IMEELEZWA kuwa viongozi VIONGOZI ambao ni wasimamizi wakuu wa rasilimali ya ziwa Victoria na mazingira yake wanadaiwa kuwa chanzo cha kuendekeza uvuvi usio hitajika(haramu) na uharibifu wa mazingira ya ziwa hilo.
Haqyo yalidaiwa na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa wakati akizungumza na baadhi ya wadau wa uvuvi ziwa Victoria kwenye kikao cha wadau wa uvuvi kilichofanyka katika ukumbi wa uwekezaji wa mkoa huo mjini Musoma.
Tupa alidai kuwa kamati za ulinzi na usalama za maeneo husika wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwakamata wahusika kwa kile alichodai kuwa wahalifu wamekuwa wakipokea taarifa kutoka kwa viongozi wasimamizi wa mialo na ofisi za samaki.
“Hawa viongozi wa mazingira,afisa uvuvi,na viongozi wanaohusika na usimamizi wa rasilimali za ziwa(BMU),nahisi ndio tatizo,kwani endapo kutakuwa na msako huwezi kuwakamata wahalifu wanaoharibu mazalia ya samaki wala wanaotumia dhana zisizohitaji ziwani”alisema Tuppa.
Aidha Tuppa aliwataka wadau na viongozi wote kushirikiana katika kuonesha msimamo wa usimamizi ili kulinusuru ziwa Victoria ambalo alidai kuwa kwa sasa linazalisha samaki chini ya kiwango hali ambayo alisema linaikosesha serikali mapato na kudidimiza ajira kwa vijana.
Nae afisa mfawidhi ulinzi wa rasilimali za uvuvi mkoani hapo Braison Meela wakatia kitoa mada alisema kuwa mapato ya serikali yatokanayo na uvuvi yameshuka kufuatia kupungua kwa samaki hususani samaki aina ya Sangara kwa sailimia 51.
Meela alidai kuwa viwanda vya samaki vinazalisha kwa kiwango cha chini ya asilimia 50 ya uwezo wa viwanda,hivyo kushindwa kikidhi mahitaji ya wateja wa ndani na nje.
Alisema kuwa sababu kubwa inayochangia kupungua kwa samaki ni uvuvi usio endelevu ambao unafanywa kinyume na mujibu wa sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni za uvuvi za mwaka 2009,kwa maana ya uvuvi haramu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment