Na mwandishi wetu,
Tarime.
JAMBAZI lililodaiwa kuhusika na mauwaji ya hivi karibuni Wilayani Tarime na kisha kutoroka na kukamatiwa Mkoani Tanga April 6 2014 Mahabusu Charles Range Kichune au Charles Joseph Msongo (38) Mkazi wa Kenyamanyori –Tarime limefaliki dunia na mwili wake uko katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Halmashauri Wilaya ya Tarime.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisema kuwa marehemu huyo amefariki February 9, 2014 majira ya saa kumi usiku ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri Tarime.
Kamugisha alisema kuwa marehemu huyo alikuwa amekamatwa kwa kuhusika na matukio ya mauwaji ya watu kwa kutumia silaha amefariki dunia akiwa hospitali hapo akiendelea kupata matibabu.
Kamugisha aliongeza kuwa marehemu aliugua akiwa mahabusu na alipelekwa hospitali na baada ya kupimwa aligundulika ana ugonjwa wa pumu nakwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwa uchunguzi zaidi nakwamba tayali watu 20 wamekamatwa kwa kujihusisha na ujambazi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime Robert onesmo alisema kuwa marehemu alifikishwa hospitali hapo majira ya saa kumi alfajiri ambapo hata hivyo muda mfupi alipoteza maisha na na mwli wake uko chumba cha kuhifadhia maiti.
Hata hivyo vyanzo vya habari vinasema kuwa marehemu alikuwa na upungufu wa akili nakwamba hawa wakati anahojiwa sababu za kufanya mauwaji alisema hayo ni matokeo na kukili kuhusika kwenye mauwaji hayo ambapo baadae akiwa anaendelea kuhojiwa alikataa kuendelea kusema chochote.
Baadhi ya wananchi Wilayani Tarime wameisifu serikali kwa kuhakikisha majambazi yamekamatwa”kwakweli polisi wamefanya kazi kubwa lazima wapongezwe kwanza tunafurahi kusikia jambazi sugu limekufa kwani huwenda lingepelekwa mahakamani lingeachiwa maana alishawahi kufanya matukio ya mauwaji akafungwa miaka 30 akaa miaka 6 jera baadae akaachiwa tukamuona mitaani,tunajua tayali alishahojiwa akawataja wenzake unyama kwa unyama sasa Tarime wanaume tutaanza kutembea barabarani usiku kwakuwa muhusika kauwawa”alisema Mwita Marwa Mkazi wa Tarime.
Pia Gabson Richard Machumbe (27) aliyekuwa akipata matibabu katika hospitali ya Bugando Mkoani Mwanza ambaye alijeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili wake na jambazi lililofanya mauwaji Tarime amekufa wakati akipatiwa matibabu na mwili wake umezikwa kijijini kwao February 2014 Mtaa wa Rebu kata ya Turwa Wilayani Tarime
Mwisho,,,,,,,,,,,
JAMBAZI LILILOKAMATWA TANGA
0 comments:
Post a Comment