NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
KUWAPO
KWA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA,UWAZI, UWAJIBIKAJI, UFANISI KATIKA KAZI NA HUDUMA
BORA YAMEELEZWA KUWA NDIYO KIASHIRIA CHA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI WAKUU HAPA
NCHINI.
HAYO
YAMESEMWA LEO KATIKA HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI UTAWALA BORA KAPT.
GEORGE MKUCHIKA KATIKA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA MARA UNAOENDELEA
KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MWEKEZAJI ULIOPO MJINI MUSOMA.
AKISOMA
HOTUBA HIYO MWENYEKITI WA MKUTANO HUO AMBAYE AMEMWAKILISHA KAIMU MKUU WA MKOA
WA MARA ENG. EVARIST NDIKILO AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA MUSOMA BW.
JACKSONE MSOME AMESEMA KUWA MAPAMBANO KATIKA DHIDI YA RUSHWA MA MAMBO MENGINEYO
KWAMWE HAVIWEZI KUWAPO IWAPO HAKUTAKUWA NA WATENDAJI WAADILIFU.
AIDHA
AMESEMA KAMA KUNAHITAJIKA KUWAPO KWA WATENDAJI WENYE UADILIFU NI LAZIMA HATUA
ZA MAKSUDI ZICHUKULIWE NA SERIKALI, WAFANYAKAZI NA JAMII NZIMA KATIKA KUJENGA
NA KUZINGATIA MAADILI NI WAZI KUWA HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA KWA WANANCHI ZITAKUWA
NA UBORA ZAIDI NA WENYE KUTENDA HAKI.
AMESEMA
IKIWA JAMII ITAZINGATIA MAADILI NI DHAHIRI KUWA MIENENDO MIBAYA YA IKIWA NI
PAMOJA NA ISHIRIKI KATIKA VITENDO VYA RUSHWA VITADHIBITIWAHIVYO KAMA JAMII
INATAKA KUONDOKA NA TABIA HIZO SERIKALI INAAMINI KUWA UJENZI WA NA UIMARISHAJI
WA UTAWALA BORA NDIYO NJIA SAHIHI NA YA UHAKIKA WA KATIKA KUPINGA RUSHWA,
UMASKINI NA UENDESHAJI MBOVU WA HUDUMA ZA UMMA.
NAYE MKURUGENZI
WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU MKOANI MARA BW. HOLE
MAKUNGU AMESEMA KUWA TAASISI YAKE IMEKUWA IKIKABILIWA NA KESI MBALI MBALI
HUSUSANI RUSHWA ZA NGONO AMBAPO WALIMU KULAZIMISHWA KUTOA RUSHWA YA NGONO NA
MAAFISA ELIMU NA ANAPOKATAA HUTISHIWA KUPELEKWA VIJIJINI NA HIVYO KUAHIDI
KUANZA KULISHUGHULIKIA SUALA HILO.
0 comments:
Post a Comment