NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
SERIKALI MKOANI
MARA LEO IMEAGIZA KUKAMATWA KWA BASI LA KAMPUNI YA BATCO ILI KUTOA MAELEZO
KUFUATIA MAANDASHI YALIYOANDIKWA KWENYE BASI HILO AMBAYO YANAWAKEJELI WAKAZI WA
MKOA WA MARA NA ABIRIA WANAOSAFIRIA BASI HILO.
HAYO AMEYASEMA
LEO NA MUWAKILISHI WA KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA
YA TARIME BW. JOHN HENJEWELE KATIKA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOANI MARA
KILCHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MWEKEZAJI MKOANI HAPA.
HENJEWELE AMESEMA
KUWA KUTOKANA NA MAANDISHI YALIYOANDIKWA KATIKA BASI LA KAMPUNI YA BATCO KUWA
MAANDISHI YANAYOSOMEKA "MKOMBOZI WA WANAMARA" NI WAZI KUWA
INAONESHA JINSI GANI WATU MKOA WA MARA HUSUSANI ABIRIA WANAOFANYA SAFARI ZAO
KWA KUTUMIA BASI HILO WASIVYOTHAMINIWA NA KAMPUNI HIYO.
AIDHA AMEONGEZA
KUWA KUKAMATWA BASI HILO KUTAKUWA MFANO KWA WENYE MABASI WOTE WENYE TABIA YA
KUANDIKA MAJINA HAYO ILI IWE FUNDISHO KWA MABASI MENGINE YENYE TABIA KAMA HIYO.
AIDHA MKUU HUYO
WA WILAYA YA TARIME AMBAYE HII LEO AMEMUWAKILISHA KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA
AKAWATAKA WAMILIKI WA MABASI KUWA NA MOYO WA UZALENDO KUMTHAMNI MTEJA HALI
ITAKAYOMFANYA MSAFIRI KUWA UHURU AWAPO SAFARINI.
HATA HIVYO
HENJEWELE AMEITAKA MAMLAKA YA USAFIRI WA MAJINI NA NCHI KAVU SUMATRA
KUHAKIKISHA INAYAFANYIA UKAGUZI YAKINIFU MABASI YA USAFIRISHAJI WA ABIRIA KABLA
YA KUYAPATIA KIBALI CHA USAFIRISHAJI.
DC amepotoka. Na maamuzi kama haya yanavuruga amani ya nchi. Sioni ni kiasi gani neno Mkombozi wa Wana Mara ni matusi au machukizo kwa abiria!!
ReplyDelete