JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA WAANDISHI
WA HABARI – 16.03.2015
AJALI YA MOTO NA
KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI:
Ndugu Waandishi wa habari; Mnamo tarehe 15.03.2015 majira ya 11:00hrs, huko maeneo ya kijiji cha Buswahili, Kata ya
Buswahili, Tarafa ya Kiagata, Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara. Kandokando ya
Mto Mara uliwaka Moto katika matete yaliyokauka na kuenea eneo kubwa.
Katika tukio hilo baadhi ya watu waliokuwa katika shughuli zao
waliathiriwa na kusababisha vifo vya watu wawili wanaofahamika kwa majina ya:- 1. KIRARYO S/O MARWA, miaka 14yrs, mwanafunzi wa shule ya msingi Buswahili, 2.TARANGWA S/O
ELIAS, miaka 11yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili ambaye
alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Aidha katika tukio hili watu watatu walijeruhiwa sehemu mbalimbali za
miili yao ambao ni;- 1. GHATI W/O CHACHA, miaka 40yrs, mkazi wa
Buswahili aliyekuwa anapata matibabu katika Hospitali ya Kongoto na ameruhisiwa
na hali yake inaendelea vizuri 2. LISO S/O MAGABE, miaka 16yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili, 3. MAGWAIGA
S/O ZAKARIA, miaka 14yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili.
Wavuvi wa kijiji cha Kongoto waliwasha moto huo majira ya 11:00hrs kwa ajili ya kuwawezesha kusafisha eneo la
kuvulia samaki na ndipo moto ulisambaa eneo kubwa na kufika eneo ambalo
walikuwepo marehemu pamoja na majeruhi ambao nao walikuwa wanatafuta eneo la
kuvulia samaki na kuwazunguka na wakashindwa kujiokoa na kupata madhara hayo.
Moto huo uliokuwa unasambaa kwa kasi kuelekea katika makazi ya watu
ulizimwa iliusielekee katika makazi ya watu kwa ushirikiano wa Askari wa Jeshi
la Polisi, Wananchi wa eneo hilo na Askari wa Kikosi cha Zimamoto cha Manispaa
ya Musoma Mjini.
Mwili wa Marehemu KIRARYO S/O MARWA umekwisha kabidhiwa kwa ndugu
zake kwa ajili ya mazishi na Mwili wa TARANGWA S/O ELIAS umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara na Majeruhi wawili
wamelazwa Hospitalini hapo wakiendelea na Matibabu. Hakuna mtu yeyote
anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi Kuhusiana na tukio hilo.
WITO.
kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,
anatoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto wao pindi wanapotoka majumbani kwenda
kucheza au katika shughuli zingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuwapata na
kusababisha vifo au hata ulemavu kwao, Pia anawataka wavuvi kuwa makini
wanapochoma moto kwa ajili ya shughuli zao za uvuvi ili kuepusha madhara
yasababishwayo na moto.
PHILIP
ALEX KALANGI- ACP.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MARA-MUSOMA.
0 comments:
Post a Comment