`

Home » » MAMIA WAMZIKA OMARY CHANGA NI ALIYEWAHI KUWA MCHEZAJI WA YANGA, VIJANA NA MORO UNITED ENZI ZA UHAI WAKE.

MAMIA WAMZIKA OMARY CHANGA NI ALIYEWAHI KUWA MCHEZAJI WA YANGA, VIJANA NA MORO UNITED ENZI ZA UHAI WAKE.

Mchezaji aliyewahikutamba na klabu ya soka ya Yanga OMMRY CHANGA amezikwa jana Jumatatu jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar es Salaam huku kifo chake kikiacha maswali mengi ya utata kuliko majibu.

Kwa mujibu wa kaka wa Changa, ambaye alikuwa mchezaji wa Moro United iliyoshuka daraja, kaka wa marehemu Idd Kambi, alisema kuwa kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na daktari imeonesha kuwa Omar Changa alichomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na kilichotokeza mbele ye tumbo huku pia shingo ikionekana kulegea.

“Mpaka sasa tumemaliza mazishi, lakini bado tuna huzuni kuhusu hii ripoti tuliyopewa, tunachofanya tunafuatilia ni timu gani aliichezea mara ya mwisho kwa sababu inaonekana inafichwa, lengo ni kujua mazingira ya mchezo yalikuwaje.”

Mdogo huyo wa marehemu alisema Omar Changa alimpigia simu Jumamosi iliyopita, akimtaka kwenda naye kushuhudia anavyocheza ndondo mchangani maeneo ya Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Changa alifunga bao moja la ushindi kwa penalti.

Mchumba wake marehemu aliyetambulika kwa jina la Sarah Mahemba alisema Changa hakurudi kwake tangu alipoondoka Jumamosi kuelekea Kigamboni katika mchezo huo, jambo ambalo liliwapa shaka wapangaji wenzake siku ya Jumapili na kuamua kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi lakini haikupatikana ingawa yeye aliijaribu na kukuta ikiita bila kupokelewa mpaka alipopata taarifa za kifo kupitia mdogo wa mshambuliaji wa Mbeya City, Omari Kijuso.

Mwili wa marehemu ulipatikana katika mtaro, maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mchezaji huyo aliyekuwa na umbo lililokuwa likiendana na nafasi yake katika soka inasemekana alinyongwa na watu wasiojulikana pamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na ubavuni

Blog ya jicho la mdadisi inapenda kutoa pole kwa ndugu, familia, Tff na marafiki wa marehemu kwa msiba huo mkubwa uliowafika.

Innalilah wainnailayh rajiuun.



PICHANI WATU WAKIENDA KUMPIMZISHA MAREHEMU CHANGA.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK