`

Home » » WANANCHI TARIME WIOMBA SERIKALI KUWAONESHA MPAKA WA MURITO NA GIBASO.

WANANCHI TARIME WIOMBA SERIKALI KUWAONESHA MPAKA WA MURITO NA GIBASO.

Na mwandishi wetu,

Tarime.
 
WANANCHI wa Kijiji cha Murito Kata ya Kemambo -Nyamongo Wilayani Tarime  wameitaka Serikali kuwaonyesha mipaka inayotenganisha  kijiji cha Murito na Gibaso Kata ya Nyarukoba ili kunusuru uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza kwa wananchi.
 
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Keisankwe Kijiji cha Murito Charles Makore (38) amesema kuwa walishapeleka malalamiko Halmashauri ya Wilaya na ofisi ya Mkuuwa Wilaya ya Tarime John Henjewele lakini hadi sasa mgogoro haujatatuliwa wala wananchi kuonyeshwa mipaka ya vijiji hivyo.
 
Ofisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Jeremia Minja amesema kuwa maeneo mengi Wilayani hapa yanakabiliwa na migogoro ya radhi na mipaka na Halmashauri haina wataalamu wa ardhi ispiokuwa yeye  pekee ambaye ni Mkuu wa Idara ya ardhi na hivyo kusababisha kutoyafikia maeneo yote yenye mgogoro na kuhaidi kuwa atajitahidi kulitatua tatizo hilo.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Othuman Akalama amesema kuwa anatambuwa kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi na mipaka ila tatizo kubwa ni halamshauri kutokuwa na wataalamu wa ardhi ambao wangesaidia kupunua kwa migogoro nakwamba walishaomba serikali iwapatie wataalamu nab ado hawajapata.
 
MWISHO......................

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK