWENYEKITI
WA BARAZA LA KAMATI YA KULEA WATOTO WENYE ULEMAVU MKOA WA MARA AMBAYE PIA NI
ASKOFU WA KANISA HILO MKOA WA MARA STEPHEN LUGONGO AIMEITAKA SERIKALI
KUTEKELEZA KWA VITENDO HAKI ZA WATOTO WENYE ULEMAVU KAMA ZILIVYOAINISHWA KATIKA
SHERIA ZINAZOWALINDA WATOTO KAMA KATIBA YA NCHI ILI KUWSAIDIA KUPATA HUDUMA ZAO
MUHIMU WANAZOZIKOSA.
HATA HIVYO
SERIKALI MKOANI HAPA KUPITIA KWA KATIBU TAWALA MKOA BW. BENEDICT OLE KUYAN
IMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALI MBALI KUWEZESHA UUNDWAJI WA BARAZA LA
WATOTO WENYE ULEMAVU NA WASIO NA ULEMAVU ILI WATOTO WAWEZE KUPAZA SAUTI ZAO NA
HIVYO KUSAIDIA HAKI ZAO ZINALINDWA.
MWISHO.....
0 comments:
Post a Comment